webnovel

Jitafute.

Mambo yalianza tangu nilipokuwa mtoto, karibia au kuanzia miaka kumi na ushehe hivi.

Sio mbali sana tangu nilipozaliwa, kwa maana, sikujua kama nilikua nakua.

Nilisanuka tu nikiwa na miaka kama kumi hivi, hiyo ndiyo sababu miaka kumi sikuona kuwa ni mingi. Lakini kama ingekua ni safari ya kutembea kwa chopa, au ndinga, baiki au miguu, basi ningekuwa nimefika mbali sana tena hata labda nje ya sayari dunia.

Mishemishe zilianza nilipoanza kucheza tu, nilicheza michezo mingi lakini miongoni mwa michezo ninayo ikumbuka ni ndondi.

Nilipenda kupigana, nyumbani, shuleni, mchana na usiku huku ndani ya kinjunga nilichovaa kulikuwa na chupi iliyoandikwa jina la nyota wa masumbwi, chuma, Mike Tyson, labda nilitaka kuwa kama yeye.

Mama hakupenda nipigane, alisema baba yangu alikuwa mkorofi enzi za ujana wake.

Siku nilirudi nyumbani nakimbia, nilipofika nilimkuta mama yangu amekaa sebreni, nikatoka nduki hadi chumbani kwangu, tayari nilikua nimeshampiga mtu.

Siku nyingine nilirudi nyumbani shati yangu nyeupe ya shule ikiwa imepakaa mchuzi wa maharage, damu iliyonimwagikia kutoka wa mpinzani wangu niliyempiga Kei O nikiwa daraja la sita huko shule ya awali chidya ilioko kusini mwa Tanzania na Mtwara.

Nilipofika darasa la tisa (9) nilijikuta sipendi tena kukunja ngumi, sikuhitaji tena kuona mtu anatokwa damu kwa ngumi yangu, labda kwa sababu ya yale maneno yake mama, " usiwe kama baba yako".

Kule sekondari nikajikuta kwenye mahab a mazito na muziki, nikaanza kujiona kwenye sayari ile ya muziki.

Mimi na rafiki yangu Fred tulikuwa Tim Mondi, Andrea yeye alikuwa Tim Kiba, wao ndio wasanii waliobamba na kutikisa kipindi kile.

Niliamua kupunguza upendo kwenye kiwanda cha disko baada ya soka kunipa marafiki wengi zaidi ambao wengi wao ni wakike nikiwa kidato cha tatu huku tukiwataja wachezaji bora wa muda ote, Gaucho na Kaka wa Brazil.

Nikiwa kwenye kabumbu nilifunga hata kile tunachoweza kukiita UTATU MTAKATIFU, yaani, mimi peke yangu kufunga magori matatu ndani ya mechi moja, huku ndipo nikabatizwa ile lakabu yangu ya Snepa kwa uwezo wangu wa kushuti nikiwa mbali na kulenga gori.

Nilikuwa hivo hata nilipofika sekondari ya juu na ubora wangu ulikua juu zaidi na jina langu likatajwa akwino kote kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita.

Hadithi yangu ya maisha ilianza kubadilika nilipofika chuo, nadhani hata washkaji zangu walishangaa kuona spendi tena kusakata bori,

"Unazingua wewe"

waliniambia wana, hata mwenyewe sikujua napenda nini tena, si mpiganaji, si mwanasoka.

Nikirudi toka kwenye kipindi, basi nitaokota tu peni yangu na kuanza kuandika mashairi kisha kulala.

Ambacho kimebakia mkononi mwangu ni karamu tu, hapo ndipo nikagundua kuwa, karamu ndiyo silaha yangu baada ya kujikuta nimeandika mashairi kadhaa, na riwaya hata leo nina tamthilia chache.