webnovel

chapter 64.

Ukimwangalia mwanaume huyu ni lazima ujue mara Moja kuwa ni mzoefu wa kupigana au vita.Anaweka sime yake kiunoni kwenye mfuko wake anainama na kumsaidia yule mwanamke anayeendelea kutetemeka pale chini.Kumwangalia kwa haraka anajua ni kijakazi." unajua aliki mtoto mkubwa wa nyumba hii?" anauliza akiendelea kuangalia huku na kule asije akajeruhiwa wakati anaongea na mwanamke huyu.

" niambie tafadhali Nina haraka" anaongea tena baada ya kuona mwanamke huyu anatetemeka hawezi hata kunyanyua mdomo kwa mshtuko wa kuponea chupu kwenda kwa wazee." wa..watoto wote wa..waliondoka na walinzi na Nemela atakuwa kaondoka nao" hatimaye anamjibu.

" walielekea njia ipi?" anamuuliza tena na mwanamke anamwonyesha upande walikoelekea kwa kidole kabla ya kuongezea "njia ya pangoni"

" asante,na kimbia elekea huku Amna atakayekuona" anamwambia na kuondoka akikimbia.

Ndani ya pangoni Kuna mtoto wa miaka kama kumi na kuendelea akiwa amejikunja machozi yakimtoka,mwili ukitetemeka kwa woga.Anasikia mtu akitembea machozi yanazidi kumtoka akijua huu ndio mwisho wake.Anaingia yule mwanaume aliyejazia tofauti na awali mwiki wake ukiwa na majeraha kidogo kifuani na mkono wake ukivuja damu kutokana na jeraha la sime karibu na kiwiko chake lakini anaonekana Kama haoninmaumivu.Anaenda na kuinama karibu na yule mtoto " wewe ndio Nemela" anauliza kwa sauti ya utulivu asije akamtisha zaidi,mtoto anaitikia kwa kichwa kukubali na mwanaume anapumua kwa ahueni aliyoipata.

" usijali kuanzia hivi Sasa nitakulinda,Mimi ni mlinzi wako naitwa Makandelo" lakini mtoto hajibu kitu anazidi kutetemeka na kulia.Makandelo anamwangalia kuona kama Kuna jereha lolote anakosa anaona atakuwa anaogopa tu.

" tuondoke hapa sio salama" anaongea akimbeba lakini anasimama baada ya kusikia mtoto akiongea.

" Nsu..Nsumbu"

" nini?" anauliza akimwangalia usoni.

" mdogo wangu, Nsumbu,siwezi kuondoka bila yeye"

" inabidi tuondoke huna mda wa kusubiri,kwani ulimwacha wapi?" anauliza Makandelo akiona mtoto anampotezea mda.

" nilimficha" Nemela anaongea akimwangalia Makandelo jicho la msaada kwa mdogo wake.

Makandelo anarudi kwenye pango akiwa ameumia zaidi kuliko awali lakini anapofika mwili wake unakosa nguvu na kuangukia magoti machozi yakimlenga baada ya kumuona Nemela akiwa ameegemea ukuta wa pango macho yakiwa yamemtoka na kifuani kwake sehemu ya moyo pakiwa wazi mwili ukimtapakaa damu na zingine chini.Makandelo anapiga makelele ya uchungu na hasira yaliyochanganyika na kujilaumu.Makelele yanatoa mwangwi katika pango hili likisababisha popo na bundi waliofanya makazi humu kutimuka mbio wakiongeza mtisho wa kilio Cha Makandelo.

Makandelo akiwa ameshikilia mwili wa kijana wa miaka kama ishiri hivi uliokuwa unaning'inia katika mti baada ya kujinyonga.Uso wake ukiwa sio wa kijana mdogo tena.Kwa Sasa ni mwanaume wa miaka thelathini au zaidi,kovu lake likimkaa vizuri zaidi usoni kwake badala ya kumchukiza misuli yake ikituna zaidi.Kilichobadilika ni macho yake yanayoonekana kukosa hisia zingine zozote isipokuwa hasira ya kisasi.

Akiwa amesimama karibu na kaburi Moshi mweusi unatokea nyuma yake anageuka na kabla hajakaa vizuri kitu chenye ncha Kali kinatua tumboni kwake.Zinge anashtuka usingizini mwili wote ukiwa umelowa jasho pembeni yake akiwa amekaa mke wake ambaye ndiye aliyemwamsha baada ya kuamka na kumuona akihangaika usingizini.

" ni ndoto mbaya tena?" mkewe anauliza akimshika bega kama kumtuliza na Zinge anaitikia kwa kichwa kukubali.Akijiuliza ni kwa nini ndoto hizi zinamwijia Kila siku.Mwanzoni ilikuwa ni vipande vifupi vifupi vya mauaji ya kutisha asiweze kuunganisha lakini Sasa vimekuwa virefu kidogo kuweza kuunda tukio

."acha kuwa mbishi tumwambie baba akupeleke kwa mganga tena,hii inanitia wasiwasi Zinge maana hulali kabisa siku hizi" Ntali mke wake anaeleza wasiwasi wake.

" naweza kumudu,nisamehe kukuamsha tena.Lala" anamsaidia kurudi kitandani anamfunika kaniki vizuri na yeye kulala.

" we mbishi sana Zinge" mke wake anaongea akipiga mwayo.

" Nikishindwa kuvumilia tutamwambia usijali kabisa" anamhakikishia.Baada ya mda anasikia pumzi za Ntali zikiwa za utulivu na kujua amelala.

" hizi ni ndoto tu au ni zaidi ya anavyofikiria" anawaza macho yake yakiwa kwenye dari kwani haiwezekani kurudia ndoto hizohizo Tangu akiwa mtoto na zisingefungwa kwa dawa zingekuwa zinamsumbua siku zote.

"Ndoto nyingi ni matokeo ya maisha yetu,na tunazigawa mara tatu. kwanza zinakuja kutokana na mambo ambayo tumeshayafanya mchana ambayo mara nyingi zinakuwa hazina maana au Zinakuwa zimejaa majuto na furaha au kuwindwa na matukio mabaya au mazuri tuliyofanya na kuganda kichwani kwetu na moyoni hivyo kufanya kwenda kuyatembelea na kuyaishi Kila tunapolala,

pili maisha yetu tuliyo ishi nyuma kabla hatujafa na kuzaliwa tena"

" hiyo inawekana?"

" hakuna kisichowezekana katika Dunia hii Nshana,na kama nilivyokuwa ninasema maisha yetu hayo ya nyuma yanakuwa hayaja katwa kabisa na hivyo kusababisha kumbukumbu hizo kuingiliana na maisha yako mapya katika Hali ya ndoto na huwa ni vigumu sana kupata ndoto hizi.

tatu maisha yetu yajayo au kuleta maono kama utabiri,hizi ni ndoto ambazo tumezizoea tunaota na mambo hayo kutoka kweli.mmhh! na kwa mtoto wako Nshana sijui anaota maisha yake yajayo au yaliyopita ni mda tu ndio unaweza kuamua hilo.Siwezi kuzitoa kabisa kwani ni sehemu ya ubongo wake ninachofanya ni kuzifunga zisimjie kwa mda na bindi ukuta ukiwa mdogo au ukianguka kabisa ataanza kuota tena.Na kama mtakuwa hamjapata maana yake mrudisheni tena nije nimfunnge tena."

Zinge anakumbuka mazungumzo ya mganga na baba yake kipindi yupo mdogo.Mazungumzo waliodhani hakuyasikia kwa kuwa alikuwa amelala pasipokujua kuwa alikuwa macho.Anaamua kuvumilia kidogo apate kujua maana ya ndoto hizi na kama ikimshinda atamwambia baba yake amrudishe kwa mganga zikafungwe tena.Kitendo Cha kutokulala usiku au usingizi wa mang'amu ng'amu vinamfanya aamke amechoka kama alibeba Kijiji kizima mabegani mwake.

" ni maisha ya mbele au nyuma?" anajiuliza kwani huyo Makandelo anayemuona kwenye ndoto hafanani kabisa na yeye anajiuliza kama ni yeye mwenyewe katika mwili tofauti? asijue kama atakuwa hivyo huko mbeleni au alikuwa hivyo huko nyuma.

Ni asubuhi nyingine tena katika Kijiji Cha Ntungu na himaya ya Mpuli.Kama ilivyokawaida ndege wa asubuhi wameshaamka na shangwe zao wakiomba na kuruka na ukiwauliza wanachofurahia watakwambia ni kuliona jua tu wapate kuruka tawi hili na kwenda tawi lingine kwa uhuru kwani wamebarikiwa kutokuwa na wasiwasi duniani.

Wanawake wanaopenda kuamka na ndege tayari wako kwenye shughuli zao za asubuhi wakiutilia maanani usemi wa ndege anayewahi kuamka hunywa maji masafi.

Tulya akiwa ni miongoni mwao kwa Sasa akiwa amemaliza kumkanda mama mkwe wake mgongo kutokana na kuangukia jana usiku " unatakiwa kuwa makini mama na Leo usitoke kitandani kabisa" anaongea Tulya akibeba kipeo chake kilicho na maji pamoja na tambara.

" usijali mwanangu kaendelee na kazi sijavunja shingo" anajibu Bibi sumbo akijaribisha kukaa vizuri aone kama mgongo wake utakubali.

" nimeshajua Nzagamba karithi wapi ubishi" Tulya anaongea kwa sauti ya chini mama mkwe wake asisike lakini kumbe amemsikia.

" we hujakutana na Mzee Kizinga,ndio utajua kati yangu Mimi na yeye Nzagamba karithi kwa nani" Anacheka kidogo Bibi sumbo akirejea kumbukumbu za mumewe.

" basi mliendana" Tulya anamjibu safari hii kwa sauti kubwa

" anagalia nani anaongea,nyie hamjioni?"

" Mimi sio mbishi na nza.." Tulya anakatishwa na Nzagamba aliyeingia chumbani kumjulia mama yake Hali.

" anaendeleaje?" anauliza akisimama na kuegemeza ukuta macho yake yakitua kwa Tulya anayeinamisha kichwa chini kwa aibu baada ya kumbukumbu za kilichotokea Jana usiku kupita kichwani kwake kabla hayajaenda kwa mama yake.

" Niko sawa twendeni tukale kifungua kinywa" anaitikia Bibi sumbo akisimama.

" unamwona" Tulya anamjibu akitoka nje kwenda kuandaa kifungua kinywa.

Mchana Tulya akiwa ameondoka kwenda kumaliza sherehe za harusi kwa Sinde Nzagamba anaingia ndani asimuone mama yake.

" kaenda wapi tena?" anajiuliza akitoka nje na kuzunguka nyuma ya nyumba kumwangalia asimuone.Kutokana na kukosa usingizi Jana usiku Nzagamba alijiegesha na usingizi ukampitia Sasa anaamka asimuone mama yake."anapenda kuzurura huyu" anaongea akianza kutembea kuelekea mtoni kuoga,akiwa njiani anahisi mtu akimfuatilia.

Tangu Nzagamba arudi kuwinda anashangaa Masikio yake yamekuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kusikia na hisia zake zimekuwa za juu zaidi.Mtu huyu asiyemuona amekuwa akihisi hisia za uwepo wake zaidi kuliko awali,hata Jana usiku alipokuwa amelala nje alihisi uwepo wake kana kwamba mtu huyu alikaa pale kitandani. Taratibu anashika sime yake akiendelea kuhesabu hatua za mtu huyu anayemfuatilia nyuma yake kwa makadirio ya hatua kama tatu na mara nyingine nne,urefu wake anaweza kufika kwenye bega lake.

Nzagamba anaongezea Kasi ya hatua zake na mtu huyo anaongezea Kisha anasimama ghafla anageuka na kumshika shingo kama makadirio yake yalivyokuwa anapatia na ghafla anasikia sauti ya mshtuko kabla ya mtu kujitokeza mbele yake ni kijana mfupi na kavalia kaniki ya rangi ya kijivu.Pasipo kushangaa anamwekea sime yake shingoni

" we ni nani na kwa nini unanifuatilia?"

Wakati Mnelela maisha yake yakiwa kwenye mikono ya Nzagamba katikati ya Kijiji Kuna mkusanyiko wa watu na Tulya akiwa amesimama uso kwa uso na Dunila.Na katika njia ya kutoka upande wa pili wa mto anakuja kijana akiwa anakimbia kuelekea Kijijini mapigo ya moyo wake yakiwa juu na hiyo ni baada ya kukutana na Bibi sumbo lakini akiwa maiti na mwili wake ukiwa umeraruliwa vibaya sana.Siku inaweza kuwa nzuri zaidi?