webnovel

chapter 6

Tulya anajizoa pale chini nakusimama anasogea karibu na yule mwanaume aliyemsukuma na kumwangalia kwa hasira, mwanaume nae anamwangalia tulya kwa mshangao na hasira juu yake "unafanya nini"wote Wanaongea kwa pamoja.Sinde anatoka katika Hali ya mshtuko na kukimbia pale alipo tulya "tulya acha tuondoke bwana" anaongea sinde kwa sauti ya chini lakini tulya anausukuma mkono wa sinde uliokuwa umemshika "sitoki hapa,mpaka aseme yeye nani kumtupa mtu namna ile, kidogo anivunje kiuno" tulya asiyekubali kushindwa pale anapoona anaonewa alikuwa bado Yuko mbali kabisa kumwacha mtu huyu aondoke hivihivi tu pasipo kumalizana nae ipasavyo "haya sema tatizo lako nini,kwanini unibwage namna ile ningeumia je?" anaongea tulya akishika kiuno.

Lakini badala ya kujibu yule mwanaume Anacheka kwa dharau tulya anabaki anashangaa na kujiuliza kinachomchekesha nini badae akili inakuja kuwa yule mtu amelewa anaona huu ugomvi utakuwa ni Bure tu, akijua kugombana na mlevi ni sawa na kuongea na kunguru "siku nyingine kama umelewa kalale sio Kuja kusumbua watu twende" tulya anamshika mkono sinde na kutaka kuondoka lakini yule mwanaume anamvuta mkono na kumrudisha

"sikia we mwanamke,siku nyingine kama unataka kujitupa katafute mwanaume mwingine sio Mimi,umeona mpango wako umeanguka unataka kujifanya uko sawa na kuondoka ila umekwama,mwanamke kama wewe kwangu ni kama jiwe tu" watu wote wanacheka wakati huo tulya akijaribu kuzungusha akili yake kukielewa kile alichokisema yule mwanaume "tulya twende" sinde anamvuta tulya,lakini miguu ya tulya haikusogea alipo alikuwa kama kachimbiwa, hii inafanya sinde ashike kichwa "subiri kidogo,kwa hiyo akili yako yote inakutuma kuwa Mimi nilikuwa najitupa kwako?!" "kwani uongo?" anajibu yule mwanaume na Sasa ikawa zamu ya tulya kucheka na kufanya watu kukaa kimya "sikiliza we kijana sijui wewe ni nani mpaka kujiamini hivyo ila kwa sababu umelewa utakuwa hukuona vizuri Kuna mtu alinisukuma ndio maana niliangukia mikononi mwako asante sana kwa kunidaka"anatulia kidogo kama anakumbuka kitu nakuendelea "aaa hukunidaka ulinitupa kwa hiyo narudisha asante yangu na kitu kingine hiki ndo Cha muhimu zaidi, hata wanaume wote wakiisha hapa duniani siwezi kujitupa kwako,mtu mwenyewe mlevi,hujielewi nawaonea huruma hao wanawake wanaojitupa kwako watakuwa hawana macho hata kidogo"anaongea tulya akiwa fanya watu wakae midomo wazi kwa mshangao.

tulya anazidi kumporomoshea mvua ya maneno yule mwanaume kitendo kilichowafanya watu wote washangae kwani huyu mwanaume hajawahi kupandishiwa sauti na mtu " unasemaje wewe?!" yule mwanaume anauliza akimfuata tulya kwa hasira lakini kabla hajafika sinde anaingilia " samahani sana, ndugu yangu akili zake kama sio nzuri" yule mwanaume anasimama baada ya kumuona sinde " nani Hana akili nzuri wewe sinde?!" tulya analipuka kwa mshangao na hasira kuona ndugu yake akimtoa akili Mbele za watu lakini sinde hakumpa nafasi akimvuta kwa nguvu nakuanza kuondoka nae lakini tulya alikuwa ni mbishi bado akitaka kurudi kumaliza ugomvi.

baada ya kutoka eneo la ngoma sinde anamwachia tulya mkono "afadhali,kidogo univunje mkono haya kitendo Cha kunitoa akili Mimi pale nini?" anauliza tulya akiuangalia mkono wake " unatakiwa kunishukuru nimekutoa pale la sivyo ungekuwa huna kichwa hapo ulipo" anaongea sinde akimnyoshea tulya kidole kuonyesha kichwa chake,tulya anashtuka "kwani yule nani nimemtukana mtemi au" "sio mtemi huyo ni kiongozi wa wawindaji wa Kijiji chetu" anamweleza sinde"aaa nilijua mtemi,halafu kwani kiongozi wa wawindaji anaruhusiwa kuua watu" anauliza tulya wakianza kutembea na sinde anacheka " kumbe unaogopa kufa" "nani anayetaka kufa" anajibu tulya akiendelea kumkumbuka huyo kiongozi wa wawindaji "haruhusiwi kuua,ila huku kwetu viongozi wa kuwinda wanaheshimika kama mtemi sababu wao ndo wanaotulisha,ila manumbu hachelewi kukuua yule Kila mtu anamuogopa,kwa hiyo jifunze kufunga mdomo wako huo ipo siku utakutia matatizoni" anaonya sinde

"najua lakini hasira zikishafika kooni mdomo wangu hutembea wenyewe pasipo ridhaa yangu" sinde anacheka kwa nguvu kutokana na jibu la tulya "utakuja juta siku moja" sinde anamaliza kucheka na kuendelea "watu walikuwa wanataka nzagamba ndo awe kiongozi lakini ndio hivo haikuweza" tulya kusikia jina la nzagamba anakumbuka Jana mama yake alimsimulia lakini hakumuelewa na alisema atamuuliza sinde Mambo yakawa mengi akasahau" eheee nimekumbuka mama aliniambia Jana tulipokuwa mtoni kuhusu huyo nzagamba sema sikumuelewa imekuwaje akawa Hana bahati?" " ulimsikia akipiga kalimba ee" tulya anaitikia kwa kichwa akiendelea kutembea " anapiga vizuri zamani kabla haijajulikana kama hana bahati tulikuwa tunafurahia sana muziki wake wa kalimba na malimba Siku hizi tunamsikia akiwa mtoni tu na hivyo mara Moja sana" " we niambie kwa nini hana bahati" anaongea tulya uvumilivu ukimshinda.

"Hana bahati kwa sababu anaharufu ambayo wanyama hawaipendi hivyo akienda porini hakutani hata na sungura,anauwezo wa kutembea pori Zima na akarudi bila kudhurika" anafafanua sinde "kwa hiyo ananuka " sinde anacheka kutokana na swali la tulya " hapana hanuki ila hiyo harufu wanaisikia wanyama tu,maskini nzagamba anakila kitu chakuitwa mwanaume rijali lakini Sasa ataishi peke yake maisha yake yote" sinde anaongea kwa masikitiko "nimesikia hawezi kuoa" anauliza tulya " sio kama hawezi kuoa wanawake hawataki kuolewa nae kwa kuhofia kuishi maisha ya shida,alikuwa na mchumba baada ya kutokea kwa matatizo mchumbaake akamuacha na kuolewa na manumbu akijua kuwa manumbu na nzagamba walikuwa hawapatani"

"manumbu? aaah yule mlevi wa mda ule" anauliza tulya kupata uhakika " ndio,manumbu alikuwa anampenda lindiwe lakini baba yake lindiwe akaamua lindiwe aolewe na nzagamba,baada ya nzagamba kupata matatizo lindiwe na baba yake wakabadili mawazo na kuvunja uchumba" moyo wa tulya unakuwa mzito kama umebeba kitu kizito akimwonea huruma nzagamba akiamini kweli watu wanaweza kukukimbia wakati wa matatizo.

kama ilivyokuwa Mila na desturi za jamii ya wawindaji na katika himaya nzima ya mpuli vijana wote pindi wafikiapo umri wa kwenda jando huanza kuandaliwa kwa ajili ya kukabiliana na majukumu ya kifamilia pamoja na namna ya kuitumikia himaya yao.baada ya kutoka jando vijana wote huingia kambini kujifunza namna ya kutumia silaha mbalimbali na namna ya kupigana kwa ajili ya kulinda himaya Yao endapo siku Moja itavamiwa.

katika kundi la vijana walioingia kambini miaka yote haijawahi kutokea kijana aliyekuwa anajiweza na kujiamini kama nzagamba alikuwa akiwaongoza wenzake kwa Kila hatua ya mazoezi waliopitia uhodari wake wa kurusha mishale na mikuki uliwafurahisha viongozi.waliweka matarajio makubwa juu yake wakijua himaya itakuwa na kiongozi Bora katika nyaja ya uwindaji na angeweza kuwa kiongozi Bora katika ulinzi kutokana na uhodari wake wa kupigana.

kiongozi wa uwindaji wa himaya mwaka huo mzee makoko aliyekuwa amezeeka akitarajia kuachia ngazi baada ya kusikia habari za nzagamba alienda Hadi Kambi ya vijana ya Kijiji Cha rumo alikokuwa nzagamba na kumpima aligundua kuwa nzagamba angekuwa kiongozi Bora sababu alikuwa ni mtulivu asiyefanya maamuzi ya haraka na alitumia busara nyingi sana katika kuamua jambo.

Hivyo alimwambia mtemi kuwa nzagamba akimalizia mafunzo atamfanya kuwa mrithi wa Cheo chake huku Kijiji Cha rumo nacho kilimtegemea sana kuwa kiongozi wao wa uwindaji kijijini.baba yake lindiwe ambaye Moja ya viongozi wa ulinzi katika himaya ya mpuli alipopata habari za nzagamba kuwa atakuwa kiongozi wa wawindaji wote pindi tu amalizapo mafunzo aliwahi na kupeleka posa kwa nzagamba Ili amuoe Binti yake.

Nzagamba alipomuona lindiwe alimpenda sana hivyo akiikubali ile posa lindiwe nae alimpenda nzagamba.

Muda ulipofika wa kuhitimu mafunzo kama ilivyo ada vijana wote huachiwa porini kwenda kuwinda na kuangaliwa Kila kijana atarudi na ngozi ya mnyama gani,atakaye winda Simba au chui hupata Cheo kikubwa sana katika kasri ya mtemi na huwa shujaa wa wengi. vijana wanaoenda kuwinda hukutana na changamoto mbalimbali kwani hupewa siku tatu mfululizo za kukaa porini na kila mtu anakaa peke yake na Kuna wengine hupoteza maisha kwa kuzidiwa nguvu na wanyama wakali.

Baada ya kukaa porini kwa siku tatu siku ya nne vijana wakianza kurudi Kila Mmoja akiwa na ngozi ya mnyama aliyewinda. mpaka jioni vijana wote walishawasili isipokuwa nzagamba ambaye alikuwa hajarudi wasiwasi ukaanza kuingia miongoni mwa watu akiwemo mama yake wakihofia endapo atakuwa kauwawa na wanyama wakali.ilipofika usiku zaidi walimuona akirudi akiwa Hana kitu zaidi ya silaha zake alizobeba watu wote walishangaa,viongozi walienda kumuuliza mnyama aliyewinda Yuko wapi wakashangazwa na jibu lake kuwa hakupata kitu.hiyo ilizua taharuki.

kesho yake wazee walimuita nzagamba na kumhoji zaidi ni kitu gani kilitokea huko porini, nzagamba akawaambia ukweli kuwa alitembea kwa siku tatu zote na hakukutana na mnyama yeyote,baada ya kusikia hivyo wazee wote walitazamana,lakini kwa sababu walikuwa wanampenda sana nzagamba walimpa siku tatu zingine za kurudi porini lakini matokea yakawa yale yale .

wazee walikuwa wameshajua tatizo nini ila walikuwa wanahitaji kufanya uhakika wa kitu ambacho walikuwa wakikisikia kama hadithi tu, hakijawahi kutokea wakakiona katika maisha Yao inasemakana kuwa zamani hizo za kale kuliwahi kutokea kwa mtu mwenye tatizo kama la nzagamba na halikupata dawa.

baada ya wazee kumrudisha nzagamba porini mara tano iliwabidi kutoa uamuzi wa nini kilichokuwa kikiendelea kwani watu wote walikuwa wakisubiri baada ya tatizo la nzagamba kutangazwa Kuna waliohuzunika sana na waliofurahi.watu waliopata furaha kubwa zaidi alikuwa ni manumbu aliyekuwa mpinzani mkubwa wa nzagamba kwani alikuwa hampendi na kilichomfanya amchukie zaidi yeye pia alikuwa anampenda lindiwe na alikuwa wa kwanza kumuona.

Tofauti na nzagamba mara ya kwanza kumtia lindiwe machoni ilikuwa ni usiku walipotoroka kambini na marafiki zake kwenda ngomani alipomuona tu alimpenda na kumwambia baba yake apeleke posa baba yake aliporudi alileta jibu kuwa baba yake lindiwe tayari alikuwa na mtu anayetaka mwanae aolewe nae.baadae alikuja kugundua kuwa mtu huyo alikuwa ni nzagamba hivyo alimchukia zaidi.

Tatizo la nzagamba lilimpatia nafasi ya kwenda kumrubuni baba yake lindiwe na kubadili mawazo na kutaka lindiwe aolewe na manumbu licha ya lindiwe kumpenda nzagamba hakuwa tayari kwenda kinyume na baba yake hivyo alikubali kuvunja uchumba nakuolewa na manumbu.manumbu aliwekwa kuwa kiongozi wa wawindaji Kijijini lakini hakuwa peke yake kwani yeye aliwinda faru pamoja na kilinge nae aliwinda faru hivyo kuwafanya kuwa na maksi sawa uongozi ukaamua kuwagawanyisha makundi Kila mtu akawa na kundi lake la kuongoza pasipo kuingiliana.

Nzagamba ambaye tayari roho yake ilikuwa imepasuka kwa kuambia Hana bahati ya kuwinda wanyama hawampendi alikuja kuvunjika moyo mara kumi zaidi baada ya mwanamke aliyekuwa anampenda kuvunja uchumba.roho ilimuuma sana lakini hakuwa na namna nyingine ila kukubaliana na Hali yake iliyobadilika ghafla Mbele ya macho yake Kila kitu kilizima kama kandili iliyozimwa na upepo mkali alijikuta Yuko gizani tena kiza kinene.

kuanzia hapo hakuna mwanamke aliyetaka kuolewa nae tena na kumuacha kuwa kijana pekee ambaye hajaoa Kijijini na kutokuwa na malengo hayo pia, nzagamba alijitenga na Kila mtu na kubaki kuwa mtu wa peke yake tu kwa sababu hakuwa na rika la kujiunga,vijana wenzake waliomaliza nae mafunzo wote walioa na Kila siku usiku wakikutana na kuongea Mambo Yao mbalimbali kuhusu familia zao na jinsi mawindo yalivyoenda kama wakitoka porini.

na wale ambao hawajao wakizungumzia namna ya kufaulu mazoezi Yao au mchumba wa nani ni mzuri zaidi hii ilimfanya nzagamba kukosa kundi la kukaa kwani hadithi zao hazikuendana nae hivyo kubaki peke yake,mda mwingi aliutumia nyumbani au porini akitafuta ulimbo kwa ajili ya kwenda mtoni kuwinda ndege kwa ulimbo kujipatia kitoweo huku akijifariji kwa malimba yake.

Usiku ulikuwa mkubwa kwa tulya baada ya kujua kuhusu nzagamba Kila akijaribu kulala usingizi hauji moyo ukitamani kumjua nzagamba kwa sura.kesho yake mchana aliamua kwenda mtoni labda angesikia sauti ya malimba lakini kulikuwa kimya aliporudi nyumbani alimuuliza sinde kuwa hakusikia sauti ya malimba sinde alimjibu kuwa nzagamba haenda Kila siku mtoni.

zimepita siku tatu tangu tulya aende mtoni peke yake,Leo wakiwa njiani kuelekea mtoni na sinde wanakutana na kijana tulya asiyemjua anasimama Mbele Yao "unatuzuiaje njiani sogea tupite" anafoka tulya "mwache namjua huyu" sinde anajibu nakumfanya tulya kumwangalia kijana mara mbilimbili "ni mchumba angu huyu" anajibu sinde kumfanya tulya amwangalie vizuri kijana ambaye amekuwa akimsikia tu tangu aje hajawahi kumuona sababu alikuwa kambini lakini kafikaje hapa anajiuliza tulya na kumwangalia sinde

" katoroka huyu humuoni,Tinde huyu ni binamu yangu mtoto wa shangazi"anamtambulisha sinde,Tinde anatikisa kichwa kukubali " habari yako" anasalimia Tinde " nzuri tu ya kwako" "nzuri tu karibu" "asante" wanabadilishana salamu na wote sinde na Tinde wanabaki wakimwangalia tulya wakisubiri awaachie nafasi kidogo,tulya anawangalia nakushtuka "ooh Mimi natangulia utanikuta mtoni" anaondoka tulya akiwapatia nafasi ya kuzungumza sinde na Tinde.

Anafika mtoni nakuanza kuchota maji akiwa ananyanyua kibuyu kukitoa mtoni anasikia sauti ya malimba anashtuka, anaweka kibuyu pembeni nakuanza kusikiliza inatokea wapi alipoona amepata mwelekeo anaanza kutembea kwenye vichaka akielekea inakotokea sauti.