webnovel

chapter 50

Nzagamba anaendelea kucheza na ziwa lake,anatawanya miguu yake na kukaa katikati yake anakutanisha maumbile yake ambayo kwa sasa yalikuwa yanaandamana kwa uhuru wao.Anaanza kuyachezesha kwenye maumbile ya Tulya akijisugua huku akimwonyesha ni jinsi gani uwepo wake ulivyo na madhara makubwa kwake. Mguno wa kuridhika unamtoka kinywani kwake.Kwa upande wa Tulya mwili unamsisimka kuliko kawaida baada ya kuhisi raha ya ajabu katikati ya mapaja yake na anajikuta akinyanyua kiuno chake juu kusogea karibu na raha hiyo.

Nzagamba anachanganyikiwa zaidi baada ya Tulya kuanza kuchezesha kiuno chake na akiweka sawa maumbile yake kwa kuzungusha kiuno chake na kujikuta akitaka vingi zaidi anachotamani ni kuchana hizo kaniki yake amwache wazi amalizane naye nyama kwa nyama kwani anaona hicho kipande Cha nguo kilichopo kati yao ni kama ukuta na kinamkera kuliko maelezo lakini anajikumbusha kuwa huu sio wakati wake anachohitaji ni kuonja tu kwa siku ya Leo.

Anashusha kitambaa alichofunga Tulya kifuani kwake na uzuri ni kuwa Tulya hakukifunga kwa kupitia shingoni kwani kilikuwa kinazunguka kifua chake mpaka mgongoni tu.Nzagamba anakishusha chini na kuachia saa sita yake yote nje.macho yake yanaangalia kile kilichopo Mbele yake asiamini maana ni kizuri kuliko maelezo,maziwa ya Tulya yakiwa na ngozi laini kabisa chuchu zake zikiwa ngumu na kukaa vizuri,mwanamke wa aina gani huyu anajiuliza Nzagamba." aahh!" mguno unamtoka Tulya ambaye alikuwa amefumba macho akisikilizia raha aliyokuwa akiiisikia ikitoka chini ya tumbo lake kutokana na kucheza na maumbile ya Nzagamba asijue kama kifua chake Kiko wazi kwa sasa mpaka alipo hisi kitu Cha maji maji kikipita kwenye chuchu yake.

Anafumbua macho yake nakuona mdomo wa Nzagamba ukinyonya chuchu yake kama mtoto mwenye njaa ambaye katishiwa kuachishwa ziwa na mama yake nakuamua kunyonya kwa mara ya mwisho asiamini kama atapata bahati nyingine tena mkono wake mwingine ukichezea ziwa lake la pili.Macho Yao yanakutana Kila mtu akiendelea kuhema akijitahidi kupata pumzi Ili kuendelea kuwepo hapa duniani.

" aaah Nzagamba"

Tulya anaachia mguno baada ya Nzagamba kukandamiza maumbile yake zaidi huku akiachia chuchu ya ziwa lake lingine na kuchukua la pili na kulitia mdomoni akiling'ata kidogo kabla ya kuendelea kulinyonya kama kupunguza maumivu.

Tulya anafumba macho yake akinyanyua miguu yake na kuizungusha kiunoni kwa Nzagamba nakuanza kuchezesha kiuno chake.

Akili yake ikirudi nakuamua kutokumuacha Nzagamba awe mshindi na yeye atamuonyesha alichofundwa unyagoni,anaendelea kuchezesha kiuno chake mikono yake ikienda kifuani kwa Nzagamba nakuanza kumpapasa anamsikia Nzagamba akiachia mguno kama Simba aliyepata nyama baada ya mawindo magumu.Haikuwachukuwa mda mrefu wote kufika kileleni akitangulia Tulya ambako haikumchukua mda mrefu Nzagamba naye kumwaga kwenye nguo yake ya ngozi aliyovaa ndani kuficha kitu chake kinachomfanya aitwe Nzagamba kisionekane ovyo.

Wote wanabaki walipo wakihema kwa mda na taratibu akili zao zinaanza kurudi.Nzagamba anafumbua macho yake nakumwangalia Tulya anayeendelea kuhema huku amefumba macho yake mwili wake ukimsukuma kuendelea zaidi lakini anaamua kutosheka kwa sasa anauhakika akirudi nyumbani atapata zaidi,ananyanyuka taratibu mkono wake unaenda kushika kitambaa alichokishusha chini nakuanza kukirudisha kuficha maziwa yake asije mtu mwingine akaona Mali yake.Tulya ananyanyuka harakaharaka baada ya kuhisi mikono ya Nzagamba kifuani kwake anasogea kidogo na kugeukia upande mwingine akianza kutengeneza kitambaa chake aking'ata mdomo wake na macho yake akiyafumba kwa aibu,atamwangaliaje? anajiuliza kwani haelewi imekuwaje kufarijiana kumeishia huku tena hadharani,atakuwa kachanganyikiwa.

Nzagamba anamwangalia anaamka nakusimama mkono wake ukienda kichwani kwake kuvuruga nywele zake mwili wake ukiwa bado unavuja jasho kutokana na kazi aliyoifanya Sasa hivi.Anageuka na kumwangalia Tulya aliyemaliza kutengeneza nguo yake lakini bado akiwa amekaa pale chini amejikunyata asigeuke kumwangalia.

" nenda nyumbani" anamsikia Nzagamba akimwambia anageuka na kunyanyua sura yake kumwangalia macho Yao yanakutana na mapigo yake ya moyo yanakata baada ya kuona Nzagamba akimwangalia kwa hasira.Anasimama haraka haraka akijitengeneza nguo zake vizuri.Anataka kuongea kitu lakini Nzagamba anageuka na kumpatia mgongo.Tulya anainama na kubeba vyombo vyake nakuanza kuondoka pasipo kusema chochote.Nzagamba anageuka na kumwangalia Tulya akiondoka baada ya kupotea anapiga mti ngumi kwa hasira asielewe ni nini kimetokea.

Kwa macho yake anahisi kama Tulya hakumpenda kilichotokea baina Yao baada ya kuamka na kusogea mbali nae asimwache hata amguse huku akimpatia mgongo.alielewa alama vibaya au? anajiuliza kwani kwake yeye anajua Tulya alipenda alipombusu na kuendelea hakupinga na inavyooneka alikuwa anafurahia kwani alikuwa anatoa ushirikiano, nini kimetokea? anaendelea kujiuliza huku akijilaumu kwa kushindwa kujidhibiti lakini siyo makosa yake mwanamke huyu anamfanya akose udhibiti kabisa na Leo ndio kati ya zile siku ambako kamba zake zote zimekata.Baada ya malumbano ya muda na akili yake anaamua kwenda kuoga mtoni kabla hajarudi na kuendelea na mazoezi na akirudi nyumbani ataongea na Tulya kuhusu kilichotokea ajue shida Iko wapi.Anaelekea upande wa mto kuoga.

" huna aibu si ndio?" sauti inaongelea sikioni kwa Mnelela aliyekuwa juu ya mti mda wote huu anashtuka na kugeuka nyuma anakutana na mschana kama umri wa miaka kumi na nane hivi lakini katika kumwangalia vizuri anagundua ndio yule mwanamke aliyemuona siku kadhaa zilizopita.

" wewe tena?" anamuuliza asijue kwa nini huyu mwanamke anapenda kumfuatilia na imekuwaje Leo anaonekana mtoto.

" mkuu wako akijua unachokifanya sidhani kama atafurahi" anaongea akijiweka vizuri kwenye tawi.

" nimefanya nini?" anauliza Mnelela akijifanya haelewi mwenzake anazungumzia nini.

" kwani we nani,siku ile ulisema utanitajia jina lakini hukusema ukakimbia"

" ukiendelea na uroho wa kutaka kuona Kila kitu ipo siku utapofuka" anaongea mwanamke nakupotea alipokuwa.

" kakimbia tena!" anaongea Mnelela akiangalia huku na kule asimuone.

" kwani wenyewe hawaoni nyumba mpaka waje kufanya mambo yao hadharani?" anajiuliza Mnelela kwani walimshtukiza hakujua mambo yangefikia huko.

Tulya anafika nyumbani na kujitupa kitandani akili yake ikirudia kilichotokea asiamini kafanya mambo kama hayo hadharani hata kama alikuwa anahitaji kiasi gani.

" nitakuwa nilichanganyikiwa!" anaongea akijivuta nywele zake Kila mara mwili ukikumbuka kilichotokea unasisimuka na mkono wake unaenda mdomoni kushika lipsi zake.

" nenda nyumbani" anakumbuka sauti ya Nzagamba iliyokuwa imejaa ubaridi.

Atakuwa amejutia au?sikuanzisha Mimi yeye ndio alianza kunibusu imekuwaje akasirike tena.

Taratibu hasira zinaanza kumpanda yeye ni mke wake inakuwa anampatia mgongo baada ya kilichotokea kati yao, huyu mwanaume anapima uvumilivu wake. kwa nini Kila akihisi mambo yanaenda vizuri anajikuta wamerudi nyuma kilichotokea mchana Leo ilikuwa ni hatua kubwa sana kwao lakini mwanaume ameweka sura ya majuto baada kumaliza haja zake.machozi yanamdondoka Tulya,afanye nini Ili Nzagamba amuelewe au baada ya yalioyotokea hajaridhika nae,hajamuona mwanamke kamili wa kuwa nae? anajiuliza.

Baada ya Nzagamba kurudi kuoga anawakuta marafiki zake wamevamia makazi yake wanafanya mazoezi.

" umekuwa hapa kwa mda gani mpaka ukaoge" anaongea Kilinge akiendelea kupiga mishale lakini Nzagamba hakuwajibu chochote anachukua upinde wake nakuanza kulenga mishale.sasa hivi Hali yake imekuwa mbaya kuliko awali kwani alitaka kuwa peke yake Ili achezeshe akili yake lakini Hawa chiriku hawatamuacha mzima.

Na kwa ukimya wake wengine wenye akili walielewa kuwa Nzagamba hakuwa kwenye hali ya kuongea,wote wakidhani ni kutokana na kwenda kuwinda wasijue kuwa hilo haliko hata akilini mwake kwa sasa.Lakini Mkita kama Mkita anahama kabisa na sehemu alikokuwa analengea mishale yake na kwenda kusimama karibu na Nzagamba akiongea na sauti yake ikifika kama mlio wa mbu msumbufu masikioni mwa Nzagamba na angekuwa mbu anauhakika angeshampa bao la kumtumbua kabisa.

Baada ya kupigizana kelele na Mkita au kupigiwa kelele tuseme maana yeye hakutia neno Giza linaingia, na hatimaye kurudi nyumbani anakokaribishwa na kimya kikubwa zaidi ya mwanga wa kibatari sebuleni.Anavuta pumzi ndefu na kutoka baada ya kuona ngozi yake ya kulalia ikiwa imetandikwa palepale pa siku zote.Alijua Leo mambo yatakuwa tofauti lakini hapana.Anaenda na kuchungulia chumbani na kumuona Tulya akiwa amelala au tuseme kujifanya kulala.

" atalalaje baada ya kilichotokea?" anajiuliza akienda kuzima taa na kujitupa kwenye ngozi yake.

Asubuhi inafika Tulya anaamka mapema na kumwangalia viazi akiweka kwenye mfuko wakati anatoka anamuona Nzagamba akiwa tayari ameshajiweka tayari kwa kuondoka mishale na upinde begani kwake,kiunoni akiwa na sime yake,akihangaika kufunga kamba za kitambaa Cha ngozi mkononi mwake,Tulya anaweka mfuko chini na kwenda kumsaidia Nzagamba anamwangalia tu.Baada ya kumaliza anapiga hatua kurudi nyuma akimwangalia mume wake aliyependeza akienda vitani anawaza halafu anajishtukia nani anawazaga namna hiyo kumwambia mumewe kapendeza akienda kufa anawaza.

"naondoka mama" anamuaga mama yake aliyesimama mlangoni akimwangalia akijikaza asilie kwani anajua mwanae akirudi atavunjika moyo tena.

" kuwa makini" anamjibu Bibi sumbo

"usijali"

anachukua mkuki wake anaanza kuondoka na Tulya anamsindikiza nyuma.Baada ya kufika mbali kidogo na nyumbani anaamua kuweka hasira zake pembeni kwani hajui ni lini atamuona tena mume wake na hataki kutia mikosi kwa ugomvi wao wa kitandani.

" Mimi naishia hapa" anaongea Tulya akimpatia mfuko wenye chakula na kibuyu Cha maji.

" kitakusaidia njiani"

" ilikuwa Haina ulazima" anamjibu akipokea Tulya anatulia kwa mda.

" safari njema"

" asante,kuwa makini mpaka nitakaporudi mwangalie mama" anaongea akimwangalia akitamani apate lile tabasamu la kumpatia nguvu safarini lakini hakulipata Tulya anaendelea kuangalia chini akijishauri afanye anachotaka kufanya au aache akihofia asije akakasirika tena.

" nenda nyumbani" Nzagamba anamwambia akitaka kuondoka lakini Tulya anamshtukiza kwa kumkumbatia.

" sijali kama utakuja na nyama au la,ninachokihitaji ni wewe urudi salama tu,niambie utarudi kwangu?" anamuuliza machozi yakimtoka na kuloanisha kifua Cha Nzagamba.

mwanamke anapenda kulia huyu na alivyo na machozi mengi,anawaza Nzagamba.

" niaangalie" anamwambia akishika kidevu na kunyanyua uso wake,Tulya anamwangalia akifuta machozi yake.

" nitarudi salama,na nikirudi Kuna kitu nataka nikwambie kwa hiyo subiri mpaka nitakaporejea sawa?" anamuuliza macho Yao yakitazamana na Tulya anaitikia kwa kichwa kukubaliana nae.Nzagamba anamkumbatia na kumwachia baada ya kumfuta machozi anaanza kuondoka akimwacha Tulya akimwangalia mgongo wake.