webnovel

chapter 25

" kwa nini?" anamuuliza huku mikono yake ikiendelea kuchezea ukindu aliokuwa akijitahidi kuanzisha ukili akimegelezea mama mkwe wake namna anavyoshona.

" unajua sisi wawindaji tunategemea wanyama kwa Kila kitu kwa ajili ya kuishi kwa hiyo wanyama wakiondoka hatutaweza kuendelea"

" si tunaanza kulima na kufuga" anamuuliza

" huwezi kulima au kufuga katika ardhi iliyolaaniwa mwanangu"

" ardhi iliyolaaniwa?kivipi?"

" ardhi yetu ni kwa ajili ya kuwinda tu na imekuwa hivyo tangu enzi za mababu na mababu na mizimu inayolinda ardhi yetu ni ileile inayoamini katika uwindaji ukitaka kubadili hilo itabiidi upate mizimu inayoamini katika ufugaji na ukulima na hiyo itawabidi kuchangia mizimu na wakulima na wafugaji na sidhani kama watakubali hilo,na itakuwa ni tatizo lisilotatulika huko Mbele na je mizimu yetu utaupeleka wapi kama haijatulaani kwa kuiona Haina kazi" anaongea bibi sumbo na kuendelea.

"Katika Kila jamii Kuna mizimu inayolinda jamii hiyo kutokana na chimbuko lao,ufugaji,uwindaji,uvuvi,na wakulima kwa hiyo huwezi kuichanganya mizimu hii iliyopo katika eneo husika kwa kulazimisha ifanye kazi nyingine utajikuta katika wakati mgumu sana kama haijatulaani kwa kutokuitii mwanangu"

" sikujua kama kulikuwa na mgawanyiko wa mizimu" anaongea tulya akifumua ukili wake uliomshinda kutengeneza kwani ulikuwa unafumuka Kila akishona nyuma unaachia.

" nipatie hiyo" anaongea bibi sumbo akinyoosha mkono ili Tulya ampatie ukindu wake naye anampatia.

" kuanzisha ukili ni kazi ngumu sana na huwa inawasumbua wengi sana,angalia ninachokifanya hapa" anaanza kumuonyesha na Tulya anamwangalia kwa makini akisuka polepole iliaone Kila hatua.

"usipofunga vizuri huku mwanzo utakuwa unakusumbua tu kama ulivyokuwa unafanya kwako hata usuke urefu gani huku nyuma utaachia tu kwa hiyo hakikisha huku mwisho unaacha nafasi ndefu kwa ajili ya kuunganishia utakapomaliza" anamuelekeza.

" Na kuhusu mgawanyiko wa mizimu ndio,upo na ndio maana Kila jamii Ina sadaka yake pale wanapoenda kufanya matambiko"

" je ni ipi yenye nguvu zaidi?"

" ni ile inayomiliki ardhi"

" inayohusika na wafunyanzi?" anauliza Tulya akikumbuka siku Bibi Sumbo ameenda kumtembelea nyumbani kwa mjomba wake baada ya harusi Yao kupangwa alizungumzia hili baada ya kumuona akifinyanga vyungu.

"ndio,unakumbukumbu nzuri" anamsifia baada ya kuona bado anakumbuka maneno yake kwani ingekuwa vijana wengine wangeshatupa mbali kwenye jiwe yasiote kabisa.

" mizimu inayomiliki ardhi inanguvu kuliko mingine kwani hivyo vyote viko juu yake na ikiamua kuwa Kila kitu kilicho juu yake kiteketee kinateketea nahisi ndio maana mmliki wake amepewa mwanamke mwenye huruma la sivyo tungekuwa na shida kwa sababu tunaiudhi Kila siku"

"na inayofuata?"anauliza kwa shauku ya kutaka kujua zaidi.

" ni mmiliki wa maji,maji yakipotea hatuna pa kwenda" Anaongea bibi sumbo na Tulya anakubaliana nae kwa kichwa.

"pale awali ulisema wanyama wakitoweka ni vibaya mbona Sasa wanyama wamepungua na nilisikia kaka zinge na kilinge wakisema siku hizi wanatembea umbali mrefu kutafuta wanyama je hii inatokana na kulaaniwa kwa ardhi uliyosema"

Anaongea na kumfanya Bibi Sumbo amwangalie kwa tabasamu akijua ni jinsi gani Tulya alivyo na akili ya kunyaka mambo haraka bila kuacha hata maelezo madogo .

" ndio,inasemekana ardhi yetu ililaaniwa miaka mingi iliyopita ikiwa ni Karne nyingi sana ni hadithi ambayo imekuwa ikitembea katika vizazi vyetu na watu wengi wakijua ni hadithi tu lakini kadri unavyoishi na kuona mabadiliko yanayotokewa kunakuja kuamini"

" sijawahi kuisikia hadithi hii" anaongea Tulya sura yake ikakaa katika Hali ya kufikiria kama alisikia lakini amesahau.

"huwezi kuisikia kwani ni hadithi iliyokatazwa hivyo watu wengi hawaijui" kwanini nahisi kama Bibi Sumbo anajua mtungi umebeba nini kuliko anavyoonyesha anawaza Tulya akimwangalia mama mkwe wake.

" inasemekana miaka mingi iliyopita mizimu ya ardhi ilimchagua mmiliki wa ardhi aliyejulikana kwa jina la Ndesha.Ndesha alikuwa ni mfinyazi mzuri sana na alikuwa ni mpole sana.kama unavyojua mmliki wa ardhi inambidi aolewe na mtemi"

Tulya anamkatisha kwa kumuuliza " kwa nini mtemi ni lazima amuoe mmliki wa ardhi?"

" swali zuri" anaitikia bibi sumbo akimpatia ukili alioushona kwa umbali mrefu kwa kumsaidia kuendeleza.

" Sasa unaweza kuendelea kushona kuanzia hapo siku nyingine ukitaka kushona ukili itakubidi uanze kama nilivyokuonyesha hapo"

" sawa" anaitikia huku akiuopokea na kuanza kushona.

" Mtemi anatakiwa kuwa ni mwindaji tena hodari na yeye pia huteuliwa na mizimu mwindaji hawezi kuwinda kama Hana kibali kutoka mizimu ya uwindaji na ndio maana Kila mwaka tunafanya matambiko kuomba mizimu iachilie baraka,ila mtemi inabidi aipate kutoka kwa mmliki mwenyewe"

" inamaana Kila mtemi anaoa mfinyanzi?"

" hapana sio wote,na wale ambao hawajaoa wafinyazi wanakuwa hawana nguvu kama wale wanaooa mmliki wa ardhi"

" kwa nini wengine hawezi kuooa mmliki wa ardhi?"

" kwa sababu wamiliki wa ardhi hutokea mara chache sana Kila baada ya Karne,mlongo au miaka kadhaa, mpaka mizimu itakapo pata mtu wa kurithisha nguvu zao,kwa hivyo kuwapata nivigumu"

Tulya anatikisa kichwa kuonyesha kaelewa anachokizungumzia na bibi sumbo anaendelea

" kilichotokea kwa Ndesha ni kwamba ilikuwa baada ya kukutana na mtemi aliyetakiwa kumuoa alikataa kuolewa nae na kusema hakustaili kuwa mtemi"

" kwa nini?" anauliza kwa mshangao

" hatuwezi jua" anachezesha mapega yake" ila wanasema wamiliki wa ardhi wananguvu za kusoma sura ya mtu"

" akamuona amejaa tamaa" Tulya anajibu na mama mkwe wake kuitikia kwa kichwa.

" ndio,lakini mtemi huyo aliyekuwa amenusa harufu ya madaraka hakutaka kukubaliana na hilo hivyo alilazimisha kumuoa Ndesha kwa kutishia kuua watu wa familia yake yote lakini bado alikataa kwani hakuwa tayari kuangamiza watu wengi kwa ajili ya kuokoa familia yake"

Siku Moja akiwa ameenda kufuata udongo porini Ndesha walikuja walinzi wa mtemi na kumkamata kwa nguvu wakampeleke nyumbani kwake akamuoa kwa lazima na kulazimisha kulala naye kwa nguvu,kwa sababu guvu za mtemi huja pale wanapokamilisha ndoa Yao na kufuata Sheria zingine .

Mtemi alijua amezipata zile nguvu lakini bado hakufanikiwa kuzipata kwani inasemekana Ndesha alizificha nguvu hizo na hii ilimkasirisha sana mtemi.

Mganga wake mkuu akamwambia endapo watamtoa sadaka Ndesha nguvu zake alizoficha kwenye mwili wake zitatoka na kumwingia mtemi,na kwa sababu mtemi alikuwa anataka sana madaraka alikuwa Yuko radhi kufanya chochote.

Walimfanyia kitu kibaya sana Ndesha kwa kumtoa kafara kwa mizimu mibaya waliofanya makubaliano nayo na ikiwaahidi kuwapatia nguvu endapo wakiipata damu ya Ndesha.

Walimuua na kumwacha chini ya mbuyu waliofanyia kafara kwa muda wa siku tatu kama mizimu ilivyowataka walimtaabisha sana.Na baada ya siku tatu mtemi alipokea nguvu kama alivyoahidiwa.Lakini mzima wa Ndesha ulikasirika sana ukailaani ardhi pamoja na mtemi na kuanzia mda huo Mambo mengi yalibadilika.

"ni mtemi gani aliyekuwa mkatili namna ile?" anauliza Tulya kifua chake kikijaa hasira kwa ukatili aliyofanyiwa Ndesha.

" na hamna mtu aliyesema chochote hata familia yake?" anazidi kuuliza

" Familia yake yote iliuwawa siku aliyotolewa kafara Ndesha kulikuwa na fujo kubwa sana baadhi ya wazee waliokuwa wakipingana na mtemi nao waliuuawa pamoja na familia zao na mtemi akipiga marufuku kwa tukio hilo kuzungumziwa popote yeyote atakayesikiwa analizungumzia anauwawa kwa kosa la kumtukana mtemi"

" ndio maana hakuna mtu anayejua,lakini wewe umejuaje mama?"

" unadhani hata kama ukizuia maneno yasiongelewe watu wataacha?"

" hapana"

" ndio,hawataongea Mbele yako lakini wataongea kwa Siri,ndivyo hadithi hii imekuwa ikiendelea kwa miaka yote hii"

" ni miaka mingapi imepita tangu Ndesha auwawe?" anauliza akiwa ameacha kushona ukili wake.

" ni Karne tano Sasa"

" Karne tano?inamaana hajatokea mmliki wa ardhi tangu miaka hiyo?"anauliza kwa mshangao.

" ndio,ila Karne mbili zilizopita alitokea mtabiri Mmoja akatabiri kuwa nguvu ya ardhi itarudi tena pamoja na mtemi mwenye nguvu ambaye hajawahi kutokea mpaka Sasa"

Hili lingine tena anawaza Tulya moyoni.

" ameshatokea Sasa?" anauliza.

" bado,kwa sababu mtabiri aliyetoa utabiri huo alinyongwa,pamoja na ile familia iliyoambiwa itakuja kumiliki wote waliuwawa?"

" na mtemi huyo huyo au?" anauliza Tulya akishangaa mtemi huyu aliishi miaka mingapi.

" hapana,ni kizazi chake"

" hicho ni kizazi Cha nyoka kinatakiwa kutoweka kabisa dunuani" anaongea Tulya na kumfanya Bibi Sumbo atabasamu jinsi anavyofanya tukio kuwa lake.

" lakini kitu kikipangwa hakuna wa kukipangua najua mambo yatakuja kubadilika tu na huo utawala mbaya utafikia ukingoni" anaongea Bibi Sumbo akiendelea kushona ukiri wake.

" lakini kwa wakati huo nadhani tutakuwa tumekufa kwa njaa au Kila kitu kitakuwa kimeteketea" anaongezea Tulya

" hapana mizimu haiwezi kuangamiza na waliowema"