webnovel

chapter 8

sinde na tulya Wanaingia nakuanza kucheza, vijana wengine wakiendelea kunywa na kuongea hili na lile "yule msichana mbona simjui anacheza vizuri kweli" anasikika kijana Mmoja aliyekuwa amekaa na manumbu na kuwafanya wengine wageuke na kuangalia kule alikokuwa anaangalia "yule sio yule mschana aliyegomba na nzagamba siku ile usiku" anaongea mwingine akimwangalia manumbu kama kuhakikisha "una uhakika meli" anauliza kijana aliyemuona tulya kwanza meli anaitikia kwa kichwa akiangalia aliko tulya kuhakikisha tena.

"ndio ni yeye" zinge anageuka na kuangalia anamuona tulya anageuka na kutabasamu anachukua kipeo Cha pombe na kunywa kidogo anakirudisha chini manumbu nae anamwangalia tulya aliyekuwa Hana hili na lile kuwa alikuwa kwenye kituo Cha maonyesho."atakuwa ni mgeni huyo mschana la sivyo asingethubutu" anaongezea kijana anayejulikana kwa jina la nsio.

"binamu yangu huyo" zinge anawaambia huku akiendelea kunywa na wale vijana wengine kubaki kwenye mshangao isipokuwa manumbu aliyekuwa anajua "aaa kweli nilimuona akiwa na sinde siku ile"anakumbusha meli "ameolewa,ni mrembo kwelikweli ni mfanye mke wa pili"nsio anaongea huku akimwangalia tulya na kumfanya zinge acheke "utamuweza anaonekana sio mwanamke wa kutulia muulize manumbu siku ile aliishiwa maneno"

meli anamwangalia manumbu aliyekuwa akinywa pombe akimwangalia tulya,kusikia maneno ya meli zinge anageuka na kumwangalia manumbu aliyekuwa anamwangalia tulya anatoa tabasamu na kusema "hajaolewa,labda manumbu atamuweza " anaongea huku akimwangalia manumbu aone atasemaje,manumbu anashtuka na kumwangalia zinge kwa mshangao lakini zinge anaonyesha kutokujali anaendelea kunywa pombe "lakini manumbu anampenda lindiwe tu hiyo itakuwa ngumu zinge kama unataka shemeji nifanye Mimi basi" anabembeleza nsio "huwezi jua moyo huwa unabadilika "zinge anaongea akimwangalia manumbu kama kumpima

"humuwezi wewe kwa hasira zile atakupiga asubuhi tu" meli anamshika bega nsio kumwambia asijaribu kabisa "ni hatari kiasi hicho" anauliza nsio "kama alimkosesha manumbu neno wewe utamuweza au zinge twambie" meli anamwangalia zinge akitarajia majibu lakini zinge hasemi kitu.

"unapotea mpaka tunakusahau nzagamba"anaongea kilinge akikaa karibu na nzagamba na wengine watatu "unajua pakunipata Mimi kama unataka kuniona" nzagamba anaongea na kumwangalia kilinge "hongera nasikia unakaribia kuwa baba"anaongezea nzagamba "asante,uwe unakuja hata kwenye maonyo ya wazee usiku nzagamba" kilinge anasisitiza alimkumbuka rafiki yake wa karibu na aliyekuwa kiongozi wao kambini "nikafanyeje maongezi hayanihusu" anamjibu nzagamba huku akinywa pombe " polepole nzagamba usije ukalewa"anaongea kijana mwingine anayejulikana kwa jina la ntula "atakuwa kamuona lindiwe mwacheni anywe tu,kwanza tangu lini nzagamba akalewa anakichwa kigumu Cha pombe" anaongea kijana mwingine na kufanya wenzake wote wamwangalie kwa jicho la onyo "unamzungumzia wa nini huyo mkita" kilinge anaongea akimpiga kibao mkita aliyekuwa karibu naye na wengine wote kumwangalia nzagamba "Haina shida hiyo ilikuwa ni Hadithi yangu ya zamani na siwezi kuwazuia watu kuongea nimeshamsahau Mimi" nzagamba anaongea na kufanya wenzake wamwangalie kwa kuhakiki kama anachoongea ni kweli.

" nadhani atakuwa anajuta Sasa hivi anavyoishi na manumbu anajua yeye tu wakati mwingine Hadi anapigwa" anazungumza kijana aliyekuwa hajaongea tangu wafike hapa "una uhakika lingo mbona Mimi nimemwona anazidi kuwa mrembo" anauliza mkita ambaye hakuamini maneno ya lingo "kingine manumbu anampenda sana lindiwe"anaongezea ntula "itakuwa inahusiana na tatizo lake la kuchelewa kuzaa si mnajua yule hapendi kushindwa" anongezea kilinge anayejua Hali halisi ya manumbu na lindiwe aliyesikia kutoka kwa mdogo wake zinge asitake kuongea zaidi sababu ya rafiki yake nzagamba asije akaumia zaidi,wote wanageuka na kuangalia aliko manumbu na kuendelea kunywa pombe

Lakini ntula anazidi kumwangalia manumbu nakuona Kuna kitu anaangalia kwa makini, anafuatisha macho yake na kuona anamwangalia tulya "kwani yule msichana ni nani?" anauliza akimkazia macho tulya na wengine wanageuka na kuangalia aliko tulya lakini kilinge na nzagamba hawakumuona vizuri "aaa yule msichana atakuwa ametoka Kijiji Cha jirani amekuja na leo" anaeleza mkita " unamaanisha nini na Leo?" anauliza kilinge "siku chache zilizopita,siku ya ngoma aligombana na manumbu kulikuwa tifutifu" anaeleza mkita na kwafanya wenzake wote waitike "nini?" wote wanageuka kumwangalia manumbu na macho yao kwenda kwa msichana isipokuwa kilinge na nzagamba ambao bado walikuwa hawamuoni vizuri "yule msichana aliyemwita mlevi manumbu alisema anajitupa kwake" anaongea ntula akihakiki "ndio,ndo yeye,ulikuwepo?" anauliza mkita

"hapana,ila nilisikia kwa mtu aliyekuwepo kuwa manumbu alipata aibu Balaa halafua baada ya hapo mschana alipotea manumbu alimtafuta hakumpata" ntula naye anaeleza anachojua na macho yao wote yanamwangalia mkita aliyekuwepo kupata taarifa kamili na mkita anaendelea "Mimi sikujua chanzo nini ila nilisikia tu makelele yule msichana akifoka na kumwambia manumbu kuwa hata wanaume wote wakiisha hawezi kuolewa na yeye" anamaliza mkita na wenzake wote kucheka kwa nguvu mpaka nzagamba "natamani ningeiona sura ya manumbu" anaongea kilinge na wengine wote wanaitikia "Mimi pia" " ilikuwa ni aibu balaa" anaongeza mkita na kumwangalia kilinge "nilijua kilinge unamjua" wote wanamwangalia kilinge naye anamtupia jicho mkita "kwa nini"

anauliza kilinge asielewe "alikuwa na mdogo wako sinde" mkita anamjulusha na kilinge aliyekuwa ametoka kunywa pombe anapaliwa kwa mshtuko anakohoa kwa nguvu na baada ya kumaliza anaangalia kule wanakocheza watu lakini bado alikuwa hamuoni tulya " unamjua" mkita,ntula na lingo wanauliza kwa pamoja na kilinge anatikisa kichwa kukubali "ni binamu yangu huyo mtoto wa shangazi yetu,yaani siamini kama wanaenda usiku kwenye ngoma wakati baba alimkataza sinde pindi tu alipochumbiwa"

"huyo binamu yako kiboko,ameolewa" anauliza lingo "bado" kilinge anajibu akiangalia wanakocheza kina tulya na safari hii anamuona vizuri kabisa "hapo kweli nani atamuoa sio kwa hasira zile hata hajifichi, nakwambia siku ile Hadi mwenyewe nilishtuka alivyokuwa anajibishana na manumbu" anaongezea mkita "lakini ni mrembo kupita hata lindiwe" anaongeza ntula akimwangalia tulya na wengine kugeuka na kuangalia isipokuwa nzagamba "sijui ni mfanye mke wa pili"anaongezea lingo na kumfanya kilinge acheke "tutakuzika siku sio zako,hataki kuolewa yule mjomba na shangazi wamekata tamaa Kila wachumba wakija anavuruga unaweza kuamini alijifanya anakifafa Mbele ya wazee walioleta Mahari nyumbani na uchumba ukafa" anafafanua kilinge na kuwafanya wengine wabaki midomo wazi kwa kutokuamini "ndio shangazi kamleta huku akitumaini baba amuozeshe sababu ataogopa kufanya fujo" anamalizia kilinge na kushika kipeo chake Ili anywe pombe "naona utapata shemeji sio mda" anaongea mkita wote wanamwangalia na kuelekeza macho yao kule anakoangalia na kuona manumbu anamwangalia tulya

"unamaanisha manumbu" anauliza lingo "hata niwe marehemu siwezi kumwozesha kwa manumbu tulya anaharakati nyingi lakini sio mtu mbaya ana tabia nzuri na roho nzuri pia,sura nayo nzuri sitaki akanichakazie binamu yangu" anapinga kilinge kwa nguvu zote "lakini zinge hasemi kitu na akipeleka posa baba yako ataikubali tu anavyompenda manumbu" mkita anatania " Mimi ndio nitakataa" kilinge bado akiwa kwenye msimamo wake na kuongeza " na kama tulya aligombana naye Nina uhakika hata kubali kuolewa nae hata ikibidi kucheza nusu kaputi"

Anaongea kilinge na kuwafanya wenzake wacheke kwa nguvu Hadi nzagamba.

kicheko kinasikika mbali hadi kina manumbu na wenzake wanasikia "nzagamba nae bado anachekaga?" anauliza nsio kiutani "naona atakuwa kajisahau baada ya kujichanganya na kundi lake la zamani" meli naye anongezea.zinge anaangalia tu bila kutia neno.

manumbu anaamka na kwenda sehemu walipo wapiga ngoma na ngoma inatulia "jamani ee ngoma inaendaje?" anauliza manumbu na kufanya watu wote wamwangalie yeye akiwemo tulya aliyeona manumbu kutaka kumwaribia sherehe.manumbu anaendelea "imekuwa siku nyingi sana hatujapata mziki mzuri,mnaonaje kama mpigaji wetu mzuri wa kalimba na malimba nzagamba akituburudisha Leo"

inasikika minong'ono na watu wakianza kugeuka na kuangalia aliko nzagamba isipokuwa tulya aliyekuwa ameganda baada ya masikio yake kusikia jina la nzagamba mapigo yake ya moyo yakimwenda mbio na kijasho chembamba kikimtoka mikononi, anaikusanya mikono yake kwa pamoja na kuiunganisha kuzuia kuonekana kuwa alikuwa anatetemeka watu wote wakiwa wamegeukia upande ambao anahisi ndiko alikokuwa nzagamba lakini asipate nguvu ya kugeuka kuangalia huko "umepatwa na nini tulya."