webnovel

chapter 57

Nyumbani kwa mzee Nshana pilika pilika zikiwa zinaendelea,maandalizi ya sherehe ya harusi itakayofanyika kesho yakiwa yamepamba moto.Tulya kwa sasa Yuko ndani akirekebisha sketi ya Sinde iliyochanika wakati akijaribisha.

" siamini kabisa kama umenenepa,natushukuru mizimu kwamba nilikumbuka kukwambia ujaribu leo,ingekuwaje kesho?sio kwa aibu hiyo,sijui ungevaa nini?"

" kwa nini nisinenepe kwa vyakula mnavyonilisha na kukaa tu ndani" Sinde anamjibu akijigeuza kitandani.

" mawazo ya kukukondesha huna?" Tulya anamuuliza akiendelea kushona nguo.

" mmmh" Sinde anamwitikia na kuongezea " Tinde hawezi kupumua bila Mimi niwaze nini?"

" hongera yako,lakini kesho ungetoka kama umeiba nguo zako mwenyewe,ndio ungekonda kwa mawazo ya milele ya kuaibika siku ya harusi yako" Sinde anacheka.

" usijali,watu wasingekumbuka hilo,nenepa kama Sinde alivyonenepa siku ya harusi yake,wata waambia hivyo mabibi harusi wanaokuja"

" Heri yako,oooh umemuona mumeo ndevu kama beberu" Tulya anacheka akikumbuka alivyomwona Tinde Jana usiku.

" mmmh??!mbona Mimi nilimuona hana ndevu?" Sinde anauliza akikaa kitandani.

" mmeonana?,lini?na saa ngapi?"Tulya anampatia mstari wa maswali akiacha kushona nguo na kumwangalia Sinde kitandani.

" Jana usiku kabla hujaja" anamjibu na Tulya kubaki mdomo wazi.

" usiniambie,usiku huo kaenda nyumbani kaoga,kanyoa na ndevu akaja na kukuona?"

" itakuwa,maana amekuja hapa Hana ndevu alikuwa Yuko vizuri kama siku zote"

" Mumeo mtarajiwa kiboko,kanishinda tabia" wote wanacheka " Tulya una mgeni" wanageuka na kumuona Malimbe amesimama mlangoni.

" mgeni?" anauliza akiweka nguo kitandani na kujaribu kusimama lakini mgeni anaingia ndani Tulya na Sinde wanashangaa kumuona Lindiwe.Kinachowafanya wagande zaidi ni sura ya Lindiwe.Mwili unamsisimka Tulya kwa jinsi Lindiwe alivyovimba akiyahisi maumivu ya Lindiwe mpaka kwenye mifupa yake.

Hakuna haja ya kuuliza kwani wanajua Manumbu kamfanyia hesabu." mu..mumeo ni..." Tulya anakosa neno la kumfananisha Manumbu kigugumizi kinamshika.Huzuni inampata baada ya kuona Lindiwe akijaribu kutabasamu kama kuwaambia amezoea hayo.

" Mimi nawaacha" Malimbe anaongea na kuondoka baada ya kumtupia jicho Lindiwe kwa mara ya mwisho.

" karibu ukae" Sinde anamkaribisha asishangae uwepo wa Lindiwe pale kwani Tulya alishamwambia kilichotokea baina Yao. Lindiwe anamwitikia asante akienda kukaa kitandani.

" ulikosa nini mpaka akuharibu kiasi hiki?" Tulya anauliza akikaa alipokaa mwanzo sura yake ikiwa bado imejaa mshtuko.Lindiwe anachezesha mabega yake kuonyesha kuwa hajafanya kitu.

" kwa hiyo kajisikia tu kukupiga?" safari hii Sinde anauliza.

" kisa Nina mkosi" anajibu Lindiwe akijaribu kuzuia machozi.

" nini?!" Sinde na Tulya wanaitikia kwa pamoja.

" kivipi?" Tulya anamuuliza macho yake yakienda kwenye uvimbe wa Lindiwe juu ya nyusi yake ya kushoto jeraha linaloonekana litachukua mda mrefu kupona kama sio kubaki na alama.Atakuwa alimpiga kichwa anawaza.

" amesema Mimi ndio Nina mkosi, Nzagamba alipokuwa na Mimi mambo yake yakaharibika na Sasa kakuoa wewe bahati yake imerudi na yeye ndio kaambulia mkosi maisha yake yote" anajibu machozi yakimdondoka na kupelekwa mkono wake kuyafuta.

"yule beberu mshenzi.." anatukana Tulya joto la mwili likimpanda.Sinde anatulia kimya akijaribu kupima uzito wa maneno ya Manumbu ambayo ukiyatafakari kwa pupa unaweza kuona ukweli ndani yake ambao umeanza kupita kichwani kwa Lindiwe akianza kujichukia na kujiona kweli anamkosi.

" itakuwa kweli Nina laana mimi" anaongea Lindiwe akiweka viganja vya mikono yake usoni kwake kwikwi ya uchungu ikimtoka.

Sinde na Tulya wanashindwa wamwambie nini Cha kumfariji maana wanajua uchungu alionao Lindiwe haufarijiki na Tulya analijua hilo baada ya kukaa na Nzagamba.na mtu kama huyu haitaji faraja ya maneno anahitaji mtu pembeni yake atakaye mwonyesha kuwa Yuko naye kwa Hali yeyote ile.Na jukumu hilo sio la kwao ni la mume wake ambaye kwa sasa yupo kama mbwa kichaa anayemuona Lindiwe kama mhanga wake wa kwanza machoni pake.

" kwa nini usirudi nyumbani kwenu,hata kama baba yako hata kuelewa mama yako atakuwa upande wako,ukiendelea hivi atakuua" anazungumza Tulya baada ya kuvuta pumzi ndefu na maneno yake yanamfanya Lindiwe alie kwa nguvu.

" mama yake Lindiwe amekufa siku nyingi wakati anamzaa Lindiwe,kalelewa na mama wa kambo na baba yake..." Sinde anajibu akiacha kumaliza alichokuwa anaongea na kumfanya Tulya kumwangalia Lindiwe kwa huruma zaidi ya hapo awali.

" ba..ba..baba yangu anasema sina faida" anaongea Lindiwe akilia.

Tulya anapepesa macho yake kuzuia machozi yaliyokuwa yanatishia kuanguka.Ni maisha gani anayoishi huyu? anajiuliza Tulya akiwaza ni namna gani Lindiwe alivyo mpweke.

" labda mizimu inaniadhibu kwa kumuacha Nzagamba katika Hali ngumu,inanifanya nipitie maisha aliyopitia yeye ya huzuni na upweke akiwa peke yake,ningefanyeje maisha yangu yote nimekuwa nikifanya anachotaka baba yangu,na sio kama sikujaribu kumuomba aniache niolewe na Nzagamba kwa sababu nilikuwa nampenda lakini baba yangu alisema hata kaa aangalie namletea laana na aibu kwenye familia yake na ukoo. na Sasa mwanae Kawa laana ileile alioikataa kaamua kukata nae undugu" anaongea Lindiwe akijaribu kutoa yote ya moyoni.

" pole sana" Sinde anamwambia lakini Tulya anaendelea kufuta machozi yake yanayoendelea kuanguka Kila anapomwangalia Lindiwe.Mtu ange mwambia hapo awali kuwa ipo siku atakuja kulia akimuonea huruma mwanamke aliyejaribu kuvunja ndoa yake ana uhakika ange mng'ata pua yake kama ukumbusho wa kumfanya aache kuongea upumbavu lakini huyu hapa machozi yana miminika kama kafikishiwa msiba wa mzee Kijoola.

" Sasa utafanya nini?" anamuuliza.

" nifanyeje?navumilia tu,siku akipata mke mdogo akamzalia mtoto atanisahau mpaka hapo nadhani maisha yangu yatakuwa haya" anawajibu.

"kwa nini usijaribu kuongea nae,utakuwa unamwonyesha woga sana ndio maana anapata nafasi kubwa,jaribu kumwonyesha umemchoka na unataka kuondoka,kwa ninavyoona anakupenda sana la sivyo angekuwa na wake watatu pembeni mpaka Sasa.Huwezi jua anaweza kupunguza" anaongea Tulya akikumbuka Jana walipowasili kutoka mawindoni namna Lindiwe alivyokuwa anatetemeka kwa kunusa harufu yake tu.

" ninaweza kufa kabla sijamalizia sentesi,akikasirika yule hasikilizi" anajibu akifuta machozi.

" jaribu huwezi jua,kama una mgonjwa hata kama unajua anaenda kufa ukisikia Kuna mganga ambaye hajanywa dawa yake utakimbia kumtafuta Ili tu kutafuta tumaini la yeye kupona" Tulya anamwambia macho yake yakienda kwenye sketi ya Tulya ambayo hajamaliza kuirekebisha.Wanaamua kubadili maada Ili wasimfanye Lindiwe kujisikia vibaya zaidi.

Hayawi hayawi, Sasa yamekuwa.Hatimaye Leo ni harusi ya Sinde na Tinde." Fanya haraka" Tulya akifunga viatu vyake anamsikia Malimbe akimwita akiwa nje.Tulya na Malimbe wamechelewa kuondoka kutokana na majukumu ya nyumbani na wanatakiwa kubeba mizigo ya Sinde na kuipeleka kwa wakwe zake au makazi mapya ya Sinde.

" usijali,tutafika makusanyiko ya sherehe kabla hawajafika" anajibu Tulya akiangalia shanga zake kiunoni kama zimemkaa vizuri.Ni shanga alizopewa kama zawadi na Lindiwe ameamua kuzivaa Leo kwani kwa kilichotokea Jana na baada ya kumsikiliza Lindiwe ameamua kuwa rafiki yake kutoka moyoni.

" umependeza bwana twende" Malimbe anaongea akimtengeneza mtoto wake mgongoni." natamani ningeenda kuona jinsi ndoa Yao inavyofungwa" anaongea Tulya akibeba furushi la nguo za Sinde na kutoka nalo nje alipo Malimbe " ohh,nimesahau njuga zangu" anaongea akirudi tena ndani." wewe msumbufu kweli" Malimbe anamjibu ambaye tayari ameshajitwisha furushi lake.

" nitaendaje bila njuga,wakati nataka nikamuonyeshe Sinde kuwa kwenye harusi yangu hakucheza alikuwa anaruka ruka,Mimi ndio nitamuonyesha watu wanavyocheza" anaongea akifunga mlango.

" ukiendelea kufanya kwa maneno tutachelewa" Malimbe anaongea akianza kuondoka.Tulya naye anajitwisha mzigo wake na kumfuata.

Makusanyiko ya sherehe Tulya na Malimbe wanawasili na kuona watu wakiwa tayari waneanza kupata chakula." nilikwambia tutachelewa" Malimbe anamwambia akiangalia huku na kule kuona watu wakiwa wamekaa makundi makundi wakipata chakula." hatujachelewa sana,ndio kwanza wameanza kula" Tulya anamjibu " ohh twende tukale pale" anamvuta na kuelekea alipo kaa Tausi na wanawake wengine anaangalia huku na kule asimuone Lindiwe.

Wakati anaendelea kupita katikati ya watu kumfuata Tausi Lingo aliyekuwa amekaa pamoja na marafiki zake akiwemo Nzagamba anamuona na kwa mshtuko anaanza kukohoa." utakufa kwa kupaliwa nyama" Mkita anamwambia akimpatia kipeo Cha maji." sio hivyo ona kule" anaongea baada ya kumeza funda la maji akiwaonyesha wenzake alipo Tulya kwa kidole.

" huyo ni Tulya?!" anauliza Kilinge asimjue binamu yake na watu wote kwenye kundi macho Yao kwenda kwa Nzagamba anayeonekana kutaka kupasuka.