webnovel

chapter 30

wote wanarudi kazini,wakigawana majukumu " mshahara wake nini?" anauliza Ntula akichimba shimo " chakula,au wewe unacho?" anajibu Zinge akiendelea kupanga majani " " Jana nilikuwa msituni,nilizurura mpaka jioni ndio nikapata chochote kinachoisha Leo jioni" anaongea akitengeneza mshipi wake vizuri " Hali inazidi kuwa mbaya,kwa nini uongozi msifanye kitu" anaongea Mkita akimwangalia Kilinge " unataka tukawaswage huko walikojificha na kuwaletea mlangoni kwenu au" anajibu Kilinge asipendezwe na lawama za yeye kuwa kiongozi na kutoweka kwa wanyama,sio makosa yake wanyama kuondoka na hata hivyo hajui hata walikojificha " kwanza Kijiji chetu,kina uwafadhali,huko kwingine Hadi maji yanakauka" anaongezea Kilinge.

"Hali ni mbaya kiasi hiki?" anauliza Lingo " ndio,na maji yakikauka,itakuwa mbaya zaidi" anaongezea Kilinge akisafisha pua yake " nipatie jembe hilo" anaongezea na Lingo anampatia " ila ninauhakika siku mbili hizi,itapigwa mbiu ya kwenda lombo kwa wanaume wote,lakini hata hatujui tutaenda wapi maana kila mahali hali ni hii hii ndio maana manumbu alikuwa amechanganyikiwa mda ule" anazidi kuelezea Kilinge." Nzagamba kuanzia leo nitakuwa mwanafunzi wako wa kujifunza kutega ndege" anaongea Mkita akisimama karibu na Nzagamba akimwangalia kama kitoto cha mbwa kilichopotea njia na hatimaye kimeiona

" sio muda ulisema mimi sio rafiki mzuri" Nzagamba anamjibu akiendelea kufukia nguzo chini pasipo kumwangalia usoni " Mimi?mda gani?" anajibu akiinua mabega yake juu kama ndio kafika eneo hili.Nzagamba anainua kichwa chake pale alipochuchumaa na kumwangalia Mkita" unaweza kuniletea ile nguzo pale" anamwambia na Mkita anakimbia kama mshale kwenda kuichukua na kuwafanya wengine kutikisa vichwa vyao.baada ya muda anarudi na nguzo " hata hivyo haitasaidia kwa sababu maji yakikauka ndege nao watahama" anaongea Nzagamba na kumkata maini Mkita.

" itasaidia kwa muda,kwani mto wetu bado una maji mengi ya kutosha,kwa siku Moja Moja sio mbaya kwani kutakuwa Amna uwezekano wa kuwa na lombo Kila baada ya siku mbili" anaongea Kilinge na tumaini linarudi usoni kwa Mkita.Mkita mwenye familia kubwa ya watu nane sita wakiwa wanawake watupu pamoja na mkewe,baba yake Mzee sana ambaye hawezi kufanya chochote hivyo kumwacha yeye katika majukumu ya kuhudumia familia tangu akiwa na umri mdogo.

Wazazi wake waliwazaa dada zake na yeye Kuja kuzaliwa wa mwisho na wakati huo wazazi wake umri ukiwa umeenda amejikuta akibeba majukumu makubwa sana na ameyazoea kwa muda mrefu, akiwa Hana mtu wa kumsaidia amekuwa akifanya Kila kitu mwenyewe na marafiki zake wanalijua hili,hivyo humsaidia sana.wakati huu wa ukosefu wa wanyama unampa wakati mgumu sana akijua ataua familia yake kwa njaa,lakini Hana jinsi kwani Hali iko hivyo kwa watu wote.

" Mimi mwenyewe utakuwa unaniona sana tu" anaongea Ntula na wengine wote wakiitikia Mimi pia.Nzagamba anaona kabisa utulivu wake mtoni umeshavunjika kwani viumbe hawa wameshavamia baada ya kusikia neno karibu." najua familia zenu hazijazoea kula ndege" anajaribu kuwakwepa " hawana jinsi watakula tu,kama hawataki kwenda chini" anajibu Zinge.Nzagamba anawaangalia na kuendelea na kazi yake.

" hivi itakuwa ni kweli ni kutokana na laana kama hadithi zinavyosema" anaongea Ntula na wengine wote kuacha kazi zao na kumwangalia " unajua ile hadithi ya zamani iliyokatazwa kuzungumziwa" anaongezea akiwakumbusha " tunaijua hiyo,na kwa nini umeileta hapa kama unajua imekatazwa" Kilinge anaongea akiangalia huku na kule kama Kuna mtu mwingine amewasikia " hii inaudhi sana,makosa wafanye wengine adhabu tutumikie sisi" anaongea Mkita akifura hasira.

" walisema atazaliwa mtemi mwingine pamoja na mwanamke atakaye pewa nguvu za umiliki wa ardhi naona watazaliwa tukishakuwa mifupa chini" anaongea Zinge baada ya kuchoka kusikiliza. " haya mambo yameendelea kwa muda mrefu sana,na tunafanya matambiko Kila mwaka hiyo mizimu haijatusamehe tu" anaongea Ntula.

" kwani hamfanyi kazi au" kilinge anaongea asitake kabisa hii maada iendelee maana anajua madhara yake.familia za watu waliozungumzia hii maada endapo wakisikiwa ,hukutwa asubuhi wameuwawa mtu asijue nini kimewakuta na wanaojua hufunga midomo Yao kuhofia kukutana na hatima kama hiyo.

"Kilinge yuko sawa,kwanini tusirudi kazini" anaongea Nzagamba wote wanamsikiliza na kuendelea na kazi zao.wakati huo Nzagamba anahisi kuna mtu anamwangalia anaangalia huku na kule kwa umakini asione mtu ' kwani leo nina matatizo gani' anajiuliza akiendelea kuangalia " Kuna nini?" Mkita aliyemuona Nzagamba akiangalia huku na kule anamuuliza " Amna kitu,fanya haraka tumalize tuondoke kama hutaki kulaza njaa familia yako" Nzagamba anarudi kazini Mkita anaangalia huku na kule asione kitu anarudi kazini kumsaidia Nzagamba kuchimbia nguzo .

Mkita hakuwa peke yake aliyeona mabadiliko ya Nzagamba Zinge aliona hilo,ingawa yeye na Nzagamba hawako karibu kama kaka yake Kilinge, sababu ya mgawanyiko wa makundi na hawakwenda lindo pamoja ila anajua kuwa Nzagamba sio mtu wa kuwa makini pasipokuwa na sababu na hali aliyoionyesha hapa haikuwa ya kawaida hivyo moyoni anajua wazi Kuna kitu.Macho yake yanazunguka huku na kule asione kitu,anamwangalia Nzagamba na Kisha anarudi kwenye kazi yake.

Mbali kidogo na walipo juu ya mti akiwa amekaa Mnelela akiwaangalia walichokuwa wanakifanya " kijana anahisia kali kama walivyosema ndio maana wakuu Wana imani kuwa anaweza kumaliza hili,huuu,Nina bahati Mimi sio binadamu ingekuwa hivyo angeshanikamata mda mrefu" tawi linakatika kidogo aanguke.Nzagamba anahisi kitu na kugeuka ghafla kuangalia kule alikosikia sauti,,Zinge naye anageuka naye kwa wakati mmoja kwani naye alikisikia,anageuka na kumwangalia Nzagamba anaona bado anaangalia kule anawaangalia wengine anaona wakiendelea na kazi zao tu ikimaanisha hawajasikia ' nini kinaendelea' anajiuliza.Nzagamba baada ya kutokuona kitu anarudi kwenye kazi yake.

Mnelela anajitengeneza vizuri pale juu ya mti kijasho kikimtoka "kidogo nianguke" anajisemea utadhani akianguka atakufa wakati hata kudhurika hawezi." na yule kijana ni nani,imekuwaje ameweza kunihisi" anajiuliza akimwangalia Zinge " sio mtu wa kawaida" anajisemea.

Ndani Tulya na Sinde wakiwa wanaandaa chakula Tulya anakumbuka alichokisema Lingo mda uliopita "Sinde" anamuita naye anageuka na kumwangalia "mmh" anaitikia na kurudisha uso wake kwenye chungu kilichokuwa na ndege akiwatengeneza kwa ajili ya kuwapika " Lingo alimaanisha nini kusema kuwa mtu akienda kwenye ile milima milima gani vile" anauliza " nkyala" Sinde anamjibu " ndio,alimaanisha nini kuwa mtu akienda kule anakufa"

" ni kwa sababu ni mlima uliozuiliwa kuwindwa wanasema umelaaniwa na mtu akiingia kule harudi anakufa,na inasemekana wanyama wengi wanamezwa na huo mlima" Sinde anamwelezea akiwa anaendelea na kazi.mwili unamsisimka Tulya baada ya kusikia hivyo " umelaaniwa na nani?" anauliza akikaa kwenye kigoda karibu na alipo Sinde." hiyo ni Siri kidogo" anaongea Sinde akiangalia nje kama Kuna mtu na baada ya kuhakikisha kuwa Amna mtu akiongea kwa kunong'ona " hapo zamani za kale inasemekana mtemi Mmoja wa ardhi yetu alifanya dhambi kwa uchu wa madaraka,na alimuua mtu asiye na hatia ili ayapate" anaeleza Sinde kabla hajaendelea Tulya anamuwahi" usiniambie hadithi itaishia kusema mwanamke alikuwa mmliki wa ardhi na alikuwa anaitwa Ndesha" " umejuaje?" anauliza Sinde kwa mshangao " aliniambia mama,namaanisha mama mkwe,si ilitakiwa kuwa Siri umejuaje?" anamuuliza " ndio ni Siri watu wengine wanajua wengine hawajui au wote wanajua nakujifanya hawajui" " najua hilo,namaanisha wewe umejuaje"

" Tulisimuliwa kwenye kudua nikiwa mdogo"

" ndio nini hiyo"

" zamani kulikuwa na tamaduni wakati wa usiku na kukiwa na mbalamwezi,vijana na watoto wa umri kuanzia miaka mitano tulikuwa tunaenda kudua,maana yake kukusanyika wakati wa usiku na kupewa mafunzo kulingana na rika kwa wazee wetu"

" aaa mkusanyiko" anajibu Tulya

" ndio nyie mtakuwa mnaita hivyo kwenu,na sisi tunaita kudua,watoto wanaenda kusimuliwa hadithi,vijana wanaenda kupokea busara kwa wakuu na pia kusimuliwa hadithi wakati mwingine kucheza ngoma,

Siku hiyo Babu aliyekuwa anatusimulia hadithi ,alitusimulia hii na kwa sababu ilikuwa inavutia sana watoto wengi waliikumbuka na kuanza kuisimulia mtaani wakati wa mchana habari zikamfikia mtemi,yule Babu na familia yake yote wakauwawa na hiyo tamaduni ya kudua ikafutwa ikabaki tu ya vijana kukusanyika mara mbili kwa mwaka kupokea busara na ngoma"

" uliona akiuwawa?" Tulya anauliza " ndio,walinyongwa Mbele ya Wanakijiji kuzuia watu kuongea,nilipokuwa mdogo nilijua ni hadithi tu lakini Sasa nimejua kuwa huwenda Kila kitu alichosema yule Mzee ni kweli kutoka na majanga yanayotupata"

" kumbe mambo ni makubwa" anachangia Tulya.

" ndio,ni mwaka jana tu msimu uluopita sijui" anaongea Sinde akivuta kumbukumbu zake " Kuna Mzee mwingine alizungumzia,kesho yake akapigwa na radi mchana kweupe Amna hata wingu" " ekhee!?" anaitika Tulya kama kaitwa mwili wake ukipatwa na ubaridi kama Kuna mtu kammwagia maji ya mtungi asubuhi." ndio,wengine hukutwa ndani wamekufa,ni miezi kama mitatu tu iliyopita kabla hujaja familia nzima iliuwawa watu asubuhi wamekuta maiti tu,habari zikavuja kuwa waliuwawa na mizimu ya mtemi"

" mtemi anaamizimu?"

" ndio,inasemekana imekuwa ikiishi kwenye kasri lake kwa Karne na Karne,ikilinda kizazi chake ila watu wanasema ndio inayoongoza mtemi hasemi kitu,wakati mwingine humuamrisha mtemi kuchukua watu na kuwatoa kafara"

" oooh mizimu ya baba yangu,mtemi aliipata wapi na kwa nini asiitoe" anauliza Tulya.

" hawezi kuitoa kwa sababu waliingia makubaliano nayo na hawawezi kuyavunja,namaanisha mababu wa mtemi"

Baada ya kusikia makubaliano Tulya anakumbuka ile ndoto aliyoota yule mwanamke akimwambia mtemi kaingia makubaliano na mizimu wa baya,kijasho chembamba kinamtoka kwenye paji lake la uso " vipi kama haikuwa ni ndoto" anawaza Tulya.