webnovel

chapter 40

Asubuhi inafika Tulya anaamka akipiga miayo macho yake yakiwa yamechoka kwani sio Nzagamba pekee aliyekesha Leo hata yeye pia amekesha,kwani usingizi uliamua kwenda likizo.Anaangalia sebuleni hamuoni Nzagamba anayejua wazi hajalala ndani.Usiku alimsikia akifungua mlango na kutoka na baada ya muda mrefu alivyoona harudi aliamua kutoka nje kumwangalia ndipo alipomuona amelala kwenye kitanda nje.Macho yake yanaenda kwenye eneo waliloanguka Jana na Kila kitu kilichotokea kinajirudia na kufanya mwili usisimke mkono wake unaenda kifuani nakuhisi mapigo yake ya moyo yanavyoenda mbio.Alikuwa anamkimbia asahau kilichotokea mtoni na Sasa kilichotokea Jana mambo yamekuwa mabaya zaidi.Atamwangaliaje? Lakini sio Mimi niliyefanya hivyo yeye ndio aliyenishika kwa nini nikimbie Sasa hivi zamu yake kuona aibu Anajisemea Tulya akitabasamu na kutamani kumuona Nzagamba akimkimbia kwa aibu.

Baada ya kufikia hitimisho la mkutano na halmashauri yake ya kichwa anatoka nje na kuchukua kibuyu chake kilichokuwa kimepachikwa kwenye fensi na kuondoka zake mtoni kuchota maji na akiwa tayari kwa majukumu yake ya siku.

Baada ya kumaliza kuchota maji wanapata kifungua kinywa yeye na Bibi sumbo ikiwa Nzagamba haonekani kabisa.Anamaliza kifungua kinywa na kuelekea uwani na hivi Sasa akiwa amesimama akiangalia udongo wake ulikauka pale chini tangu autelekeze.

" samahani sana siku ile nilikuwa nimevurugwa sana la sivyo nisingewaacha katika Hali hii" anaongea akichota maji kwenye kipeo na kuumwagia baada ya kuona ameweka maji ya kutosha anakaa chini nakuanza kuukanda akiuchanganya Ili ulainike vizuri.

"mamaaa!" anashtuka Tulya baada ya kugeuka na kumuona Nzagamba akimwangalia pasipo kusema chochote.Nzagamba aliyefika nyumbani mda sio mrefu alisikia sauti nzuri ikiimba uwaani anaamua Kuja na kumuona Tulya akiwa anatengeneza chungu huku akiiimba umakini wake wote ukiwa kwenye chungu akikigeuza na kukitengeneza sehemu ambako hakijakaa vizuri mara kwa mara.Macho yake makubwa yakipepesa Kila baada ya sekunde anaendelea kumwangalia mpaka alipokuwa anataka kugeuka ndipo alipomuona na kupiga makelele.

" umenshtua" anaongea akipeleka mkono wake usoni kama kufuta jasho na pasipo kujua anajipaka udongo karibu na nyusi zake.akiongezea alama za udongo ambazo tayari zilikuwa zimetapakaa usoni pake na kumfanya Nzagamba atake kucheka namna anavyoonekana kama katoka kuchimbiwa.

" unashtuka nini?"anauliza pasipo kufanya juhudi ya kumwambia ajifute au kumfuta maana hataki kumsogelea akihofia ya jana kujirudia.Tulya anafungua mdomo wake aseme kitu lakini anaufumba tena.

"Naelekea mtoni" anamuaga na kutegemea Tulya aseme kitu lakini anabaki akimwangalia tu.Baada ya kuona hasemi kitu anageuka na kuondoka.Tulya anabaki akimwangalia mgongo wake akiondoka." yupo kawaida" anaongea Tulya baada ya kuona Nzagamba Yuko sawa kama siku zote.Laiti angejua ni jinsi gani mwenzake alikuwa anajikaza kuonekana kawaida.

Mchana Tulya anaoga vizuri nakuvaa nguo nzuri na mpango wake madhubuti wa kumtega Nzagamba ukiwa pale pale.Anatikisa kifua chake kidogo kuhakikisha kuwa maziwa yake yanatikisa." hapa sawa" anajisemea na kutoka sebuleni anabeba kikapu chake na kuelekea mtoni kumpelekea Nzagamba chakula.Njiani mapigo yake ya moyo yakilipuka Kila mara akikumbuka lengo lake na vile vile akiwaza kama akimkuta na Lindiwe tena itakuwaje.

Anafika mtoni na kumuona Nzagamba akiwa amelala juu ya jiwe mkono wake Mmoja ukiwa umefunika macho yake na kama amemsikia vile anatoa mkono wake na kumwangalia.

" nimekuletea chakula" anaongea Tulya meno yake yote nje akijaribu kuwa sawa kama siku zote pasipokujua kuwa anazidisha kwani Nzagamba anaona kuwa mwendo wake umebadilika. kwani alikuwa anajitahidi kutembea kwa nguvu Ili maziwa yake yatikisike asijue anatembea kama ardhi inang'ang'ania nyayo zake.

Nzagamba anamwangalia tu akijiuliza atakuwa na matatizo gani safari hii maana anatembea kama anakuja kumvamia.

" weka hapo nitakula baadae" Tulya anajisikia vibaya kwani yeye alitaka amtengee akae amsubiri amalize kula ndio aondoke.Anamwangalia Nzagamba aliyerudi na kuendelea kulala kama awali akijifanya kama hamuoni mwenzake,maisha gani haya ya mke na mume anajiuliza Tulya kitu kizito kinamka kooni hasira za juzi zikianza kurudi na machozi yakianza kumlenga.

" Samahani kwa kilichotokea juzi,sikumaanisha kukupandishia sauti" anaongea kutaka kurudisha Hali kawaida maana inavyooneka Nzagamba bado amekasirika kama Jana alilala uwaani atajuaje kama leo akilalia mtaa wa tatu.Anawaza akihisi labda atakuwa anajisikia vibaya baada ya kumshika vile jana,kwani yeye ni mbaya kiasi hicho hata kilichotokea jana hakijamsogeza karibu yake.

Nzagamba anafumbua macho yake na kumwangalia anaona macho ya Tulya yakilenga machozi midomo yake ikitikisika kwa kujizuia kulia.

" nilijua yameisha,kweli anajua kuweka fundo" anajisemea Nzagamba na kabla Nzagamba hajajibu kitu Tulya anaendelea.

" Nikuombe tu kitu kimoja,tafadhali usifanye kitu kitakachodhalilisha ndoa yetu" anaongea Tulya anageuka na kutaka kuondoka lakini Nzagamba anamshika mkono. Tulya anasimama na kugeuka, Nzagamba anasimama pale alipo na kumsogelea karibu alipo pasipo kumwachia mkono.

" unataka kula nyama?" anamuuliza na kumfanya Tulya amshangae kwa hiyo nilichokiongea yeye ndio kaja na nyama.

" naweza kuwasha moto tukachoma ndege tukala wote" Tulya anamwangalia nabaada ya muda anakubali kwa kichwa akifuta machozi yake.

" Kaa hapo nakuja" Nzagamba anamsaidia kukaa kwenye jiwe na yeye kuondoka na baada ya muda anarudi akiwa na Kuni,anawasha moto na kuchukua ndege ambao alishawinda nakuanza kuchoma.

" chukua" anampatia aliyetayari Tulya anachukua nakuanza kula akipuliza.

" Amna kitu kinachoendelea kati yangu na Lindiwe,ulinielewa vibaya tu,sina mazoea naye zaidi ya salamu na siku ile tulikuwa tunasalimiana tu na wewe ukatukuta hapo"

Tulya anamwangalia kama hakutarajia kusikia akijieleza.

" Najua" anaongea Tulya akiangalia nyama ya ndege aliyoshika mkononi.Sio kama alikuwa hamwamini Nzagamba na alikuwa anajua Amna kitakachotokea kati yao lakini yeye kujua kuwa hapendwi kunamfanya kuwa katika ulinzi anajua akiacha ufa h

tu hajui ni lini utaangusha Nzagamba anmwangalia kwa mshangao.

" sio kama sikuamini,nakuamini sana lakini simuamini mwanamke yeyote ambaye sio Mimi kukaa karibu yako hasa nikijua hunipendi, naogopa kuwa utampenda,utaniacha juhudi zangu zote za kukufanya unipende zitapotea,na..na..nilipokuona na Lindiwe wivu ulitawala na nikaishia kulipuka samahani" anaongea macho yake yakiwa chini na machozi aliyokuwa akiyazuia kuanguka yanatoka na kutua kwenye mikono yake.

Nzagamba anamwangalia asijue mwanamke huyu ana matatizo gani kwani kwa wanaume wote imekuwaje aje kumpenda mtu kama yeye mwenye mkosi na kujiharibia maisha lakini wakati huo huo roho yake inaruka kama ndama kifuani kwake alichokisema Tulya kinamfanya ajisikie fahari kwa kiasi kikubwa. asijue ni kwa sababu anapendwa au ni nini?

" kwa nini umpende mtu kama Mimi nitakufanya uteseke tu" anaongea akiangalia Mbele kama anaona maisha Yao ya Mbele yatakavyokuwa.

" huogopi?" anamuuliza akiwa bado anaangalia Mbele.

" sio kama ni ukoma" anaongea Tulya akicheka kidogo."mwanzoni nilikuwa sijui kama nakupenda mpaka pale posa ya Manumbu ilipokuja nilipata mshtuko na pasipokujua nilitaja jina lako lakini nashukuru ilinisaidia kuzijua hisia zangu vizuri,kwa hiyo nilifanya maamuzi nikaamua kuufuata moyo wangu na ndio maana Niko hapa"

" utajutia uamuzi wako mambo yakiwa magumu" Nzagamba anaongea akimwangalia ,Tulya nae anamwangalia kwenye macho yake kumuonyesha kuwa harudi nyuma.

" sitajutia endapo tu ukiwa pembeni yangu kwani wewe ni sababu yangu ya kuendelea Mbele,na uniamini kuwa nitakuwa pembeni yako siku zote kwa shida na raha siku zote,hapa pamoja na wewe daima" Tulya anaongea pasipo kupepesa macho maana anajua wanahitaji kuongea kwani tangu waoane hawajawahi kukaa waongee kama wanandoa na anahitaji Nzagamba aanze kumwangalia tofauti hivyo inampasa kuwa muwazi.

Nzagamba anamwangalia mwanamke ambaye haachi kumshangaza Kila siku.

"Kuna nini?" Nzagamba anamuuliza baada ya kumuona Tulya akiangalia huku na kule.

" aaah! nimehisi kama mtu alikuwa anatusikiliza" anaongea Tulya akiweka kipande Cha nyama mdomoni.

" kivipi?" anamuuliza akiangalia huku na kule akiwa na wasiwasi kuwa Tulya alichokihisi ni sawa na kile anachokihisi yeye.

" Amna mtu mbona"

" Sijui siku hizi nimekuwa nikihisi kama Kuna mtu ananifuatilia au kuniangalia" Nzagamba anashtuka kusikia hivyo.

" nini kinaendelea" anajiuliza Nzagamba.