webnovel

chapter 62

Nzagamba ananyosha mkono wake agonge mlango lakini anaurudisha macho yake yanaenda sehemu nusu ya damu ya mwili wake ilipokimbilia na kutukana kimoyomoyo.Bibi sumbo angekuwa sio mama yake anajua yeye mwenyewe angemfanya nini kwa kumkosesha usingizi ,haamini kama mwanamke aliyekuwa upande wake siku zote za maisha yake atasababisha kesho aamke na mshipi unekaza na maumivu juu

" inakuwaje na huyu mwanamke analala baada ya kusababishia yeye majanga!" anawaza Nzagamba akijivuta na kwenda kukaaa kwenye kichanja tena mikono yake yote ikishikilia kichwa chake kama kimemzidi uzito.

Anaamua kulala tena pale nje akiomba mizimu upepo upite upate kupoza damu yake inayochemka mwilini.Masikio yake yakitega antenna zake na kusikia sauti za watu wakiendelea kuburudika na harusi ya Sinde na Tinde.Nzagamba anawaonea wivu watu hao wasio na wasiwasi wa maisha kama yeye.Wivu unaenda zaidi kwa Tinde ambaye atakuwa anafaidi kwa Sasa " pumbavu" anatukana baada ya kusikia vigeregere na miruzi kutoka ngomani.

Tofauti na Kijiji Cha Ntungu kilichojaa shamra shamra za ngoma na vigeregere kwingine kukiwa kumetaliwa na ukimya mkubwa watu wakiwa wamerejea katika vibanda vyao na kujikunyata wakiwa katika wimbi zito la usingizi wakiota ndoto za furaha,wengine wakisumbuliwa na majinamizi ya usiku katika ndoto zao, wengine wakiwa wamelala fofo kutokana na uchovu wa kazi zao za mchana au wengine wakihesabu shanga za maisha Yao kuhakikisha wanazitunga zote katika uzi kwani endapo ikipotea Moja Kuna tatizo.

Moja kati ya watu hao ni mtemi Limbo aliyekaa kwenye kiti chake Cha miti Cha kuegemeza nje katika kianda Cha nyumba yake,moto mkubwa uliochochewa magogo makubwa kuhakikisha unawaka kwa mda mrefu au mpaka asubuhi ukiwa unawaka mbele yake.Cheche zikiruka na Kuni zikitoa sauti kila moto unapokolea zaidi katika mifuoa Yao.

Mkononi mwake akiwa ameshikilia kijiti Cha mti akiwa ameinama na kufanya kifua chake kuishia kwenye mapaja na kidevu kwenye magoti yake,Macho yake yakiwa yanafuatisha mkono wake wenye kijiti unao zunguka huku na kule ukichora chini kwenye majivu michoro ambayo anaielewa mwenyewe na akiifuta kila baada ya mda na kuchora mwingine au unaweza sema akirekebisha wa awali.Ukimwangalia kwa haraka unaweza kujua umakini wake upo kwenye ile michoro pale chini lakini ukiwa makini zaidi utajua kilichopo pale ni mwili tu akili haipo.Ni watu wengi ambayo hawalijui hili isipokuwa nyampala wake na kijana wake Dunila ndio wanaojua ni namna gani Mzee huyu hutumia akili nyingi kufikiria mambo utadhani ameenda kesho kuchungulia Kuna nini.

Sauti za mbwa wakibweka na fisi wakiunguruma wakikaribia Kijiji zikisikika lakini ukimuuliza Mzee huyu kama amesikia atakuuliza nini? Sauti za hatua za mtu au watu zinasikika kwa mbali zikiendelea kukaribia mahali alipo na baada ya mda mfupi anatokea nyampara wake akifuatiwa na kijana wake Dunila. wanakuja kusimama karibu alipo na wote kutoa heshima.Lakini Mzee Limbo anaendelea na kazi yake." ungeniambia kama Yuko hivi mi ningekuja baadae" anaongea Dunila akionekana kukerekwa na nyampara wa baba yake aliyekuja kumwita akimwambia kuwa anaitwa na mtemi matokeo yake anafika na kumkuta Yuko katika nchi ya ahadi.

" nilivyo ondoka hakuwa hivi bwana wangu" Nyampara anamjibu akiinamisha kichwa chake kidogo kama kuomba radhi." Lakini ulijua kama mpaka nikifika atakuwa hivi" anaongea Dunila macho yake yakienda kwenye majivu anayochorea baba yake pale chini akiwa na uhakika kuwa nyampara huyu ndie aliyemwekea baba yake kabla hajampa amri ya kumwita.Na anajua kama baba yake humfanyia makusudi na nyampara huyu hufanya Kila kitu anachosema,anashika kiuno akimwangalia baba yake na macho yake kwenda kwa nyampara anayeenda kuchochea moto na Kisha anachukua majivu pembeni na kwenda kuongezea pale anapochora Mtemi.

Dunila anatamani aondoke lakini akifikiria umbali wa nyumbani kwake mpaka huku anakuwa Hana jinsi ila kukaa amsubirie mpaka baba yake atakapoamua kuongea.Ingawa wanakaa boma Moja ila nyumba zao zipo tofauti na Kuna umbali kidogo na anavyomjua Mzee huyu anaweza akaondoka akaamka kwenye usingizi wake akaagizwa aitwe na anapofika anakuta kalala tena akiwa macho wazi.Hii imetokea mara nyingi akiwa mdogo,alipokuwa akifika akimkuta Yuko hivi anaondoka na kusema akiamka wamemwite na kitendo Cha kufika nyumbani kwake kabla hajaweka hata Tako chini nyampara au kijakazi anafika kumwita utadhani alimfuata nyuma yake kwani ni kweli na akirudi mpaka akifika anamkuta kalala tena.

kitendo kilichomfanya agundue kuwa baba yake anamfanyiaga kusudi kwani ukikaa umsubirie anaweza kuchukua hata lisaa hajaamka na wewe ukiwa umesimama au umekaa kama mlinzi wake. Dunila akaamua kujifunza kuwa mvumilivu na kusubiri kuliko kujipa kazi ya kwenda na kurudi.

Anatoa Kiko yake alioichomeka katika kimfuko Cha ngozi karibu na kiuno chake anaweka tumbaku anaenda karibu na moto anainama na kuwasha anavuta na kutoa Moshi kidogo akiupuliza karibu na uso wa baba yake kujaribu bahati yake lakini Mzee hata hakukohoa ni bora kajaribu si ndio.Macho yanamtoka nyampara aliyesimama pembeni na kuona alichokifanya Dunila.Anasimama akitukana ndani kwa ndani na kwenda nje kidogo ya kianda anasimama na kuanza kuvuta Kiko yake akikiangalia kivuli chake kirefu kinacho akisiwa na moto unaotoka nyuma yake.

Macho yake yanaenda angani akiangalia nyota zinavyolipendezesha anga na kutangaza kuwa Sasa ni usiku na watu wote wakapumzike lakini baba yake ameamua kumfanya mlinzi.Anageuka na kumwangalia akiwa bado anachora anachokijua mwenyewe , Anatamani kiburi hicho angewafanyia wale wazee wanaokaa pangoni kule aone watakavyomfanya,tabasamu linatokea usoni kwake akifikiria ni namna gani Mzee Zulimo pua zitakavyo mpanuka kwa hasira siku akipuuziwa na baba yake.Anavuta Kiko na Moshi kuutolea puani akiendelea kupiga picha ya timbwili la siku hiyo.

"usiuvunje uvumilivu kijana kwani ukivunjika husababisha tafrani" Inasikika sauti ya Mzee Limbo baada ya kama mwaka kwa Dunila na ukweli ni kuwa ni nusu saa tu,na hapo anahisi kawahi kuamka." hatimaye" anawaza Dunila akigeuka kumwangalia baba yake ambaye macho yake yalikuwa kwenye moto mbele yake. " kama ulikuwa unaenda kulala kama sungura usingetuma mtu kuniita mpaka uamke" anaongea Dunila ilihari akijua haitasaidia kitu kwani ni mchezo ambayo amekuwa akifanya siku zote za maisha yake na mpaka Sasa hajui furaha yake iko wapi?

" jifunze kuwa mvumilivu kijana mambo mengine hayahitaji haraka yanapaswa kusubiria kwa uvumilivu mkubwa" anaongea Mzee Limbo akijiweka vizuri kwenye kitu.

" hayo tena" anawaza Dunila akifikiria sentesi ya uvumilivu ambayo baba yake hupenda kuitumia Kila akiamka kwenye usingizi wake wa ndoto ya kuchora.Anaenda na kukaa kwenye kiti upande wa pili akitazamana na baba yake,anajua akishasikia maneno hayo basi mazungumzo hayaishi leo.

" na siku nyingine usitumie hiyo mitego yako ya kipuuzi kuniamsha" anazungumza Mzee Limbo akikohoa kidogo na Dunila anajua anazungumzia alipo mpulizia moshi usoni.Ndio anakuwa anakusikia vizuri sana sema anajifanya hakuoni wala kusikia Ili akutese tu,anawaza Dunila." kwa nini umeniita huoni kama ni mda wa kupumzika huu?" anauliza akipuuzia alichokisema baba yake.

" hapo zamani za kale kulikuwa na msafiri" anaanza Mzee Limbo." ohoooo! tunakesha Leo" anawaza Dunila akitamani wakati nyampara anakuja kumwita angejifanya hayupo na kwa bahati mbaya alimkuta nje.

" msafiri huyo alipenda kuzunguka huku na kule akitamani kuijua Dunia,na Kila akirudi watu walijikusanya nyumbani kwake kutaka kusikia hadithi ya maajabu aliyoyaona safarini" anatulia kidogo na macho yake yakivuta hisia kama vile anamuona huyo msafiri au wanakijiji wanaosikia hadithi zake.

" siku Moja alirudi kutoka safarini na watu walijikusanya kama siku zote kusikia maajabu ya safari yake,lakini msafiri aliwaambia kuwa mara hii ana kitu Cha kuwaonyesha,msafiri alikuwa na gunia lililojaa vitu ambavyo hawajawahi kuviona.Alimwambia kijakazi wake abebe gunia na kwenda nalo shambani na watu walimfuata kutaka kujua Kuna nini kwenye gunia."

Dunila anamsikiliza kwa umakini akijaribu kutafakari simulizi hii ina maana gani?Siku zote baba yake humsimulia simulizi ambazo mpaka Leo akizungusha kichwa kujua maana yake huwa hapati jibu lakini siku zote amekuwa akiamini kuwa simulizi hizi Zina maana yake na Kila mara akiwa anasimulia hujikuta anakuwa makini apate kusikia Kila kitu akiwaza moyoni labda ataweza kujua anacho maanisha asiweze kumpuuzia.

" Baada ya kufika shambani msafiri alitoa mbegu kubwa, watu walishangaa sana aliwaambia katika safari yangu nilifika katika himaya Moja na nilikuta watu wa kule wa Kila matunda haya,niliyapenda sana hivyo nilitamani niwaletee na nyie muone lakini nilipokuwa njiani yalinizidi nguvu nikawa nakula nakupunguza uzito,baadae nikaona sio lazima nilete matunda nikaamua kuhifadhi mbegu Ili nije nipande kwetu tule sisi na vizazi vyetu.

Basi msafiri na wanakijiji walishirikiana kupanda mbegu hizo wakisubiri kwa hamu kwa miti ya matunda kuota wapate kula matunda.Kila siku walienda kuangalia kama imeota wakiwaza kama mbegu ni kubwa kiasi hiki mti wake utakuwaje?kama wa mbuyu au?Shauku ilikuwa inakuwa Kila siku. lakini walikuta hakuna hata mche na hata baada ya msimu wa mvua kufika na kupita bado mbegu hazikuota.Msafiri akafa na shauka Yao ikafa pia"