webnovel

chapter 29

Kilinge na Zinge wanamwangalia kwa kutokuamini "unataka kufuga mbwa!?" Kilinge anamuuliza " ndio,umenisikia vizuri" anawajibu na kuwaangalia "naona na nyie mmerudi mikono mitupu" anachukua shoka lake na kuelekea kukata miti " Hali inazidi kuwa mbaya kila kukicha" anajibu kilinge akiweka mkono wake kiunoni " na nyie mna kibarua gani hapa?" anauliza Kilinge akiwaangalia Mkita na Lingo " tunatafuta ulaji kama unataka unaweza kuungana na sisi kwani hatuna mda wa kupoteza, jua linapanda" anajibu Mkita akienda kujiweka kwenye kazi yake ya kupunguza matawi ya miti iliyokatwa,Lingo nae akirudi kwenye kazi yake "sijawaelewa" anauliza Kilinge akiendelea kusimama.

"inaweza kumchukuwa mwaka huyo kuelewa" anaongea Zinge ambaye tayari alikwisha jiweka karibu na Mkita akianza kumsaidia kupunguza miti " Sasa hii miti inahusikaje katika kutega ndege" anauliza Kilinge baada ya kuelewa wenzake wanazungumzia nini " dada yako kipenzi anataka uwaa wa kutengenezea vyungu vyake, hivyo shemeji yako kipenzi hapa kaja kukata miti kwa ajili ya kutengenezea uwaa na sisi tumemkuta hapa tukamuomba atusaidie mlo wa Leo ndio katupatia sharti la kumsaidia hapa hivyo kama unataka usilale njaa changamka" Lingo anamsomea muhtasari.

Kilinge anatikisa kichwa kwa ishara ya kuelewa kinachoendelea anasogea alipo Lingo na kuchomoa sime yake kabla hajashika mti anamsikia Nzagamba akiongea " kwanini nyie wawili msikate majani" " nini?" anabwatuka Mkita na wengine wote kuacha kazi zao na kumwangalia Nzagamba " usiniambie tunafunika Leo" anauliza Kilinge " ndio " anajibu Nzagamba kama alichokisema walikipanga wote tangu juzi " tutachelewa bwana Nzagamba" analalamika Mkita "tutachelewa endapo mtakuwa mnaongea pasipo kufanya kazi" anaongea Nzagamba akiendelea na kazi yake ya kuangusha miti "haya umeshinda Leo wewe ndio umeshika makali,hayo majani tunayapata wapi?" anauliza Kilinge " tembeeni Mbele kidogo kama mnaelekea upande ule wa kisima mtaona mbuyu mdogo hapohapo" anawaelekeza " sawa wewe ndio mkubwa leo" anaongea Lingo akiondoka pamoja na Kilinge wakimwacha Nzagamba akitabasamu bila wao kumuona.

Nyumbani Tulya na Sinde wanarudi na kukuta pako kimya " watakuwa wameenda wapi hawa" anauliza kwa sauti utadhani alimwacha mlinzi nyumbani.wanahamisha maji ndani na kubeba vibuyu vyao kuelekea mtoni tena,pasipo kuangalia nyuma ya nyumba miti iliyorundikana pamoja na majani iliyoletwa na Nzagamba na wenzake kabla hawajarudi tena porini kuchukua majani na miti tena.

Wakati Tulya na Sinde wanarudi nyumbani tena wanasikia sauti za watu wengi wakiongea nyuma ya nyumba na kucheka na kelele za mapanga zikisikika " Kuna nini tena?" anauliza akiweka kibuyu chake chini Sinde naye anafanya hivyo " mbona hiyo kama sauti ya kaka Kilinge" anaongea Sinde na wote wanaanza kuelekea zinakotokea sauti na baada ya kufika huko wanashangaa kwa wanachokiona,Kila mtu akiwa na dhana mkoni wengine wakichimba mashimo,wengine wakichimbia miti kwenye mashimo " mnafanya nini?" anauliza wakati akiona kabisa kinachoendelea.

"umerudi"Nzagamba anaongea akiachia mti aliokuwa ameushika kidogo umpige kichwa Mkita naye anapiga mayowe " aaaah! kwa nini usiwe makini najua umemkumbuka bibi harusi wako,lakini mbona hii inazidi Sasa humuoni hata rafiki yako!?" anaongea akizidisha mbwembwe utadhani katolewa damu.Maneno yake yanamfanya Tulya kuangalia chini kwa aibu na Sinde aliyekuwa pembeni yake kucheka akimpiga bega.

Nzagamba anamwangalia Mkita na kuona Yuko sawa isipokuwa mbwembwe zake zisizomuisha na kuanza kutembea alipo Tulya na Sinde.

"mnafanya nini?" anauliza tena Tulya akimwangalia Nzagamba machoni,macho yake yanashuka kwenye mdomo wake mpaka kifuani.kifua chake kikiwa na unyevunyevu wa jasho lililotokana na kufanya kazi misuli ya kifua ikiwa imemkaa barabara na kumpendeza,mikono yake inamuwasha kwenda kwenye nyama za kifua hicho na kufanya utalii kadri iwezavyo lakini anahisi hata ikifanya hivyo sidhani kama itaridhika,Koo lake linapokea msafara wa funda la mate aliyomeza likishangaa tangu lini kumekuwa na msongamano wa mate.

Nzagamba anakohoa kidogo kama anasafisha Koo na Tulya anatoa macho yake kifuani na kupeleka usoni akitikisa kichwa chake kuondoa fikra mbaya." uko sawa ?" anamuuliza 'nitakuwaje sawa wakati umesimama Mbele yangu namna hii' anawaza moyoni na kusema " ndio,mnafanya nini?" anauliza tena swali lake.Nzagamba anakuna nywele zake zilizosokotana kichwani nakusema" tunajenga uwaa" "ndio,najua lakini mbona hivi,namaanisha haikuwa na haraka kiasi cha kuita watu kukusaidia tungejenga tu polepole" anaeleza na kabla Nzagamba hajaibu Mkita aliyekuwa amejisogeza karibu kabisa na walipo analipuka " unajua shemeji,tulimkuta mumeo huko porini akikata miti sisi tukiwa tumetoka kuwinda pasipo kupata kitu lakini" anaeleza na kusimama kidogo akimwangalia Tulya kama habari imemwingia "Mkita" anasikia onyo la Nzagamba lakini hakuwa tayari kuacha nafasi ya kumsemea Nzagamba kwa kuwafanyisha kazi Ili awapatie chakula " unamaanisha nini pasipokupata kitu" anauliza Tulya macho yake yakienda kwa Nzagamba na kwa wengine Kisha kutua tena kwa Mkita.

"hawezi kujua huyo" Lingo anamkumbusha Mkita " aaa!" anasema Mkita baada ya kukumbuka kuwa Tulya ni mgeni hapa " Kuna uhaba wa wanyama kwa hiyo uwindaji umekuwa wa shida sana kupata wanyama ni mpaka uende mbali na kwa mtu Mmoja haiwezekani" anaeleza Kilinge " ni mbaya kiasi hicho" anauliza na wote wanamwitikia kwa ndio " lakini kipindi Cha nyuma mbona nilikuwa naona mnakuja na nyama za kutosha tu" anauliza " tulikuwa tunatembea umbali mrefu sana kuwapata na hii ilikuwa inachukua siku mbili mpaka tatu" anaeleza Zinge na Tulya anabaki akiwaangalia " au uende milima nkyala kama unataka kufa lakini" anaongezea Lingo akiweka ugolo wake mdomoni na sura yake kujawa furaha kama wamekutana na rafiki ambaye hajaonana naye kwa muda mrefu." kivipi?" anauliza Tulya " aaa, tuachane nayo turudi kwenye maada" Mkita anaingilia " Sasa ndiyo hivyo,tulipokosa wanyama tukaona tumuombe mumeo kipenzi au rafiki yetu kipenzi,kwa sababu yeye ana ulimbo na mitego atusaidie kwenda kutega ndege huko mtoni kwenye lindo lake Ili tupate kitoweo Cha siku mbili hizi mpaka pale uongozi wa uwindaji utakapokuja na mpango wa sisi tule nini,ndio akatupatia hicho kibarua hapo kasema tumsaidie kwanza ajenge uwaa wa mkewe kipenzi ndio atatusaidia" anamaliza Mkita akimwangalia Nzagamba aliyekuwa anaangalia kwingine akikwepa macho ya Tulya.

" unajua shemeji" anaongea Tulya akimwangalia Mkita na wengine " hakuna Cha bure hapa duniani" anaongea na kumfanya Mkita na wengine kumwangalia kwa mshangao,macho ya Nzagamba yanarudi usoni kwa Tulya huku Zinge akitoa tabasamu la nilijua tu yatakuwa haya " ekhe!?" anashangaa mkita " ndio,ukitaka kitu lazima ukitolee jasho ili matunda yake yawe matamu,ndicho nilichojifunza kwa wazee wangu" anaongea akikunja mikono yake kifuani chini kidogo ya saa sita yake na kufunika kidogo tumbo lake lililokuwa wazi likionyesha kitovu chake pamoja na kiuno chake upande wa mgongo uliokuwa wazi pia.shanga za kiuno zikipendezesha kiuno chake kidogo kama nyigu 'ukamilifu mkubwa' anawaza Nzagamba aliyekuwa anamchora Tulya.

" isitoshe Sasa bado ni asubuhi kwenda kutega kwa hiyo changamsha damu kidogo" anamalizia akimwangalia Mkita kwa tabasamu " siamini kabisa kinachotokea,nilijua utamwambia tabia mbaya hiyo,inabidi uwasaidie marafiki zako wanapokuomba kitu pasipo kutaka kitu" anajaribu kumshawishi " ndio ninachozungumzia hapa, Nzagamba kakuomba msaada inabidi umsaidie" "kaniomba saa ngapi?" anauliza Mkita " kama hivi unavyojenga uwaa hapo" Tulya anamjibu.

" Mkita kapata saizi yake" anaongea Lingo kwa sauti ya chini lakini Zinge aliyekuwa karibu yake anamsikia na kucheka " wahenga wanasema wanandoa wakikaa mda mrefu huwa wanafanana,mbona kama nyie mnaenda haraka zaidi" anaongea Mkita na wote wanasikia kicheko wanageuka na kumuona Ntula aliyefika mda mrefu akiangalia Tulya na Mkita wakibishana " Mkita umepata kiboko yako" anaongea akiendelea kucheka " umefika saa ngapi?" anauliza Lingo " tangu ulipokuwa unafurahia kukutana na ugolo wako" anamjibu na wakati huo Lingo anatema mate yake pembeni.

Anawageukia wengine " tabia gani hii ya kukutana pasipo Mimi" anawauliza " umejuaje kama tupo hapa" Kilinge anamuuliza " nimepata taarifa kutokana na upepo" wenzake wanamwangalia na anaendelea " nememsikia Manumbu akiongea na kuwataja kama karanga za mbegu nikajua Kuna uhondo nimeukosa,nikaamua nitafute hata makapi tu" anaongea na Tulya anamwangalia Nzagamba " Amna kitu usijali" Nzagamba anamwakikishia " karibu kwenye uwanja wa vita" Mkita anamkaribisha akirudi sehemu alikokuwa anafanyia kazi.

Nzagamba anamwangalia Tulya " unaweza kuandaa chakula cha kutosha kwa watu wote hawa" " ndio usijali,sinde atanisaidia" " sawa" anaitikia akiondoka kabla hajafika mbali anamsikia Tulya akimuuliza " mama kaenda wapi?" " sijui,niliporudi hakuwepo,usijali atakuwa hajaenda mbali kama hajaaga" anamjibu " sawa" anamvuta Sinde na wote wanaelekea ndani." haya kama mmemaliza kulalamika turudi kazini kama hamtaki saa nane itufike hapa" anaongea Nzagamba akimwangalia Mkita.