webnovel

chapter 5

"nzagamba"anajibu runde "anapiga vizuri kweli" anaitikia tulya akitengeneza ngata yake tayari kwa kujitwisha "ndio nzagamba Yuko vizuri kwa Kila kitu hata malimba anajua kupiga" runde anajibu huku akijitwisha kibuyu tayari na wanaanza kutembea.

Njiani tulya Kila akisikiliza mziki huo anaona kama Kuna kitu kimepotea anasikiliza zaidi na kugundua kuwa mziki huo haukuwa wa furaha,na anavyojua mziki unawakilisha ya moyoni mtu ambayo hawezi kuyasema kawaida anayasema kupitia mziki "mbona mziki ni wa huzuni?" anauliza tulya kwa sauti ya chini lakini runde anaisikia vizuri.

"ndio,kwa sababu anayepiga hana furaha" "kwa nini?"anauliza tulya akiwa na shauku ya kujua "nzagamba hawezi kuwinda tulya" tulya anawaza labda nzagamba atakuwa ni kilema ndo maana hawezi kuwinda "kwa sababu ni kilema" runde Anacheka kidogo kusikia tulya amewaza kuwa nzagamba ni kilema "hapana ni mzima kabisa afadhali hata angekuwa na ulemavu hiyo ingekuwa afadhali" tulya anaona mama yake anamchanganya tu,akijiuliza kama sio kilema inakuwaje hawezi kuwinda "Hana bahati ya kuwinda"anajibu runde kama aliona maswali yaliokuwa yakiendelea kichwani pake "bahati ya kuwinda?kwani kuwinda kunahitaji bahati mama?" kwa tulya aliyekulia katika jamii ya wafugaji alikuwa hajui Mambo mengi kuhusu jamii ya wawindaji kwake yeye kuwinda ni kubeba mkuki au upinde na mshale silaha yeyote ile ukikutana na mnyama unaua unapata nyama lakini alikuwa hajui kama Kuna Mambo mengine mengi ambayo mwindaji anatakiwa kuwa nayo ikiwemo bahati.

runde anamsikiliza tulya na kuendelea "wewe uliyekulia katika jamii tofauti hutaweza kuelewa,ila kwa kifupi ni kuwa mwindaji akikosa bahati ni sawa na mwiba kuingia mguuni Pako usiweze kuutoa usubiri mguu uote tende,hicho ndicho kilichomkuta nzagamba licha ya kuwa hodari kwa Kila kitu amekosa kitu kimoja tu 'bahati" tulya anaona mama yake runde anamchanganya tu Kila akizungusha ubongo wake hamuelewi hata kidogo "anatia huruma hapa Kijijini hawezi kuoa hawezi kujichanganya na rika lolote lile mda wote Yuko peke yake tu ndio maana anatumia kalimba kujifariji huyo ndio rafiki yake"

tulya anaona tatizo la nzagamba ni kubwa kuliko anavyofikiria lakini bado haelewi tatizo nini "kwa hiyo akiwa hana bahati ya kuwinda hawezi hata kuoa" anauliza tulya akihakiki alichokisikia "inakuwa ni vigumu kwa sababu uwindaji ndo unalisha familia je asipowinda atalishaje familia yake na ni Binti gani atakayekubali kwenda kula ndege maisha yake yote na hata kama akikubali nadhani wazazi wake hawawezi kukubali mtoto wao akateseke,Kila mtu anataka kulalia ngozi kavu mwanangu mbichi usingizi hauji' anaeleza runde "namwonea huruma tu bibi sumbo umri umeenda hana hata mka mwana wa kumtuma kumchotea maji" tulya hatii neno kwenye maneno ya mama yake runde kwani anajua hata akijaribu kuhoji zaidi kile anachotaka kukijua mama yake huyo hataongea kwa sababu huwa sio mwongeaji hivyo akaamua kukaa kimya akisema atamuuliza sinde amweleze zaidi kwani anajua Kuna zaidi ya hadithi kuhusu nzagamba na yeye Kuna kitu kinamtuma kutaka kujua zaidi.

"kimbia" sinde akiwa anakimbia usiku ulioangaza mbalamwezi ukiacha hatua chache tu kulingana na mchana "nimechoka Mimi" tulya aliyekuwa ameachwa nyuma hatua chache anaanza kutembea sinde naye anasimama akiinama na kuweka mikono yake magotini kujipumzisha tulya anafika mpaka Mahali alipo sinde huku akihema "yaani wewe hujiwezi kabisa tukikimbizwa na fisi utakamatwa wa kwanza"anaongea sinde wakianza kutembea huku wakihema "weee utaona, Mbele ya kifo nitakimbia kama mbuni" wote wanacheka.

kama kawaida yao leo ilikuwa ni siku ya kucheza ngoma hivyo wametoroka nyumbani mama Yao asijue na kuelekea huko "tukae hapo tuvae hizi njuga" anaongea sinde akimwonyesha tulya pembeni ya njia na kwenda kukaa "una uhakika mama hatajua"anauliza tulya akiwa Hana uhakika kama mpango wao ulikuwa mzuri wa kutoroka "hawezi kujua kalala huyo,nitaachaje kwenda ngomani ngoma yenyewe inakuwa mwara Moja kwa mwezi " anaongea sinde akiwa tayari amemaliza kuvaa njuga zake miguuni akitengeneza mdundiko wake vizuri kiunoni.

"kwani shangazi anajua kama Leo ni siku ya ngoma" anauliza tulya na yeye akijitengeza vizuri kifuani kwake akijaribu kukaza kitambaa Cha kaniki kinachofunika kifua chake "ndio" Anacheka tulya baada ya kusikia jibu la sinde "unacheka nini" anauliza sinde akimwangalia kwa mshangao "hembu nisaidie huko mgongoni" sinde anaenda na kuanza kuinyoosha kaniki ya tulya iliyojikunja mgongoni "Nina uhakika anajua kama tumekuja ngomani sema hataki tu kuongea kwa sababu anajua hata akitukataza tutatoroka kama hivi na kwenda, kwa hiyo kaamua kutuacha tujichunge wenyewe" sinde anabaki mdomo wazi "kwa hiyo siku zote anajuaga kama Mimi naendaga ngomani"anauliza sinde "alikuwa anakuacha tu,siku nyingine usinikimbize kabisa Mimi" sinde anabaki kimya baada ya kugundua kuwa mama yake amekuwa akijua mchezo wake kwa siku nyingi na alimwacha tu.

Wanausikia mlio wa ngoma wakiwa wanakaribia maeneo ilipo,mwendo wao unaongezeka na bashasha ya kucheza ikiwajia moyoni "una hakika hatutakutana na kina kaka huku" anauliza tulya akitembea huku anacheza cheza akiufatisha mdundo wa ngoma "hawajagi ngomani hao kaka kilinge na marafiki zake hawapendi kujichanganya katika Mambo kama haya wanaona ni ya kitoto huenda tu siku ya kusikiliza maonyo ya wazee, kaka zinge hapendi makelele kwa Sasa atakuwa amelala fofofoo na mkewe nyumbani" sinde anamtoa mwenzake wasiwasi "hapo kweli kaka zinge hapendi makelele na wala sio mwongeaje yupo kama mama na mke kampata mpole kama yeye wameendana mtoto wao atakuwaje nawaza" "atakuwa kama Mimi shangazi yake" anajibu sinde na wote wanacheka

wanafika eneo la ngoma, vijana wakiwa wamefunika uwanja wakitimua vumbi kwa kucheza njuga zao miguuni zikiunogesha mziki ulio changanyika na ngoma,zeze,malimba,kalimba,kayamba na zingine na kufanya vijana wapotelee kwenye mziki.

"vipi mbona unakaa hapo"anauliza tulya baada ya kumuona sinde akikaa badala ya kuingia mduara wa ngoma "nahisi tumbo linaniuma we nenda tu ukacheze nikijisikia vizuri nitakuja kujiunga " "mbona ulikuwa mzima tu" anauliza tulya uso ukimjaa wasiwasi "nilivyoondoka nyumbani nilikunywa maji halafu nimekimbia itakuwa sababu hiyo" "au turudi tu nyumbani" "hapana wewe nenda kacheze likizidi kuuma nitakuita tuondoke" tulya anamwangalia sinde kwa muda "haya sitaenda mbali nitakuwa tu hapo" sinde anaitikia kwa kichwa na tulya anaondoka kwenda kujiunga na mduara.

Wakati ngoma zikiendelea nje kidogo ya Kijiji katika nyumba Moja kijana akiwa amelala chali nje juu ya kitanda kilichotengenezwa kwa miti kama kichanja.mkono wake wa kulia ukiwa chini ya kichwa chake na mwingine akiupitisha usoni pake mguu wake mmoja ukiwa juu ya mwingine macho yake akiwa ameyafumba kama aliyelala lakini masikio yake yakisikia saunti za ngoma barabara.

Anashtuliwa na mtu aliyempiga kwenye mkono wake anautoa mkono usoni na kufumbua macho kuangalia baada ya kuona aliyempiga anarudi tena kwenye mkao wake uleule wa awali "unataka nini mama hujalala tu" anaongea huku akiwa amefumba macho, lakini mama yake hamjibu anampiga tena mkononi anaamka na kukaa huku miguu yake ameikunja sura ikionyesha kukereka "si uonge nikuelewe Sasa unanipiga tu Mimi nitajua unataka nini au umekuwa bubu" anaongea huku akimwangalia mama wa takribani miaka hamsini "husikii"anaongea mama huyo huku akikaa kitandani hapo karibu na kijana wake "kusikia nin?i" anauliza akimwangalia mama yake tena "sauti ya ngoma, vijana wenzako wote wapo huko wewe umelala hapa nenda huko unalala mapema kama kuku" analalamika mama "mama mi niende ngomani nikafanye nini?" mama anamwangalia mwanae kwa kumhurumia asijue atafanyaje juu yake "nzagamba mwanangu ukiendelea kujitenga hivi na watu utabaki mwenyewe kweli, utaishije peke yake nenda ukajichanganye huko kwanini muda wote uwe peke yako unaukoma wewe" nzagamba anainamisha kichwa chake chini akiangalia miguu yake.

"nenda unaweza ukapata hata mchumba huko mwanangu" nzagamba kusikia hivyo miguu yake inatua ardhini na kusimama " utakuwa umechoka mama nenda kapumzike ndani na Mimi naenda kulala"anaanza kuelekea ndani ya nyumba Moja kati ya mbili zilizokuwa katika boma Yao"kwa hiyo una mpango wa kutokuoa kabisa umekata tamaa namna hii" nzagamba anasimama na kufumba macho yake huku viganja vyake vikifunga ngumu akizuia hasira zake " nimeshakwambia mara ngapi mama,hiyo maada sitaki kuisikia tena utakuja kuzoea lini kuwa maisha haya ni Mimi na wewe tu" anaongea nzagamba pasipo kugeuka kuangalia nyuma aliko mama yake.

Bibi sumbo anasimama alipo nakuelekea aliko nzagamba "usifanye hivyo mwanangu kwanini unataka kufunga milango yote ya maisha yako huwezi ukakosa riziki zote mizimu ikikufanyia hivyo itakuwa inakosea Sana,basi nenda angalau ukajaribu huwezi jua Mahali Kuna mtu atakayekuelewa na kuelewa unavyojisikia" " mama upende usipende inabidi ukabiliane na Hali halisi na sitaki hii maada tena masikioni mwanangu" anaongea nzagamba uso wake ukionyesha kumaanisha anachokitaka bibi sumbo anataka kusema kitu lakini anakatishwa na nzagamba " Mimi nimechoka naenda kulala" anamwacha mama yake nje na kupiga hatua kubwa kama anapima marefu na za haraka na kuingia ndani kwake anafunga mlango wake wa miti na kuugemea macho yake yakiangalia moto uliyokuwa ukififia katika mafiga anavuta pumzi ndefu na kwenda kujitupa juu ya kitanda kilichotandikwa ngozi.

nje bibi sumbo anaangalia mlango wa mwanae uliofungwa anapiga makofi na kushika kiuno" naona mizimu mnatafuta ugomvi na Mimi,na Mimi nawaambia kabisa kuanzia msimu huu msahau kabisa tambiko kutoka nyumba hii mbuzi mtazisikia harufu kwa wenzenu" bibi sumbo anagombana na mizimu kabla ya kwenda kuingia nyumba ya pili.

Ngomani vijana wakiwa wanaendelea kucheza linafika kundi la vijana kama sita wakiwa wamelewa sinde aliyekuwa amekaa pembeni anawaona na kusimama" Hawa wamefika hapa " anawangalia vizuri na kuwaona wamelewa " hii hali sio nzuri kabisa tulya Yuko wapi tuondoke" anatembea haraka haraka na kuingia katikati ya watu akimtafuta tulya ' alikuwa hapa sio mda na alisema haendi mbali kaenda wapi tena huyu' anawaza sinde akiendelea kupekua kumtafuta tulya katikati ya watu huku uso wake ukiwa umejaa wasiwasi na woga .

upande wa pili tulya akiwa anaendelea kucheza hakuweza kuona mabadiliko yaliyotokea na kufanya watu wote kucheza kwa kujihami akiwa Hana hili wala lile anaendelea tu kulisakata rumba.vijana waliofika Wanaingia mduara na kuanza kucheza kilevi wakijitupa huku na kule.sinde anamuona tulya akiwa karibu kabisa na wale vijana na yeye akiwa hana hata wazo ngoma imemkolea kichwani,sinde anapiga hatua za haraka katikati ya watu na kufanikiwa kumfikia .

Tulya anashtuka baada ya kuhisi mtu anamshika mkono kugeuka anamuona sinde "umekuja kucheza" anauliza huku akiendelea kucheza "tuondoke haraka" tulya anaacha kucheza na kumwangalia sinde " tumbo bado linauma?" anauliza akiwa na uso wa wasiwasi" sio hivyo we twende nitakwambia tukitoka hapa hilo ndo la muhimu" tulya anamwangalia sinde na kuona anawasiwasi na woga " sinde Kuna tatizo gani?" "maswali mengi ya nini twende bwana nitakwambia njiani" sinde anaanza kumvuta tulya iliwaondoke "sawa twende" sinde anageuka nakuanza kuondoka tulya nae anmfuata lakini anapiga hatua kama mbili tu anapamiana na mtu anataka kuanguka nakumwangukia mtu mwingine yule anamsukuma naye anaenda kudondokea katika kitu kama ukuta kuangalia vizuri anaona ni kifua Cha mtu kilichojazia misuli vizuri kiasi kufanya kuwa na maziwa makubwa kidogo kwa mwanaume,mikono yake iliyomdaka tulya ikiwa ni imara kweli na juu ya kiwiko Cha Kila mkono akiwa amefunga kidani Cha ngozi chenye kama kikengere kikining'inia na bangili za chuma mikono yote karibu na kiganjani.Ingawa Kila mwanaume hasa vijana walikuwa wanavaa hivyo lakini tulya aliona huyu vilikuwa vimemkaa vizuri kabisa .

Akiwa anashangaa harufu ya pombe inayotoka kwa mwanaume huyu inamrudisha akilini nakuziba pua yake,watu wote walikuwa wakiangalia varangati hili akiwemo sinde aliyekuwa akiona kama miti yote imeteleza na nyani kaanguka chini na kufa.wakati tahariki ikiendelea tulya anashangaa anatupwa chini na kuangukia makalio pwiii! viganja vyake vinawahi kufika chini na kumsaidia asipitilize tena,viganja vilitua kwa nguvu kubwa kumfanya asikie maumivu makali makalioni na viganjani.

unafuata ukimya mkubwa kwani wakati purukushani hilo likiendelea Hadi wapiga ngoma waliacha kupiga na macho yao kuelekea kule, na watu wengine kubana pumzi kwa mshangao na woga wa nini kitakachotokea baada ya hapo.tulya anagugumia maumivu pale chini na hasira zikimpanda na kumwangalia mtu huyu asiye na huruma aliyemtupa kama gunia la viazi pale chini, baada ya hapo zinasikika sauti mbili tu zilizoongea kwa pamoja na zote zikiwa zimejaa jazba

"unafanya niniii?"

"we nani?"

habari zenu wasomaji wangu samahani sana kwa kuwacheleweshea update ya Leo nilikuwa na majukumu yaliyonifanya nichelewe kuandika, kingine nawaomba sana ushirikiano wenu naombeni mnaposoma muwe mnaacha comment hapo chini Ili nijue maendeleo ya story yangu maoni ushauri chochote kile kinaweza kunisaidia katika uandishi support yenu ni muhimu sana, asanteni.