webnovel

chapter 67

Wakati Bibi sumbo anaendelea kukata ukindu anahisi Hali ya hewa ikibadilika na nywele za kichwa chake zote kuamka na kusimama licha ya kuwa kichwa chake kilikuwa kimenyolewa.

Hali ya hatari anayohisi mtu yeyote pale anapopita sehemu yenye hatari ya vitu visivyoonekana kwa Hali ya kawaida.

Bibi sumbo anahisi damu ya mwili wake kuganda na wakati huo huo mapigo ya moyo wake kuongezea Kasi.Anavuta pumzi ndefu kujaribu kujiweka sawa.

Ingekuwa ni mtu mwingine angepuuzia kwa kusema amehisi jinamizi limepita au kwa aliyemuoga zaidi angetimua mbio na wazo la pili kilikuwa zuri zaidi kwa Bibi sumbo kwa wakati huo angekuwa na miguu inayompa hatua za uhakika lakini kwa umri wake anajikuta anatumia busara zaidi katika Hali tatanishi kama hii.

Kutokana na umri wake mrefu amepitia mengi na anajua mengi na Hali ya hewa iliyopita wakati huu sio nzuri kabisa ikiashiria kitu kilichopo maeneo hayo sio kizuri kabisa.

Kitu kichafu chenye harufu nzito na kilichojaa kiza Totoro ndani yake hakuna nuru kisicho Cha kibinadamu na hakitakiwi kabisa kuwa sehemu ya ulimwengu huu wa watu hai wanaotembea pasipo kujua kinacho wazunguka kwa macho ya nyama.

Anavuta pumzi tena na kuamua kujiweka sawa jambo ambalo anafanikiwa kwani ukijua Simba hali mzoga ukishindwa kujinasua kwake njia nyingine ni kujifanya umekufa na kujaribu bahati yako.

Ndicho alichokifanya Bibi sumbo anajifanya kama hajui kinachoendelea maeneo Yale na kuendelea na kazi zake asitake kuvuta umakini wa kitu kinachopita.

Lakini bahati haikuwa kwake kwani anaendelea kuhisi kiumbe hicho kikimsogelea na kujua Moja kwa Moja kuwa hiki kiumbe kilikuwa na shida na yeye na hata afanye nini hawezi kujiokoa kutokana na kitu kinachotaka kutoka kwake.

" Amna mtu atakayejua kama ulikuwa mzuri na wa thamani kwa Sababu umeoza na unanuka hufai kwa matumizi unatakiwa kwenda unakostaili" Maneno yake ya kejeli hayakukosea njia yalimfikia mhusika ipasavyo.

" unanizungumzia Mimi au?" anasikia sauti nyuma yake anasimama pole pole na kugeuka kumwangalia mtu aliyeko nyuma yake.

Baada ya kumuona mhusika anajua wazi kuwa maneno yake yalikuwa sahihi.

Mbele yake amesimama ..sio kusimama bali ni mwanaume anaye pepesuka kama Jani la mti linalo peperushwa na upepo mkali.

Ngozi yake ikiwa imepauka kuonyesha mwili wake usiokuwa na damu,mishipa yake ikiwa inajionyesha kwenye ngozi yake.

Macho yake yakionyesha kukosa uhai na mwili wake ukionekana kukosa nyama.Isingekuwa ngozi ya mwili wake Bibi sumbo anauhakika mifupa yake ingekuwa inaporomoka chini. kaniki yake ikionekana kubwa kuliko mwili.

Aliyesimama mbele yake ni Moja kati ya mizimu mitatu iliyoasi na kushika madara kwa kutumia watemi na watemi walio pita na mpaka wa Sasa.wasiokuwa na mpango wa kuondoka wakiwa na lengo la kutumia na watemi wanaokuja kuendeleza tamaa zao za kuwepo duniani.Zulimo.

Zulimo alikuwa katika msako wa kumtafuta mtoto wa utabiri anayewachanga vichwa kwa Sasa na baada ya mzunguko wa mda mrefu katika himaya ya mpuli pasipo mafanikio yeyote anaamua kurudi.

Wakati akiwa njiani anajikuta akiishiwa nguvu na mwili wake ukianza kukongoroka ukionyesha uhalisia wake wa mzimu.

Anakumbuka ametumia nguvu nyingi katika kusafisri kwa kupotea na kutokea sehemu nyingine hata akose uwezo wa kujirudisha kwenye pango lao kwani Kila alipojaribu kupote alijikuta mwili usikubali na hivyo kuishia kutembea kama binadamu.

Jua Kali la Saa sita likimpiga na mwili ukizidi kudhoofu.

" siamini kuwa napiga ng'ondi zulimo Mimi"

Analalamika akijiuliza mara yake ya mwisho kutembea ni lini." labda karne nyingi zilizopita nikiwa binadamu" anajijibu mwenyewe.

" ukizungumzia binadamu kwani Leo wako wapi mbona sioni hata mmoja?"

Kutokana na kupungua kwa nguvu zao Zulimo na wenzake wamekuwa wakitegemea nafsi za watu wakichukua uhai wao na kuongezea siku zao za kuishia mpaka pale watakapo pata kafara yenye nguvu ikiwa ni uhai wa mmilikiwa ardhi itakayo wasaidia kurudi katika Hali Yao ya awali.

Lakini nguvu za kumtafuta mmiliki zimekuwa zikigonga mwamba kwa miaka mingi na kufanya Hali Yao kuwa mbaya.

Zulimo anaendelea kutembea akiangalia huku na kule na hata kutumia pua zake kunusa kama atapata binadamu yeyote apate kuiba uhai wake.

" kwani binadamu wamehama au?" anajiuliza huku matusi yakimtoka mfululizo lakini hiyo yote haikusaidia ukilinganisha alikuwa porini na uwindaji umekuwa ni mdogo kutokana na kukosekana kwa wanyama na wanakijiji wakiwa bado Wana chakula Cha kutosha kutokana na chakula kilicholetwa siku tatu zilizopita na wawindaji.

Baada ya kama milele pua zake Zina nusa harufu ya binadamu.

" hatimaye!" anajisemea akianza kutembea akifuata harufu mtu angemuona angejua ni mbwa wa miguu miwili tena wa mawindo namna alivyokuwa ananusa kwa nguvu.

" kikongwe!" anang'aka baada ya kuona binadamu aliye fanikiwa kumpata kwani haikuwa hadhi yake na uhai wake sio mrefu wa kumpa maisha marefu.

Zulimo na wenzake hutumia uhai wa vijana kwani maisha yao bado ni marefu tofauti na wazee.

" Sio mda wa kuchagua chakula ukiwa na njaa" anaongea baada ya kuona mwili wake ukipepesuka.Anauhakika uhai wa mzee huyu utamsaidia kurudi nyumbani angalau.

Anapiga hatua kumsogekea lakini kabla hajafika anamsikia kikongwe huyo akimtukana asiamini masikio yake.

" Kwani Kuna mzoga mwingine hapa zaidi yako?" Bibi sumbo anauliza macho yake yakionyesha jeuri na kutokumuogopa mtu aliyeko mble yake.

" kweli unauthubutu kikongwe na umrii huo huogopi?" Zulimo bado haamini.

" Umewahi kumuona nani anauogopa mzoga zaidi ya kutema mate kwa harufu yake mbaya" Bibi sumbo hakurudi nyuma.

" unajua kwa ukikongwe wako huo una mdomo san...arghh" Zulimo anajaribu kuongea lakini anaishia kukohoa akipepesuka zaidi kuonyesha anavyozidi kuongea ndivyo nguvu zinavyomwishia.

" tss,ts" Bibi sumbo anatikisa ulimi wake kama anamwonea huruma." hembu jiulize kati yetu hapa ni nani kigongwe? Mimi ni kikongwe wa miguu mitatu lakini Nina jiweza na wewe ni kikongwe wa miguu miwili lakini hujiwezi"

" unaongea sana we bibi,situmiagi nafsi zilizozeeka lakini Leo itabidi nitumie yako hata kama inachefua" Anajibu Zulimo mboni ya jicho lake ikibadirika na kuwa nyekundu.

" unajua mwisho wenu unakaribia na utakuwa mwisho mbaya sana'"

" wewe kama nani kuamua mwisho wangu?" anaongea akimsogelea lakini Bibi sumbo hakupiga hatua kurudi nyuma.

" na kwa kuwa umenikera kwa mdomo wako nitakupatia unacho staili"

"utakufa kifo kibaya sana na utalipa kwa mambo yote uliyofanya" Bibi sumbo anamtemea mate usoni.

" tayari nimeshakufa kikongwe" anajifuta mate usoni na mkono wake unaenda kifuani kwa Bibi sumbo.

Maumivu makali yana mpata Bibi sumbo macho yakimtoka lakini mdomo wake usitoe sauti yeyote ya maumivu zaidi ya damu.

Mkono wa Zulimo ukiwa kifuani kwa Bibi sumbo sehemu ulipo moyo wake na kuushikilia ndani ya kifua chake.Macho yake yakiwa yamefumbwa na pua zake zikiwa zinavuta pumzi ndefu kama mtu aliyeko katikati ya bustani nzuri ya maua yenye harufu nzuri .Sura yake ikionyesha kuridhika na anachokipata.

Taratibu uhai wa Bibi sumbo unaanza kumtoka na haikumchukua mda mrefu mwili wake kulegea kuashiria mwisho wake.Mwili wake unakuwa mkavu na ngozi yake ikiganda kwenye mifupa kama alivyokuwa Zulimo hapo awali.

Taratibu ngozi ya Zulimo iliyo kuwa imepauka inaanza kupata nuru na macho yake yanarudisha uhai mwili wake uliokuwa umekongoroka unarudisha nyama na mwonekano wake unakuwa mzuri usiokuwa wa kutusha.

" Ingawa ulikuwaa na mdomo nafsi yako angalau inafaida kidogo,binadamu mpumbavu"

Anachomoa mkono wake kifuani kwa Bibi sumbo lakini haukutoka peke yake ukitoka na moyo wa bibi huyo damu ikichuruzika waliposimama na mwili wa mzee huyo kuanguka chini kwa kishindo kifua chake kikiwa kipo wazi kikitoa damu nyeusi inayoganda pindi tu inapoguswa na upepo.

" Hii itakuwa sawa mpaka nitakapo pata damu changa" anaongea akijiangalia mwili wake wenye mabadiliko uliorudi kama awali na wenye nguvu.

" Sasa tutaona ni nani atakayekuwa mzoga kati yetu" Zulimo anaongea akiondoka mkononi akiwa ameshikilia moyo wa Bibi sumbo.

" hata wakikupata watakuzika pasipo moyo wako.

Ghafla anapotea mahali pale na kubaki kama hakufika. chini ukibakia mwili wa Bibi sumbo ukiwa hauna uhai zaidi ya kuzungukwa na damu yake mwenye nyeusi iliyoganda pamoja na ukindu aliyokuwa anaupenda maisha yake yote.

Ni kifo gani kizuri kama kufa ukiwa sehemu uipendayo zaidi.

****usisahau comment yako msomaji****