webnovel

Chapter 56

Manangwa na Gulumo wanaangalia kama wameona mzimu kwa Mara ya kwanza angalia wao wenyewe ni mizimu.

" niambie sio yeye" anaongea Gulumo akiendelea kuangalia katikati ya umati wa watu macho yake yakiwa yametua kwa mtu Mmoja anayeendelea kuongea na watu na kama anahisi mtu anamwangalia macho yake yanageuka na macho Yao yanakutana.

" Makandelo ndio na.."

" shiiii" anaanza kuuliza Mnelela lakini ananyamazishwa na Mzee Manangwa ambaye yuko makini akimtafakari mtu anayetazamana naye macho kwa macho.

" kimbia" anaongea Manangwa akiwa tayari ameshapotea aliposimama akifuatiwa na Gulumo wakimwacha Mnelela akizubaa asijue akimbilie wapi na anakimbi kitu gani?.Wakati akiendelea kuzubaa anashangaa akivutwa na anajikuta mbali kidogo na sherehe ilipo.

" ulikuwa unafikiria nini kubaki hapo?" anauliza Gulumo wakati Manangwa akiendelea kushikilia moyo wake usio dunda kifuani kwake akihema kama kakimbia mbio." Sikujua nikimbilie wapi?" anajibu Mnelela kwani hajui wenzake wanamkimbia nani asijue akakimbia kumbe anakoelekea ndiko kwenye hatari yenyewe.

" mkuu kwani Kuna nini?" anauliza kwani hajawahi kuwaona wakuu wake hasa Manangwa katika Hali kama hii.

" niache nifikirie kwanza" anasema Manangwa akigeuka na kuangalia upande zinakotokea sauti za ngoma na vigeregele.

" Ni yeye,si ndio?" anauliza Gulumo swali ambalo tayari uhakika anao lakini moyoni akitamani Manangwa aseme sio ili kumpa ahueni.Lakini nguvu zote zinamuisha baada ya Manangwa kumhakikishia kwa kichwa kuwa mtu waliyemuona ni yule wanaemdhania.

" lakini si alikufa yule?" anauliza Gulumo wakimfanya Mnelela kukuna kichwa akiona anaachwa njia panda.

" ndio,sura siyo hiyo lakini Nina uhakika ni yeye,macho yake bado yana moto Kama siku zote" anaongea Manangwa ambaye kwa sasa ameweza kujiweka sawa.

" usiniambie amezaliwa tena"

" mmmh" anaitikia Mzee Manangwa busara ikianza kurudi usoni kwake baada ya burudani yake kukatishwa.

" lakini haiwezekani,aliuwawa na mzimu yule au Zulimo alifanya kazi chafya" anajibu Gulumo uso wake ukionyesha utatanishi anaopitia.

" Nadhani karudi kwa sababu hakumaliza kazi yake,na nadhani hajapata nguvu zake na kumbukumbu hazija mrudia lakini haitachukua mda kwa macho aliyokuwa anatuangalia nadhani ametuona na atakuwa anapata matukio mbalimbali kama ndoto bado tu kuyaunganisha" anaongea Manangwa akimalizia kwa kuvuta pumzi ndefu.

" kweli,angekuwa kapata nguvu zake asingechelewa kutuunguza pale" anajibu Gulumo

" kwa nini wasingeleta mtu mwingine tu,wakaamua kumrudisha Makandelo katika watu wote duniani waliokufa" anaongea Manangwa akionyesha kukerekwa na mtu aliyemleta Makandelo.

"unaogopa kwa kilichotokea kabla hajafa eee,kwa hasira yake yule najua atakuua atakapo kutia machoni tu" anajibu Gulumo akikunja mikono yake kifuani baada ya kutengeneza rubega yake.

" utadhani wewe utasalimika" Manangwa nae anamjibu na kumfanya Gulumo kugeuka na kumwangalia.

" Mimi nimekosea nini? nilikuwa nafata amri yako tu?" anajitetea Gulumo.

" Makandelo analijua hilo?,kabla hujajieleza umeshakuwa majivu mda mrefu"

" mmh,wakuu.." wanamsikia Mnelela na wote wanageuka kumwangalia.

" samahani kwa kuwaingilia lakini nilitaka tu niwakumbushe,hamuwezi kufa kwa sababu mmeshakufa" anaongea na kufanya wakuu wake wamwangalie Kama yeye ni kalunguyeye asiye na miiba.

" wakati mwingine ujinga nao ni faida" anaongea Manangwa anageuka na kuangalia mbele yake kichwa chake kikiwa kwenye mzunguko wa mawazo.

" Kuna watu wawili tu wanaoweza kuua mizimu" Gulumo anaanza kumuelimisha." Mmoja ni mtoto nyota kwa sababu anakuwa na nguvu zote na wa pili ni mmiliki wa moto ambaye ni mlinzi wake,kufa namaanisha ukipigana nae anakuua nafsi yako inapotea,haiendi kupumzika kwa wazee na duniani hakuna mtu atakaye kukumbuka kama ulikuwepo" anamaliza Gulumo akisisitiza ukubwa wa tatizo.

" lakini kizazi Cha wamiliki wa moto si kiliisha miaka mingi iliyopita?" anauliza Mnelela.

" na wa mwisho katika kizazi chao ndio karudi kutumaliza sisi" anajibu Manangwa.

" Sasa mmemkosea nini Makandelo mpaka awaue? ninavyojua mizimu na wamiliki wa ardhi wanatakiwa kupatana kwani kazi Yao wote ni moja kumlinda mtoto nyota" anauliza Mnelela na macho ya Gulumo yanaenda kwa Manangwa kama kumwambia huyu ndiye kalizua janga.

" sio atuue sisi,akikuona hata wewe anakua" Gulumo anamjibu na macho ya Mnelela yanakaribia kuanguka kwa woga wa kufa mara mbili angali bado mdogo sio zuri kabisa,na kibaya zaidi asiwaone wazee na duniani asikumbukwe pia.Wazo halikuja vizuri kabisa kwake imekuwaje anaingizwa kwenye ugomvi asioujua.

" lakini Mimi sijamkosea" anajitetea haraka haraka.

" hivyo ndivyo anavyowachukia mizimu" anajibu Manangwa na Kama anakumbuka kitu anageuka na kumwangalia Mnelela.

"Tofauti na Nzagamba hukuona,mtu mwingine yeyote wa tofauti hapa kijijini?"

" hapana" anaitikia Mnelela.

" atakuwa hatoki Kijiji hiki" anajibu Gulumo.

" uwezekan..." Manangwa anakatishwa na Mnelela aliyekuwa anazungusha kichwa baada ya kuulizwa swali.

" aaaah,yupo rafiki yake Nzagamba lakini hawako karibu sana Kuna mda huwa nahisi Kama ananiona vile lak...aaah" anapiga kelele baada ya kupigwa kwenzi na Manangwa.

" si nilikwambia ukiona kitu chochote Cha ajabu utoe taarifa wewe"

" sikuona Cha ajabu" anajibu Mnelela akijikuna kichwa.

" tuondoke" anaongea Manangwa akianza kutembea asitake kuumiza kichwa zaidi na Mnelela.

" na wewe unaenda wapi?"anauliza baada ya kuona Mnelela anataka kuwafuata na yeye akimwangalia kwa kutokuelewa.

" kazi yako haijaisha hapa,endelea kumwangalia Nzagamba,hakikisha haukamatwi" Manangwa anapotea baada ya kuongea hivyo.

"na ni bora ukaishia mikononi mwa Nzagamba kuliko Makandelo,kwa sababu wewe ndio utakuwa wa kwanza kulamba jivu" anamalizia Gulumo akitaka kuondoka lakini Mnelela anamshika.

" si mjui Makandelo"

" yule unayehisi anakuona ndio Makandelo " anamjibu na kutoweka.

" mbona kama nimetolewa kafara" anajisemea Mnelela akiangalia huku na kule.

"Zinge"

"eeeh" Zinge anashtuka baada ya mtu kumwita nyuma yake anageuka na kumuona kaka yake Kilinge.

" unaangalia nini mda wote huo?" anamuuliza akiangalia alikokuwa anatazama Zinge asione Cha ajabu zaidi ya watu wakicheza.

" Amna kitu" anajibu na kuanza kuondoka.

" Zinge" anasimama anageuka na kumwangalia Kilinge anayekuja na kusimama mbele yake.

" Unaota ndoto mbaya tena au?" Kilinge anamuuliza kwani siku nyingi amekuwa akimuona ndugu yake akiwa amechoka asubuhi.

Kilinge anajua kuwa Zinge anatabia ya kuota ndoto mbaya na za kutisha Kama mwenyewe Zinge anavyoelezea na walipokuwa wadogo ilikuwa inamsumbua sana kiasi Cha kumfanya asilale kabisa.Hali hii iliwatia wasiwasi mzee Nshana na mama yake Runde walimpeleka kwa mtaalamu aliyefanikiwa kuzifunga ndoto hizo.Hali ambayo ilimsaidia lakini kwa kipindi. Sasa Hali hii imekuwa ikijirudia na kwa kumbukumbu zake ni tangu harusi ya Tulya na nzagamba.kipindi Cha nyuma haikuwa mara kwa mara kama ilivyo hivi karibuni.

" unajua Sasa hivi nim...." anaongea na macho yake yanaenda kule alikokuwa anaangalia mwanzo.

" Amna kitu" anaamua kupotezea akihisi kukosa usingizi,uchovu wa kutoka kuwinda pamoja na pombe aliyoionja vinamfanya aone mauza uza.Kwani muda si mrefu aliowaona watu watatu wasio wa kawaida na alipopepesa macho yake tu walitoweka.Anatikisa kichwa chake akijaribu kujiweka sawa.

" Ukiwa tayari utaniambia kinachokusumbua,na Kama ni ndoto itabidi tumwambue baba Ili ukatibiwe tena" Kilinge anamwambia akitaka ndugu yake ajue wako pamoja

" mmmh" Zinge anaitikia akimwangalia kaka yake.

" twende huku" wote wanaondoka na kujiunga na wenzao waliokuwa wakinywa.

" ndio maana nilihisi,hayuoko sawa kabisa huyu" anaongea Mnelela aliyekuwa amejificha nyuma ya jungu kubwa lenye pombe karibu na waliposimama akisikiliza maongezi Yao.

" natakiwa kuwa makini" anamalizia mwili wake ukimsisimka Kila akifikiria kuunguzwa na kuwa majivu.