webnovel

CHAPTER 13

Ofisi ya Reuben ilikuwa ndani ya nyumba yake. Kulikuwa na chumba maalumu kwaajili ya kufanyia kazi zake. Chumba hicho kilikuwa na kila kitu, kuanzia computer, maabara ndogo, chumba cha uhifadhi ushahidi na vitabu vingi vilivyohusiana na upelelezi. Vingi viliandikwa kwa lugha ya kiingereza, lakini pia kulikuwa na vya lugha ya kifaransa, kijerumani na kichina.

Nyumba yake ilijengwa mbali na mji, hivyo ilikuwa na eneo kubwa sana. Ili kumuepushia Joy usumbufu wa safari kila asubuhi, Reuben alimuandalia chumba cha wageni.

Kwa mbali, Joy alihisi yupo nchi nyingine akiwa ndani ya nyumba ya Reuben. Alishangazwa na kila alichokiona; picha za ukutani, mimea ya ndani, na usanifu mzima wa nyumba ile. Reuben aliona jinsi Joy alivokuwa akipepesa macho kila sekunde. Alielewa sababu.

"Ukifanya kazi kwa bidii, one day utakuwa na nyumba kama hii.", Reuben alimwambia Joy,

"It's my dream. I'll work hard, no, harder, I'll work even harder.", Joy alitamka kwa shauku,

"Well, hard work itaanza na kucrack hii case. Ukimaliza kuweka vitu vyako chumbani, utanikuta ofisini.", Reuben alianza kuondoka, "Oh, ukija njoo na vikombe viwili vya kahawa. Hakuna kulala.",

"Yes detective.",

Saa moja baadae, ofisi ya Reuben ilikuwa kimya. Sauti pekee iliyosikika ilikuwa ni vidole vya Joy vikibonyeza kompyuta kwa spidi. Joy alikuwa mahili wa kompyuta. Ilikuwa ni sababu moja ya Reuben kumuajiri. Wote wakiwa bize kwenye kazi zao, Reuben aliingiwa na wazo;

"Joy.", aliita,

"Yes, detective.",

"Kati ya Suzy, Janat, Leah na Annabella, who do you think is guilty and why?",

"Janat. Because sasa hivi anakabiliwa na kesi juu ya aliyowapa saratani. Vithibitisho vikionesha kuwa bidhaa zake kweli zinahusika atapoteza kila kitu na kwenda jela.",

"So unasema Janat amemuua Montana ili wote wakose.",

"Yeah.",

Reuben alitikisa kichwa kama ishara ya kuelewa maelezo yake,

"Wewe je? Unahisi nani ana hatia?", Joy alimuuliza,

"Natakiwa niwahoji wote wanne. I'm sure tapata jibu baada ya hapo.",

Ghafla mlio wa kengele ulilia kutoka kwenye kompyuta ya Joy. Joy alibonyeza ujumbe ule ulioingia;

"Detective, njoo uone hii.", Joy aliongea kwa haraka,

Reuben alinyanyuka na kujongea meza ya Joy. Kwenye kioo cha kompyuta kulikuwa na tiketi ya ndege ya Annabella. Ilionesha kuwa imekatwa dakika 20 zilizopita kuelekea kisiwa cha Cyprus barani Ulaya. Pia tiketi ilionesha kwenda tu, hakukuwa na tarehe ya kurudi. Tarehe ya kuondoka ilikuwa ni siku ya pili yake.

"Annabella atakuwa wa kwanza kuhojiwa.", alisema Reuben, "Good job, Joy.",

"Thank you, detective.", Joy alitabasamu.

...

Asubuhi.

Cecilia alikuwa na wafungwa wenzie wakilima bustani. Alikuwa ni mwanamke mwenye uzuri wa asili ila maisha ya jela yalimchakaza sana. Kitu pekee kilichompatia matumaini ni ufahamu wa kuwa kifungo chake kilikuwa kikiisha wiki iliyofuata. Miaka ya usichana wake iliishia gerezani. Hakujua chochote zaidi ya shida lakini bado alibaki na mapenzi ya kweli kwa Paul kwa miaka yote hiyo kwani ndiye mtu pekee aliyebakia maishani mwake.

Askari mmoja alikaribia lile kundi.

"Cecy.", aliita,

Cecy alimgeukia, "Abee.",

"Una mgeni.",

Midomo ya Cecy ilitengeneza tabasamu. Aliingiwa na furaha akijua fika ni nani aliyekuja kumtembelea. Askari alimsindikiza mpaka kwenye chumba cha wageni na kumuacha aingie mwenyewe. Cecy alimshukuru na kufungua mlango. Alipigwa na mshangao wa milenia pale alipoingia ndani na kukutana uso kwa uso na mgeni wake.

Leah!

Leah hakuongea chochote huku akisubiri Cecy aketi, lakini Cecy hakutaka kukaa. Uwoga ulimfanya ashindwe kupiga hatua mbele. Alitamani askari afungue mlango ili aweze kukimbia, lakini kwa bahati mbaya alikuwa na dakika kumi za kukaa ndani ya kile chumba na mgeni wake. 

"Mbona umeganda mlangoni?", Leah alimuuliza, "Njoo ukae.",

"Umefata nini?", kwa sauti ya kutetemeka, Cecy aliuliza,

"Unaulizaga wageni wako wote hilo swali? Au upo comfortable kusimama?",

Cecy alisogelea kiti chake na kukaa. Alipepesa macho huku na kule kumkwepa Leah. Uwoga ulimpa udhaifu, na ndicho kitu Leah alichokuwa anataka kukiona kutoka kwake.

"Nilikuwa nimejiandaa kujitambulisha lakini umezihirisha kuwa tayari unanifahamu.", alisema Leah, 

"Umejuaje nipo _",

"Sikujua kama wewe ni mzuri hivi. Now I see why my husband likes you so much.",

"Mume wako?",

"Mbona unauliza kama hujui?",

"Paul aliniambia kuwa _",

"Amenipa talaka, sio? Kwa bahati mbaya nimegoma. Mimi na Paul hatujaachana. Bado sisi ni mume na mke, na itaendelea kuwa hivyo for a long time.",

Cecy alikasirika, "Kwanini hutaki kumuacha?",

"Kwa nini unataka nimuache?",

"Kwa sababu hakupendi na unajua.",

"Ukimaanisha kuwa anakupenda wewe, sio?",

"Ndiyo.",

"Wewe unampenda?",

"Ndiyo.",

"Utamzalia watoto wangapi?",

Cecy alisita kujibu. 

"Amekuahidi kuwa atakuoa? Una uhakika ndoa yako wewe itadumu?",

"Hujui chochote.", Cecy aliongea kwa kwikwi,

Leah alicheka, "Sijui chochote? Wewe ndio hujui chochote. Nikwambie kwanini Paul anataka kuniacha? It's not about love, girl, it's about his pride and ego.",

"Sio kweli.",

"Uliwekwa jela ukiwa na miaka 18 au 19, right? Kama sikosei Paul alikuwa ni boyfriend wako wa kwanza na wa mwisho. Hujui wanaume vizuri, Cecy. Ngoja nikwambie. You know me, unajua utajiri wangu. Unajua kuwa uchumi wangu umezidi wa Paul kwa asilimia kubwa sana, so he felt inferior.",

"Hauna uhakika _",

"Wanaume wanapenda kuwa juu, whether kiuchumi au kiakili, hawapendi kuwa chini ya mwanamke. Miaka mitano ya kwanza ya ndoa, Paul ndio alikuwa provider huku mimi nikihangaika kutafuta watu wakunitolea kitabu changu cha kwanza. Siku niliyotoa kitabu changu na kuwa maarufu, mbegu ya wivu na chuki ilipandwa kwenye moyo wa Paul. Kadiri miaka ilivyoenda na mimi kutajirika, his love for me completely shifted.",

"Paul hayupo hivyo!", Cecy aliendelea kubisha bila sababu ya msingi,

"Every man is like that, darling. Embu jiangalie; umekaa jela miaka 20, hauna kazi, hauna hata senti moja. Ukitoka hapa unamtegemea Paul kwa kila kitu hadi mambo ya ndani. That's what he wants. He wants you to worship him. He wants to feel superior. He wants to leave me because of that. You, darling, unamfanya ajione powerful. Utakuwa unamuomba kila kitu; ukitaka kusuka, kutengeneza kucha, kununua nguo, pochi, vibanio, everything, itabidi upitie kwake. What does he get in return? Unampa nguvu ya kufanya chochote anachotaka. Hautaweza kumuuliza swali akichelewa kurudi, au akirudi na harufu ya perfume ya kike, hautaweza kufungua mdomo wako kwasababu maisha yako ameyashikilia.", 

Akili ya Cecy ilianza kuchemka. Kidogo kidogo maneno ya Leah yalileta maana nyingine kabisa na kumfumbua macho. Alianza kujiona mjinga.

"Maybe anakupenda kweli.", Leah aliendelea, "Lakini haimaanishi hatokupelekesha. Love is transactional. I always advocate for women na ndio maana nipo hapa kukuonya. Tune your mind towards a different direction. Kitu pekee unachotakiwa kufikiria ukitoka jela wiki ijayo ni kupata kazi na kujitengenezea maisha yako ili mwanaume yoyote asije kukufanya zoba. I can help you, mwanamke kwa mwanamke mwenzie.",

"Hata maisha ni transactional. Najua kuna kitu unataka kutoka kwangu pia.",

Leah alitabasamu, "You're so smart. I like you already.",

***

Next chapter