8 CHAPTER 7

Fahamu zilimrudia Janat. Alifumbua macho taratibu. Kichwa kilimuuma na alihisi kizunguzungu. Ingawa macho yaliona ukungu, alijua ya kuwa hayupo kwenye gari wala nyumbani kwake. Mwanga wa chumba alichokuwepo ulikuwa umefifia. Hii pia ilimfanya agundue kuwa nje kulikuwa giza. Mkono wake wa kulia ulikuwa mzito kutokana na dripu ya maji iliyokuwa ikikaribia kuisha. Sasa bila shaka aligundua kuwa yupo hospitali. 

Mlango ulifunguliwa na Ariana aliingia ndani. Alikuwa na chupa kubwa ya maji ambayo ilikuwa imebakia robo tu. Alipoona ya kwamba Janat ameamka aliwahi pembeni ya kitanda. Alivuta kiti na kuketi haraka. Uso wake ulikuwa umepauka kwa mawazo na wasiwasi.

"Boss, unajisikiaje?", Ariana aliuliza huku akimkagua Janat kwa macho.

"Nini kinaendelea?", aliuliza Janat kwa sauti ya chini.

"Ulipoteza fahamu ukiwa ndani ya gari. Kwa bahati nzuri wasamalia wema walikutoa kwenye gari na kukuwahisha hospitali ya karibu. Mmoja alichukua simu yako na kunipigia mimi.", Ariana alielezea.

"Walinipeleka hospitali gani?",

"Ilikuwa ni dispensari, ila nilivofika nikaomba tukulete hapa. Upo Aga Khan.",

 Janat alianza kupata kumbukumbu, "Ni habari gani ambazo zinatrend sasa hivi?", aliuliza.

"Kila mtu anakuongelea wewe. Waandishi wa habari wamefurika hospitali ya Muhimbili na Amana kuwahoji walioathirika na cancer. Asilimia themanini wamesema ni pedi za Upendo toleo la kwanza ndio sababu. Kuna uwezekano mkubwa wa kufunguliwa mashitaka hivyo utahitaji mwanasheria mzuri.",

"Nini kingine?",

"Waziri Magambo amenipigia simu. Anasema fanya ufanyavyo uiambie nchi kwamba wewe na yeye hamna ukaribu. Pia ameondoa jina lako kwenye list ya wataokwenda Australia.",

"What?", Janat alivunjika moyo, "Kwanini ametoa jina langu?",

"Nahisi ni njia moja ya kukukomoa. Isitoshe wawekezaji wetu wote wamepull out their investments kutokana na hii scandal inayoendelea.",

"Impossible!", Janat aliweweseka. Yote aliyosikia yalikuwa kama ndoto mbaya iliyomtisha sana. 

"Serikali imesimamisha bidhaa zetu zote zisiingie sokoni mpaka utafiti mkubwa ufanyike. Imebidi tukabidhishe vitabu vyetu vyote kwa mkaguzi mkuu wa serikali. Hatujui yatakayojiri.",

Kwa mara ya kwanza Janat hakuweza kuona njia ya kutokea. Alizungukwa na giza na hakukuwa na tumaini la mwangaza.

"Nifanyeje?", Janat aliuliza kwa unyonge.

"Boss, huna budi kumtafuta huyu mtangazaji.", alisema Ariana, "Sasa hivi nchi haiwezi kukusikiliza bali yeye. Ukishajua yeye ni nani unaweza kumuomba aishawishi nchi ya kuwa vyote vinavyoendelea ni fitna. Kama waziri alivyokutupia baharini, na sisi tutamtumia yeye kama njia ya kutokea.",

"Kivipi?",

"Tutawaambia watu kuwa waziri alikutaka kimapenzi, na ulivyomkataa akafanya yote haya ili kukuharibia.",

Janat alianza kupata matumaini. Wazo alilotoa Ariana lilikuwa wazo zuri. Ugumu ni kwamba mtangazaji yule alikuwa ni kama upepo, unausikia lakini hauwezi kuuona wala kuushika. Pamoja na yote bado Janat alifanya uamuzi wa kumsaka, hata kama itamfanya atumie mamilioni ya pesa. 

...

"Tumebaki mimi na wewe tu.", alisema Annabella kwa wasiwasi.

Japokuwa kazi zao ziliwafanya wawe bize, habari zilizokuwa zikisambaa nchini ziliwafanya watafute nafasi ya kukutana. Tayari Suzy na Janat walikwishakumbwa na majanga. Sasa macho yote yalikuwa kwao, na kati yao wawili, yaani, Annabella na Leah, Annabella alikuwa na mashaka makubwa.

Walikutana kwenye mgahawa uliojificha.

"Unahisi tufanyeje?", bado Annabella aliendelea kuuliza.

"Kwanini una wasiwasi hivyo? Umeua mtu?", Leah aliuliza bila kuonesha dalili ya hamasa wala woga,

"What? No.",

"Sasa kwanini unaogopa? Kama hauna cha kuficha ondoa uwoga endelea kupiga kazi.",

"Natamani ingekuwa rahisi hivyo.",

"Unamaanisha nini?",

Annabella alipepesa macho akimkwepa Leah, "Kila mtu ana siri ambayo hayupo tayari dunia ijue.", Annabella alisema, "So, nina siri ambayo sitaki mtu yoyote ajue.",

"Kila mtu ana siri, ni kweli. Kama umeiweka moyoni na hakuna mtu yoyote anayeifahamu, usiwe na wasiwasi. Huyu mtangazaji sio mchawi na wala sio Mungu. Hawezi akajua kila kitu.", alisema Leah.

"But what if amejua? Kuna kitu ndani yangu kinaniambia kabisa kuwa she knows. I don't know what to do.",

"How bad is it?",

"So bad.", Annabella alivuta pumzi, "If she reveals it, I think I'll kill myself.",

Leah alisogeza kiti chake mbele, "Anna, niambie ukweli; Are you sure you haven't killed a person?", alinong'oneza.

"Depends on how you define killing.",

Jibu lilijieleza. Leah hakuhitaji maelezo zaidi. Taratibu alirudi kuegamia kiti chake. 

Asubuhi na mapema redio zilikuwa wazi, kipindi pendwa kilikuwa hewani;

"Mama ni nani?", aliuliza mtangazaji wa redioni, "Wanasema kuwa mama ni zawadi kutoka kwa Mungu. Ukimdharau mama yako huwezi kuingia peponi. Swali linakuja; Mama ni nani? Ni kitu gani kinakufanya uitwe mama? Je, ni kubeba mimba miezi tisa?",

Annabella alikuwa peke yake ofisini. Hakutaka mtu aingie hivyo aliloki mlango. Juu ya meza kulikuwa na risasi ambayo alikuwa akiihesabia dakika tu.

"Kama kuwa mama ni kubeba mimba miezi tisa; Je, tunawaitaje wanaojifungua na kutupa watoto wao vichakani? Je, hawa tunawaita mama pia?", mtangazaji aliendelea, "Okay, tufanye ameibeba mimba miezi tisa na akajifungua salama bila kumtupa mtoto wake. Lakini mzazi huyu akaanza kumuonea wivu mwanae na kumnyanyasa. Je, huyu pia ni mama?",

Mlango wa ofisi ya Annabella ulianza kugongwa kwa nguvu. Mlinzi wake, Thomas, alikuwa akijitahidi kuufungua kwasababu aliotea hatari iliyokuwa ikijongea.

"Mama ni neno kubwa sana.", alisema mtangazaji, "Swali kwa Annabella; Je wewe ni mama? Katika vitu ambavyo sikutegemea kujua kuhusu wewe ni hichi. Stori yako ilinigusa sana, kuanzia ulipoolewa ukiwa na umri mdogo, kupendwa sana na mume wako na hatimaye kurithi biashara zake zote baada ya kifo chake. Lakini kabla mume wako hajafariki, ulikuwa tayari una ujauzito, lakini ujauzito huu haukuwa wa kwake bali wa mdogo wake.",

Annabella aliikamata risasi na kuanza kuielekezea kichwani pake.

"Haukutaka mume wako wala baba halali wa mtoto kujua, uliifanya iwe siri yako kwasababu kama ingegundulika, kwanza ungefukuzwa, ungeachwa mtupu kama alivyokukuta kijijini kwenu. Kwa bahati nzuri au mbaya, mume wako alipata ajali ya ndege iliyomuua, na kutokana na sheria wewe ndiye ukawa mrithi mkuu. Lakini ulijua familia ikijua una ujauzito, mali zitahamia kwa mtoto. Hivyo ukajifanya kusafiri kwenda Italy mwaka mzima kutuliza akili, kumbe ulienda kujifungua na baadaye kumuacha mtoto wako kwenye nyumba ya masista wa kanisa katoloki.",

Annabella alikoki risasi. Mlinzi wake alizidi kugonga mlango kwa nguvu. 

"Binti yako ametimiza miaka 20. Ni vizuri kama angepewa haki yake. Au unataka umsikie mwenyewe akisema? Haya ngoja nimuunganishe.",

Annabella alishtuka na kutupa macho yake kwenye laptop aliyokuwa akiitumia kusikiliza habari zile. Hakutaka kuamini kuwa anakwenda kusikia sauti ya binti yake kwa mara ya kwanza toka amzae. Bella hakuwa na mahusiano na binti yake. Alimfahamu tu kwa picha alizokuwa akitumiwa na mama mlezi wa kituo hicho cha masista.

"Mama, it's me, Cassidy.", aliongea binti yake kupitia redio. Mfumo wa sauti ulithibitisha hayupo studio bali mtangazaji yule alimuunganisha kupitia simu, "I don't even think it's fair to call you mom since you abandoned me. Look; I don't need your money. All I want is for you to repent and live the rest of your life knowing that you had a wonderful daughter and you gave her up for something so stupid. Hell might just be a concept, but I truly hope it becomes real for you.", 

Annabella alidondosha risasi bila kujua, na kabla haijatua chini, Thomas alifanikiwa kuvunja mlango na kuingia ndani kwa fosi. Alikuwa amelowa jasho, macho yakiwa wazi kama ameona jini. Alimkuta Annabella akitetemeka kwa hasira, chemchemi ya machozi ikilowesha uso wake ambao sasa ulielekea kuwa mwekundu. Alikunja vidole vyake kama ngumi. Thomas hakuwahi kumuona bosi wake akiwa na hasira ya kile kipimo.

"How dare she?", Annabella aliuliza bila jibu, "Kwanini amethubutu kuchimba maisha yangu? Anajua nini? How dare she brings my daughter into this mess?",

Kwa kumendea ili asimshitue bosi wake, Thomas aliinyatia risasi iliyokuwa sakafuni kabla Annabella hajashituka. Kwa bahati nzuri aliweza kuifikia na kuiokota.

"Anahisi anaweza kunihukumu mimi? Anajua niliyoyapitia mpaka nimefika hapa? Who the fuck does she think she is?", Annabella alibamiza meza kwa hasira na kunyanyuka. Alikuwa kama kifaru awindaye, "She messed with a wrong girl!", aliunguruma, "Nikimjua ni nani, tamfanya ajutie maisha yake yote. Naapa kwa Mungu.",

Wafanyakazi waliokuwa wamesimama nje ya mlango walianza kuondoka taratibu. Wengi walimuona kama kichaa, na wachache walimuhurumia. Alibadilika ghafla na kuwa mtu tofauti sana. Siri hii alijitahidi kuificha kutokana na sababu zake binafsi, na ilionekana kwamba haikupita hata siku moja bila yeye kujutia uamuzi alioufanya. Lakini hakutaka kurudi nyuma. 

Kitendo cha mtangazaji yule kutoboa siri hiyo, na isitoshe pia kumuunganisha binti yake ambaye ametamka maneno makali kimeenda kutonesha donda alilokuwa nalo moyoni kwa miaka yote ishirini. Hakutaka kupotezea jambo hilo.

***

avataravatar
Next chapter