19 CHAPTER 18

Leah alikuwa peke yake kwenye chumba cha mahojiano. Aliviangalia viganja vyake vilivyofungwa kwa pingu. Ilikuwa kama ndoto. Kila jambo alilofikiri halikumpatia jibu alilokuwa anataka. Alitamani kulia lakini hakutaka kuonekana dhaifu. Hakujua afanyeje? 

Reuben na Joy waliwasili na kuketi mbele ya Leah. Leah alimtazama Reuben kwa macho makavu yenye kiu ya kujua kinachoendelea. 

"Leah Shahidi; unamfahamuje Cecilia?", Reuben aliuliza,

"Mpenzi wa mume wangu Leah alijib.",u,

"Umewahi kukutana naye kabla ya leo?",

"Ndiyo. Nilienda kumtembelea jela.",

"Ukamwambia nini?",

"Aachane na Paul na mimi tamsaidia akae vizuri.",

"Hayo maneno uliyamaanisha?",

"Asilimia mia.",

Joy alifungua faili na kuweka karatasi ya meseji walioichapa kutoka kwenye simu ya Cecy. Reuben alitandaza karatasi mbele ya Leah.

"Hiyo ni namba yako ya simu?",

Leah aliisoma, "Yes.",

"Je, huo ujumbe uliuandika?",

"No.",

"Kuna mtu anashikaga simu yako?",

Leah alitikisa kichwa, "No.",

"So nani aliandika hiyo message na kuituma kwa Cecy?",

"I-I don't know.",

"Kama hiyo namba ya simu na yako na hakuna mtu anayeshika simu yako zaidi yako, ni nani ameandika hiyo message, Leah?", Reuben aliuliza kwa mkazo,

"Kama nilivyosema, I don't know.",

Mlango ulifunguliwa na askari aliingia akiwa amemshikilia mbaba kwa pingu. Mbaba alionekana kutojipenda. Nguo zake zilikuwa na madoa. Nywele, ndevu na kucha zake zilikuwa ndefu na chafu. Harufu yake ilikuwa ni mchanganyiko wa pombe na sigara.

"Leah, unamfahamu huyu mwanaume?", Reuben aliuliza,

"Hapana.", Leah alijibu huku akijitahidi asivute pumzi, maana harufu ilikuwa kali,

"Huyu ndiye aliyemgonga gari Cecy. Amekuja kujiwasilisha leo asubuhi baada ya ugomvi wenu.",

"What the fuck?", Leah alimuangalia yule mbaba, "Ugomvi gani? Unanijua?",

Yule mbaba aliangua kicheko kizito, "Wewe Leah unajifanya hunijui mimi? Ulinikuta maskani kwangu ukanishawishi nisababishe ajali ya Cecilia na kuniahidi milioni 15. Jana jioni nimekufata ukaniruka. Sasa hivi unajifanya hunijui?",

Leah alinyanyuka kwa hasira, "WHAT THE HECK ARE YOU TALKING ABOUT? SIKUFAHAMU! WHO THE FUCK ARE YOU? WHAT KIND OF GAME IS THIS?", Leah alifoka,

"Leah, kaa chini. Hasira haitakufikisha popote.", Reuben alisema.

Askari aliondoka na yule mwanaume. Leah alikaa chini taratibu, machozi yakimlengalenga. Kichwa kilimuuma na alihisi kutapika.

"Leah, siku zote ukweli humuweka mtu huru, hata kama ni mbaya.", alisema Reuben, "Sema ukweli.",

Leah hakutaka kuongea. Hakuona maana yoyote.

"Leah, ndoa yako na Paul ipoje?", Reuben aliuliza,

"Tayari unajua kila kitu. Stop asking me.", Leah aliongea kwa majonzi,

"Leah, kwanini baada ya Montana kutangaza vita haukuonesha ushirikiano na wenzio?',

Leah alivuta pumzi na kunyanyua uso wake, "Mimi na wale wanawake hatukuwahi kuzungumza hata siku moja. Miaka miwili iliyopita nilifanya sherehe nikawatumia mialiko lakini hawakuja. Janat na Suzanne walitamka kuwa mimi sio level yao so niache kuwaalika kwenye sherehe zangu za bajeti ndogo. Then Montana announced that ndio wakataka tujifanye marafiki ili tutatue tatizo. I'm not fake, detective.",

"Wanasema haukuwa na wasiwasi.",

"Ndiyo, sikuwa na wasiwasi. I had nothing to hide. Unajua ni kitu gani ambacho mpaka sasa hivi sielewei?",

"Kitu gani?",

"Mimi na Paul hatukuwahi kuzungumzia swala la talaka mpaka ule usiku, na ulikuwa usiku wa manane. And then asubuhi na mapema habari za ndoa yangu zilikuwa zimemfikia Montana. Alijuaje? Mpaka leo bado natafuta jibu.", Leah alitabasamu, "Detective, simfahamu huyu mwanaume aliyekuja humu na wala sijasababisha ajali ya Cecy. And to save your time, I also had nothing to do with kifo cha Montana or mama mwenye nyumba. But if you think nina hatia, nifungeni.",

Reuben alirudi kuegamia kiti chake.

Jioni, Leah alikuwa huru baada ya Reuben kukosa ushahidi uliokamilika. Babra alitoa pesa kwenye akaunti ya Leah na kuitumia kulipa dhamana. Leah alikuwa mnyonge sana, hata mwili wake haukuwa na nguvu. Babra alimfikisha vizuri nyumbani na kuhakikisha Leah ameingia ndani kisha aliondoka.

Leah alizitazama ngazi za sebuleni kwa uvivu. Miguu ilikuwa imechoka na hakuweza kuzipanda. Hivyo basi, alivua viatu vyake na kwenye kujirusha kwenye kochi. Aliangalia dari kwa muda mrefu bila kufikiri kitu chochote. Alipokuja kukamatwa hospitalini alikuwa na ufahamu kuwa watu walikuwa wakirekodi hivyo bila shaka kila mtu alijua habari zile. 

Je, ni nani yupo upande wake? Nani ataamini kuwa ile ilikuwa ni kosa na yeye hana hatia? Watu wanapenda kuamini kile wanachotaka hata kama wanajua hakina ukweli. Unyonge wake ulikuwa furaha ya wengi. Ni wapi alikosea?

Alipokuwa akijigeuza, rimoti ya TV ilianguka na betri ziliingia kwenye uvungu wa kochi. Ingawa alikuwa amechoka aliona ni bora aziokote yaishe. Leah alitoka kwenye kochi, akainama na kuingiza mkono uvunguni. Lakini betri zilikuwa mbali kidogo. Alichukua simu yake na kuwasha tochi kisha kumulika uvunguni. 

Ole!

Aliziona betri zote mbili, lakini pia aliona kitu kingine. Leah alivuta betri na pia kukifyatua kitu hicho kutoka chini ya kochi. Alikaa kitako na kukimulika vizuri kitu kile kwa tochi. Asalale! Ndipo alipogundua kuwa kilikuwa ni kifaa cha kurekodia sauti. Ilitengeneza gumzo kichwani mwake. 

Ni mtu mmoja tu aliyekuwa na uwezo wa kuingia ndani ya nyumba yake na kutegesha kifaa hicho. Moyo wake ulivunjika baada ya kupata jibu.

Babra hakujua kwanini bosi wake amempatia ofa ile kubwa. Walikuwa kwenye mgahawa wa bei ambao Babra alikuwa akitaka sana kuutembelea na kula chakula chake. Ni watu wakubwa tu walioweza kuimudu gharama; sura nyingi zilikuwa za kizungu. 

Babra alihisi labda wamekwenda pale kukutana na mtu mkubwa lakini dakika kumi na tano zilipita na ilikuwa ni yeye tu na Leah. Leah alikunywa mvinyo wake taratibu na Babra aliona bora aulize;

"Boss, kwanini tupo hapa?", aliuliza,

"Kwa ajili yako, mamy.", Leah alijibu kwa upole,

"Kuna kitu nimefanya kimekufurahisha?",

"No. Agiza chakula chochote unachotaka.",

Muhudumu alikuja na kuchukua oda zao. Babra aliitumia ofa ipasavyo. Wakisubiri chakula chao kiwe tayari, Leah aliona ni wakati muafaka;

"Hivi Babra, umefanya kazi na mimi kwa muda gani?", aliuliza,

"Miaka nane, boss.", Babra alijibu,

"Wow! At this point nahisi unajua kila kitu kuhusu mimi.",

"Sio kila kitu.",

"Anyway, mama yako anaendeleaje?',

"Anaendelea vizuri. Operation yake ilienda vizuri, asante sana kwa kugharamikia kila kitu.",

"Na mdogo wako je?",

"Ameingia form 5 mwezi wa sita.",

"Wow, amekuwa mkubwa.",

Babra alicheka kidogo, "Sana. Yote hayo ni kwa ajili ya msaada wako, boss.",

"Oh, it's nothing love. Nafurahi kuwa familia yako imesimama vizuri.", Leah alizungumza, "Katika miaka yetu nane ya kazi, nimeshawahi kufanya kitu ambacho kilikukwaza sana na ukashindwa kuniambia?",

"Ha-hapana.",

"Kweli?",

"Kweli.", Babra alianza kupata wasiwasi maana haikuwa kawaida ya Leah kuzungumza vile, "Wewe ni mtu mwema sana. Mimi ndiye nilikuwa nakosea ila ukawa unanirekebisha kwa upole.",

"Sasa kwanini umefanya hivi?",

"Unama-unamaanisha nini, boss?",

Leah alitoa kifaa cha kurekodia kutoka kwenye pochi yake na kukiweka mezani. Babra alishituka sana, nusura kinywaji kimpalie.

"Seeing the way ulivyoshtuka inaonesha ni wewe ndiye uliekitegesha hichi kidude chini ya kochi langu.", alitamka Leah bila kuonesha dalili yoyote ya hasira, "Kusema ukweli sitaki kujua ni kwanini ulikiweka or anything. Maumivu niliyonayo yanatosha. Nataka tu ufahamu Babra, kuwa nilikupenda sana na kukujali wewe na familia yako. Nilikuona kama mdogo wangu wa damu na nilikuamini.",

Babra alianza kulia, "Boss, naomba unisikilize _",

"Sijawaambia polisi kuhusu kitu chochote. Nimekuwekea pesa ya kutosha kwenye akaunti yako. Naamini itakusaidia kwa kipindi kirefu mpaka utakapopata kazi nyingine. Pia nimekuleta kwenye huu mgahawa unaoupenda kama njia yangu ya kukushukuru kwa miaka yote nane na kukuaga. You're fired, Babra.",

Leah aliondoka bila kugeuka nyuma maana angeweza kumuhurumia Babra. Babra aliumia sana moyo na alijutia jambo alilofanya. Kilichomuuma zaidi ni jinsi Leah alivyomuacha kwa upole pamoja na hasira zote alizokuwa nazo. Alijua kuwa hastahili msamaha, na alifahamu fika kuwa Leah hakustahili mateso aliyokuwa akiyapitia. Hakuweza kumlipa Leah wema wote aliomfanyia, lakini kuna kitu kimoja ambacho alijuwa kitalipa deni lake.

*** 

avataravatar
Next chapter