6 CHAPTER 5

Leah alikuwa jikoni akipika chakula cha jioni. Paul hakuwepo nyumbani, kitu ambacho hakikuwa cha kawaida kwani ilikuwa ni weekend, na siku zote walibaki nyumbani au kwenda sehemu pamoja na si tofauti. Japokuwa halikumpa Leah mawazo, bado ilimpatia maswali machache. Hizo siku mbili tatu, Paul hakuwa kama Leah alivyomzoea.

Wimbi la wasiwasi lilimpiga. Kwa haraka aliweka chini beseni la mchele na kuondoka jikoni. Aliifata simu yake iliyokuwa chumbani ikipata chaji. Alipoiwasha hakukuta simu wala meseji kutoka kwa mume wake. Nyingi zilikuwa kutoka kwa watu wengine, zote zikiongelea habari za Suzanne.

Leah alienda kwenye namba ya mume wake na kumpigia simu. Huku akisubiri apokee, hakuweza kukaa kitako. Alitembea mbele na nyuma, mkono mmoja ukiwa kiunoni. 

Paul alipokea hatimaye, "Hello.", aliongea,

"Upo wapi?", Leah aliuliza.

"Nipo kwa mama. Kuna kitu namsaidia kufanya.",

"Kitu gani?",

"Kitu cha kawaida tu.",

"Tokea asubuhi?",

Kimya.

Leah alitizama simu yake na kuirudisha tena sikioni.

"Paul?", aliita.

"Nakusikia.", Paul alijibu.

"Nijibu swali langu; ulikuwa unamsaidia tokea asubuhi?",

"Ndiyo.",

"Mbona hujaniaga wala kunipigia simu? What if I had plans for today?",

"Mama yangu alihitaji msaada. Ulitaka nifanyeje?", ingawa alijitahidi kuficha, bado sauti yake ilibeba ukali.

"Nilitaka taarifa. Siku zote huwa tunapeana taarifa. Nilitaka uniambie hicho unachoniambia sasa hivi mapema.", Leah alizungumza.

"Okay. Yaishe.",

"Jana mbona ulichelewa kurudi? Ulikuwa wapi? Mbona hata chakula haukugusa?",

"Leah, mimi si mtu mzima lakini? Mbona unaniuliza maswali kama mtoto?",

"What?", Leah alishangazwa na kauli ile, "Umeingiliwa na nini, Paul? Mbona sikuelewi siku hizi?",

"Leah, come on.",

"Hivi upo kweli kwa mama yako au unanidanganya? For what?",

Leah alisubiria jibu kwa hamu lakini jibu lilikuja na sauti ambayo siyo ya Paul.

"Leah, hujambo?", aliongea mama Paul.

Leah alishtuka, "Mama? Shikamoo.",

"Acha kukwaruzana na mume wako kwenye simu. Mpikie chakula, anakuja.",

"Mama _", sentensi yake ilikatishwa baada ya simu kukatwa. 

Leah alikunja vidole vya mikono yake kwa hasira. Alihisi kuna kitu kinaendelea, ila hakufahamu ni kitu gani.

Usiku mzima usingizi haukumpata Suzy. Kila alipofumba macho aliona maisha yake yakimong'ongyoka kama udongo. Alikuwa akijiuliza maswali mengi bila majibu;

"Huyu mtangazaji ni nani na amejuaje yote haya?", alijiuliza kimoyomoyo, "Najua hajakutana na Flaviana, so ni nani kamwambia?", 

Kichwa kilimuuma sana. Alishangaa pale kengele ya saa yake ya mezani ilipoanza kulia. Ilikuwa imekwishafika saa kumi na mbili asubuhi. Muda ulienda wapi?

Simu yake alikuwa kaizima na kuiweka mbali na yeye. Hakuwa na nguvu za kukabiliana na siku nyingine ya maumivu na ukali wa ulimwengu. Ila ni jambo moja tu lililomtoa kitandani asubuhi ile. Kuna mahali alipaswa kwenda.

Baba Suzy alisimama barazani akitizama gari ya Suzy ikipita getini. Sura yake ilikunjika kwa hasira aliyokuwa nayo. Ilikuwa ni mara ya kwanza yeye kumuangalia Suzy bila kumtambua. Yule Suzy, damu yake, binti yake aliyekuwa akimuona tangia mtoto mchanga hakuwa yule Suzy aliyekuwa akishuka kwenye gari yake. Kama mzazi, ilikuwa ni kama mtu amechomeka kisu katikati ya moyo wake na akiendelea kukididimiza ndani kwa nguvu.

Suzy alihisi macho ya baba yake yakimtazama. Kwa aibu alitizama chini na kufanya kila mbinu ya kukwepa uso wa mzee wake.

"Shikamoo baba.", aliamkia kwa sauti ya chini na ya kukwaruza. Hii ilitokana na kilio cha usiku kucha.

"Siamini nilichosikia.", baba Suzy alisema kwa mshangao kisha kufungua mlango na kuingia ndani.

Suzy alimfata baba yake kwa uwoga. Alipofika sebuleni alimkuta mwanasheria wa baba yake akiwasubiri. Alikuwa ni mwanaume, mtu mzima. Kulikuwa na makaratasi na kalamu juu ya meza. Suzy alisita kupiga hatua nyingine mbele. Alisimama palepale alipokuwa. 

Baba Suzy aliketi na kumpa uwanja wa maelezo mwanasheria wake.

"Suzanne, naamini umesikia kila kitu kinachosemwa kuhusu wewe.", mwanasheria alizungumza, "Jana niliweza kukutana na Flaviana na amenisimulia kila kitu. Tunavyoongea, Flaviana ametolewa hospitali ya St. Monica na amepelekwa hospitali ya Muhimbili kufanyiwa general checkup. Baada ya hapo, Flaviana anarudi nyumbani rasmi.",

Suzy hakuweza kufunua mdomo wake. 

"Tumeweza kuthibitisha kuwa msingi mzima wa kampuni yako umeibwa kutoka kwenye file la Flaviana. Kila kitu kutoka business proposal, michoro, expectations na njia yako nzima ya kuendesha biashara hii imetoka kwenye akili ya binamu yako. Hivyo, familia yako imeamua kukuvua madaraka na kumkabidhi Flaviana.",

"What?", Suzy alishtuka, "Mnivue madaraka? I'm the fucking CEO of my company! Hamuwezi kunivua cheo changu.",

Baba Suzy aliuma meno kwa hasira.

"Suzanne, hivi unafahamu kuwa jambo ulilomfanyia binamu yako ni kosa la jinai?", aliuliza mwanasheria, "According to the law, unatakiwa uwekwe jela for many years, ila Flaviana amekataa kufungua mashitaka. Hauna jinsi; either uvue madaraka, au uende jela.",

Suzy alikimbia kwenye miguu ya baba yake na kupiga magoti. Machozi yalimbubujika kama chemchemi, jasho likitapakaa kwenye viganja vyake. Kwa uchungu alikamata mguu wa baba yake.

"Baba nakuomba, please usinipokonye kampuni yangu. It's all I have.", Suzy alilia.

"Kwanini ulimfanyia Flaviana ukatili wa namna hii? Alikukosea nini?", baba Suzy aliuliza bila kumtazama Suzy machoni.

"Baba, she had everything! Wewe na mama mlimfanya kama mtoto wenu na kunisahau _",

"Hakuna aliyekusahau! Wewe ulijazwa wivu! Flaviana hakuwa na kila kitu. Binti wa watu alifiwa na wazazi wake kwa mpigo. Alikuwa na sisi tu. Alifahamu hilo na ndio maana alijitahidi sana shuleni na kwenye maisha. Lakini wewe badala ya kufata nyayo zake, ukaona umuharibie.",

"Baba please _",

"Siwezi kukusamehe. Hata mama yako angekuwa hai asingekusamehe. Umenivunja moyo, Suzy. Siamini kama wewe ni katili namna hii. Sina mtoto kama wewe.",

Suzy alilia kwa uchungu.

"Hapo mezani kuna makaratasi yanayohitaji sahihi yako. Moja; kuhamisha madaraka kwenda kwa Flaviana. Mbili; I disown you.",

"Baba no!",

Baba Suzy alisimama na kutoa mguu wake kutoka kwenye mikono ya Suzy. Aliondoka sebuleni kwa haraka. Halikuwa jambo rahisi yeye kumkana Suzy. Moyo ulijawa na maumivu makali, hasahasa kila akisikia kilio cha Suzy kikitokea sebuleni. Ingawa alimpenda mwanae kwa dhati, aliona kumuadhibu namna ile ndio njia pekee ya kulipa mabaya aliyofanyiwa Flaviana. Na hata akifariki, aliona ni jambo pekee litalompatia nguvu ya kukabiliana na wazazi wa Flaviana waliotangulia mbele za haki.

Usiku uliwasili na Suzy alikuwa ameketi juu ya kitanda chake. Alikuwa amevaa gauni zuri jeupe, refu la kufunika miguu. Nywele zake alikuwa amezibana vizuri na sura yake ilikuwa na kipodozi kilichotulia. Juu ya mto wake kulikuwa na barua yenye mwandiko wake. Na mkononi mwake alikuwa amekatama glasi ya maji, huku mkono wake wa kushoto ukiwa umejaa vidonge vya kila rangi. Idadi ya vidonge vile ilifika kumi. Alikuwa tayari kuiaga dunia.

Hofu kubwa ilimvaa. Aliogopa kifo. Kwa uovu aliomfanyia binamu yake alijua hukumu yake itakuwa ni moja kwa moja jehanamu. Ila aliona ni bora hivyo kuliko kuishi kwenye ulimwengu ambao alichukiwa na kila mtu.

Suzy alianza kupeleka mkono wenye vidonge mdomoni mwake, lakini ghafla kengele ya mlangoni kwake ililia, tena kwa sauti iliyomshitua na kumfanya adondoshe vidonge vile juu ya gauni lake. Hakujua ni nani yupo malangoni kwake. Alinyanyuka haraka kitandani na kwenda kufungua mlango. Alishuka ngazi kwa haraka, moyoni akiomba awe ni baba yake amekuja kumsamehe. Lakini aliganda pale alipofungua mlango na kumkuta Flaviana.

Flaviana alikuwa na muonekano wa tofauti sasa. Alikuwa msafi na kuvaa mavazi maridadi. Flaviana alimtazama Suzy kuanzia juu mpaka chini kisha kutikisa kichwa.

"You're very weak.", alisema Flaviana, "Kitu kidogo tu unataka kujiuwa?", 

"Nani kakwambia _",

"Inaonekana ulikuwa unaogopa kufa na mikono yako ilikuwa inatoka jasho. Vidonge vilivyolowa vimeacha madoa kwenye gauni lako.",

Suzy alitizama gauni lake, sehemu alipoangushia vidonge. Kweli kulikuwa na madoa ya bluu, kijani na pinki.

"You win Flaviana.", Suzy alizungumza akiuma meno kwa hasira.

"Hauna hamu ya kujua nimewezaje kukumbuka yote haya?", Flaviana aliuliza.

"I don't care.",

"What about kujua mtangazaji amepataje information zako?",

"Si wewe ndo umemwambia?",

"Believe it or not, sijakutana na mtu yoyote isipokuwa wewe na manesi. I'm really curious kujua huyo mtangazaji ni nani na amejuaje yote haya.",

"Ili iweje? Una kila kitu sasa hivi.",

"Nataka nimshukuru kwa kunifanya niwe huru.", Flaviana alijibu,

"Mtafute mwenyewe umpe shukrani zako. I don't care anymore.",

"Actually, nimekuja hapa to make a deal na wewe. I want you to find out who that girl is.", 

"Wewe, embu sikiliza, she's untraceable. And by the way, huwezi kuniamrisha nikufanyie kitu.", Suzy alijibu kwa jeuri.

"Nimesema ni deal which means ukinisaidia kuna kitu utapata. Ukiweza kumjua huyo mtangazaji ni nani, takufanya raisi msaidizi wa kampuni yetu, na ninaweza nikakusamehe pia. Unajua nikikusamehe, baba yako pia atakusamehe, right?", 

Taratibu, Suzy alianza kuwa mpole.

"Niletee taarifa kuhusu huyo mtangazaji na kila kitu ulichopoteza kitarudi kwako. I might even tell waandishi wa habari kuwa ni misunderstanding na kwamba wewe ni binadamu mzuri na mtu pekee ninayemwamini. Si unajua, ili nikusafishie jina lako watu wakuone kama mtakatifu.",

"Kwanini unataka ufanye hivyo? Kwanini unataka kunisaidia?", Suzy aliuliza,

Flaviana alicheka kidogo na kumshika Suzy begani, "Mimi sio katili kama wewe. So don't kill yourself, cousin.",

Flaviana aligeuka na kuondoka. Kuna gari ilikuwa ikimsubiri. Huku, Suzy alikuwa ameona mwanga, njia ya kurudisha maisha yake. Aliapa kumsaka na kumjua mtangazaji huyo.

***

avataravatar
Next chapter