webnovel

chapter 36

"nakupenda" Nzagamba anayasikia maneno haya yakijirudia masikioni kwake kwa mara ya tatu Sasa.Macho yake yanabaki yakimwangalia Tulya ambaye naye anamwangalia kwa macho yake makubwa yaliyojaa machozi."najua huwezi kunipenda kwa sababu moyoni mwako yupo Lindiwe tu,lakini bado nilitegemea heshima kutoka kwako nilichokitaka ni wewe kuithamini ndoa yetu na kuipatia nafasi,sikutarajia mengi kutoka kwako,ilikuwa ni kidogo tu uheshimu ndoa yetu lakini wewe umekuwa uko na huyo Lindiwe wako Kila siku ukija huku mtoni,unajuwa watu watasemaje?"

" unamaanisha nini?" hili linamrudisha Nzagamba duniani.

" hembu niambie ulifuata nini kule,njia ya mtoni wanakochota maji wanawake mbali kabisa na huku?"

" nilikuwa nimet...."

" hapana Nzagamba,sitarajii urudushe hisia zangu ila ninachoomba ni heshima tu,kwangu na kwa ndoa yetu"

Tulya anageuka na kuondoka akilia, Nzagamba anabaki akimwangalia asielewe kimetokea nini.kakosea wapi kuwa njia ya wachota maji ni kosa au anajiuliza.

" subiri" anashtuka na kuanza kumkimbilia

" Tulya subiri" anamshika mkono na kupita mbili yake kumzuia asiendelee kutembea.

" subiri,utakuwa umenielewa vibaya"

Tulya anaendelea kulia huku ameangalia chini.

" niaangalie" anatoa macho yake chini na kumwangalia,macho yake yakiwa yamejaa machozi.'hayo machozi au mvua za masika' anawaza Nzagamba.Anaendelea kumwangalia macho yake makubwa yakiendelea kutoka machozi kadri akipeleka mkono wake kuyafuta yanakuja mengine pua yake ukitoka makamasi membamba ambayo anajaribu kuyafuta na bado yanatoka macho yake yanenda kwenye mdomo wake na kuona lipsi zake zinacheza kidogo kutokana na kulia yanasogea mpaka kwenye shingo yake ndefu iliyokuwa imekaza misuli kwa kulia na kujiuliza inakuwaje mtu anakuwa na shingo ndefu namna ile kama twiga inayotenganisha mabega yake na bado anaonekana vizuri kabisa,utalii wake unaendelea na unafika mpaka kifuani kwake na kukutana na saa sita yake ambayo Tulya hakutaka kabisa kuikaza Leo kwani aliiacha makusudi kwa ajili ya kumtega yeye na kwa sasa zikiwa zikipanda juu na kushuka kwa kasi kutokana na kulia mate yanamjaa mdomoni kama kaona nyama choma anayasukumiza kwa kishindo kooni na macho yake yanarudi usoni kwa Tulya tena " mrembo" wazo linapita kichwani kwake pasipokujua " inakuwaje anakuwa mrembo hata akilia" anawaza akiendelea kumwangalia.

Tulya aliyekuwa ameanza kutulia kidogo anamwangalia kwa mshangao kope zake ndefu zikifumba na kufumbua Kila baada ya sekunde asijue kitendo hicho kinamfanya nini mtoto wa bibi sumbo aliyesimama Mbele yake.Joto la kiangazi linampiga Nzagamba na kujikuta mwili wake ukipanda joto na akilihisi jasho kwenye paji la uso wake.mkono wake uliokuwa kwenye kiwiko Cha Tulya unasogea wenyewe kuelekea juu karibu na begani na anajikuta akisogea karibu zaidi akiendelea kumwangalia.

" Nzagamba"

Wote wanashtuliwa na sauti ya mtu aliyeongea nyuma Yao.Wanageuka na kumuona Mkita akiwa na Lingo wakiwakaribia.Nzagamba anatoa mkono wake haraka Tulya naye anapiga hatua nyuma kuweka nafasi kati yao ambayo Nzagamba alikuwa anaelekea kuiangamiza anaficha uso wake na viganya vya mikono yake vinakimbia usoni kufuta machozi na kujiweka sawa.

" shemeji huyo" Mkita anaongea meno yake yote thelathini na mbili yakiwa nje utadhani kalipwa deni lake la siku nyingi.

" habari zenu" Tulya anawasalimia akilazimisha tabasamu lakini mtihani anaanguka vibaya mno kwani macho yake ni mekundu kuashiria kuwa amelia na uthibitisho zaidi ni michirizi ya machozi iliyoanza kukauka mashavuni mwake nakuacha alama nyeupe.

"ni mda mbaya au" anaongea Lingo baada ya kutema mate ya ugoro wake chini." nadhani" Mkita anaitikia macho yake yakiendelea kuwaangalia Tulya na Nzagamba.

" hapana" Tulya anaongea akiwaangalia na macho yake yanageuka kwa Nzagamba aliyekuwa akimwangalia " Mimi naondoka mama atakuwa ananisubiri,muwe na siku njema" maneno ya mwisho anaongea akiwaangalia Mkita na Lingo na kabla hawajajibu anatoka kama mshale.

" nadhani akipata kichaka Cha kumficha atakimbia hu.." kabla Mkita hajamalizia sentensi yake wanamuona Tulya akitimka mbio.Mkita anaanza kucheka Nzagamba akishika kiuno chake na ulimi wake ukitoka kulamba lipsi zake za chini kichwani akiwa amevurugwa sio kidogo.

" kaka zake watakuua" Lingo anaongea akimwangalia Nzagamba ambaye macho yake yalikuwa bado yapo upande alikopotelea Tulya.

" hao wako mbali,acha Kilinge atakuonea huruma sababu ni maswahiba Zinge atakuuua"

Nzagamba anaachana nao na kuanza kutembea kuelekea kijiweni kwake.

" wapuuzi hawa wameniharibia,mambo yalikuwa yanaelekea kuzuri" analalamika Mnelela aliyekuwa juu ya mti mda wote akishuhudia ugomvi wa Tulya na Nzagamba.

"ndio kilichokuleta hapa,utawachungulia na chumbani au?" anasikia sauti ya kike ikiongea karibu na sikio lake.

" mamaaa!" anapiga makelele Mnelela na kuanguka chini.

" nini unamsumbua mama yako mtu mzima wewe tena usiye hata na uhai" inazungumza tena sauti ikiwa nyuma yake,Mnelela anageuka pale chini na kukutana na mdada.

" wewe nani? na imekuwaje unaniona?"

" Mimi?"

Mnelela anaitikia kwa kichwa.

" nitakwambia" anajibu mwanamke akiwaangalia Nzagamba na marafiki zake .

" mmefuata nini?" Nzagamba anawauliza akiendelea kutembea.

" unajua tumefuata nini'" Mkita anamjibu

wanafika Nzagamba anaenda kukaa kwenye jiwe mkono wake ukienda kuvuruga nyweke zake zilizosokotana kichwani na akivuta pumzi ndefu.

" ohh! wanakimbia wale!" wanamsikia Mkita akipiga makelele wanageuka nakuona ndege waliokuwa wamenasa wanakaribia kujitoa kwenye ulimbo.

" ohhh,aargh!" lingo anajaribu kupiga makelele akielekea mtoni lakini anapaliwa na ugoro wake anaanza kukohoa, Mkita anaingia kwenye maji lakini ndege tayari walishajinasua na kukimbia.

" aaah,mlo wa mtu Mmoja huo" analalamika Mkita akienda kushika mti uliokuwa na ulimbo .

" umeshakauka huu,umetega kuanzia mda gani Nzagamba?" anageuka na kumwangalia Nzagamba aliyekuwa anawaangalia tu mda wote huu.

" ulete huku" Nzagamba anamjibu akimwangalia Lingo akiendelea kukohoa.

" usiniambie umemeza kibando Lingo?"

Mkita anamuuliza huku akitoka kwenye maji, Lingo anayeendelea kukohoa.

" kama amemeza arudi nyumbani kabisa siko kwenye Hali nzuri ya kupambana na mlevi wa ugoro Mimi" Nzagamba anamjibu Mkita huku akipokea mti uliokuwa na ulimbo na kuanza kuutoa ulimbo kwenye mti macho yake yakienda kwa Lingo na kuyarudisha kwenye mti.

" kumetokea nini?" wanageuka na kumuona Ntula.

" kameza kibando Cha ulimbo" anajibu Mkita akikaa karibu na Nzagamba huku akitengeneza rubega yake vizuri.

" oooh,sio mda atakuwa chakari huyo atachangamsha hapa" Ntula anaitikia akitabasamu mkono wake Mmoja unaenda juu na kushika tawi la mti lililokaribu yake huku uzito wa mwili wake akiuegesha kwenye mguu Mmoja mwingine akiunyanyua na kuupindisha juu ya mwingine.

" Nzagamba kasema aondoke hajisikii kukaa na mlevi Leo" Mkita anamjibu macho yake yakimwayamwaya kama kaokota swala wa kulisha familia yake siku tatu na ulimi wake ukiwa nje ukilamba midomo yake kama katoka kuiba asali anahakikisha kufuta ushahidi kabisa.

" kwa nini? wakati Lingo akilewa hutoa raha tu" anajibu Ntula akimwangalia Nzagamba aliyekuwa Yuko makini na kazi yake ya kuweka ulimbo kwenye mti macho yake yanarudi kwa Lingo ambaye bado anaendelea kukohoa akiwa ameinama na vidole vyake mdomoni.

" kunywa maji" anamwambia na wakati huo anamsikia Mkita akijibu swali lake " kagombana na shemeji"

" ehhh?!" anauliza Ntula kwa mshangao na hapo hapo wanamsikia Lingo akitapika.

" kaitoa hiyo" Mkita anaongea akicheka hali ya Lingo, Ntula anaenda alipo Lingo nakuanza kumpiga piga mgongoni huku akicheka Nzagamba anawaangalia nakutikisa kichwa chake anaendelea kuzungusha ulimbo kwenye mti.

" ohhh,hiyo ilikuwa karibu" anaongea Lingo huku akikaa chini akihema.

" kunywa maji na uache kula maugoro yako,hata sijui unayapendeaga nini" Ntula anamwambia akishika kiuno.

" usinipigie kelele bwana,mbona wewe sijawahi kukwambia uachane na Kiko yako"

" Shauri yako" Ntula anamwambia akiondoka kuelekea walipo Nzagamba na Mkita.

" mbona uko mwenyewe" Mkita anamuuliza Ntula baada ya kukaa karibu yake.

" sijapita kwao,Nina uhakika wanaijua njia maana sio vipofu" anamjibu akiwazungumzia Kilinge na Zinge.

" na imekuwaje kugombana na shemeji?" anauliza akimwangalia Nzagamba.

" hata hatujui tumewakuta njiani pale shemeji macho puuu kwa kulia" Mkita katika ubora wake akionyesha kwa kidole alikowakuta Nzagamba na Tulya.

" Zinge atamuua"

" nimeshasema mda..ouch!" analalama Mkita kwani Nzagamba kampiga na mti wenye ulimbo kichwani anauvuta kwa nguvu na Mkita anpiga makelele kwani ulimbo unaondoka na nywele zake na mwingine kubakia. anautoa lakini ulimbo mwingine unabakia kwenye nywele.

" itakuchua wiki huo kutoka" anaongea Lingo akija kukaa karibu yao akifuta mdomo wake.

" ndio nini hiki?" anaongea Mkita mkono wake ukiwa kichwani ukijaribu kutoa ulimbo lakini anavuta na nywele.

" acha utoto kaweke mtego huko kama hutaki kulala njaa" Nzagamba anamjibu akilaza mgongo wake kwenye jiwe na mikono yake ikiegemea kichwa kufanya mto macho yake yakienda juu kuona matawi ya mti yakicheza.

" nakupenda" sauti ya Tulya inapita kichwani kwake mapigo ya moyo yanaenda juu na anafumba macho yake na kuvuta pumzi ndefu sura na macho ya Tulya akilia yanapita machoni pake.

" Nzagamba" anashtuliwa na sauti ya Ntula anageuza kichwa upande aliko na kumwangalia.

" tunauliza umemfanya nini shemeji mpaka alie" Ntula anamuuliza

" kwa inavyoonekana hujampiga" Lingo anaongezea.

" Nzagamba hapigagi wanawake mmesahau Sheria yake au?" anaongea Mkita akisimama na mti wake wa ulimbo nakuanza kuelekea kwenye mto sura yake ikiwa bado imekereka na mkono wako ukiwa kichwani kupambana na ulimbo kwenye nywele.

" hajamkera tu" Ntula anaongea

" tena usiombe awe na mdomo kama mke wa Nsio" Lingo anaongezea na Ntula anacheka.

" sema kweli eti umemfanyeje,labda tutakusaidia njia ya kubembeleza unaweza kulala nje eti" Lingo anaongezea.

" amenikuta na Lindiwe"