webnovel

chapter 18

Anamwangalia manumbu na kupiga hatua Moja nyuma kuweka umbali kati Yao 'kwani hii siku inaendaje' anajiuliza.

" nikuuliza wewe,unafanya nini hapa" manumbu anamuuliza akipiga hatua nyingine kumsogelea,tulya nae anapiga nyingine nyuma kumkimbia.

" haikuhusu"

manumbu Anacheka kidogo " kwa mwonekano wako hauna furaha" anatulia kidogo " furaha inatoka wapi kwa shimo ulilojichimbia,ndio maana umekuja kukaa mtoni,vipi unajuta kunikataa Mimi au"

Tulya anamwangalia kwa dharau " hapana,nijute Ili iweje wakati nimeamua mwenyewe"

" una uhakika,kwa sababu ninavyojua Mimi utakuwa haulali usiku ukihofia maisha yako yatakavyokuwa,kula ndege Kila siku mpaka unaingia kaburini,bado hujachelewa ukirudi kwangu nitakupokea kwa mikono miwili na nitakupenda mpaka kufa"

tulya anamwangalia kwa kutokuamini anachoona na kusikia anajua lindiwe alimchukua kwa swaga hizihizi na Sasa anamfanya ngoma.

" nisikilize manumbu.." lakini manumbu anamkatisha " utakuwa hujui maisha yetu sisi wawindaji tunaishije sababu umekulia kwa wafugaji.lakini maisha ya hapa pasipo kuwinda ni magumu sana hatuwezi kufuga wala kulima kutokana na mazingira yetu,ukiolewa na nzagamba uzuri wako huo wote utapotea na utaanza kujuta tufanye kama Mimi nakufanyia msaada tu"

" nisikie wewe manumbu,Bora niharibike sura kuliko kuolewa na mwanaume ambaye anamtenda vibaya mwanaume mwenzie kwa faida yake,wewe uliyembinafsi na kujifikiria wewe tu huwezi kunioa Mimi, na kingine Mimi tayari ni mchumba wa mtu unachokifanya kinakushusha hadhi,nzagamba ni Bora kuliko wewe"

uso wa manumbu ulioiva kwa hasira unamtisha tulya lakini bado anasimama kibabe na kumwangalia.

Manumbu anapiga hatua ndefu kabla tulya hajafikiria Cha kufanya tayari anamshika mkono wake.

" Sasa nitakuonyesha kama Mimi ni Bora kuliko huyo nzagamba wako" anaanza kumvuta na tulya anawaza afanye nini kwani manumbu alikuwa na nguvu kumzidi.

" unafanya nini,niachie,niachie nimesema" anampiga mkono wake uliokuwa ukimvuta kuelekea vichakani pasipo mafanikio,anashusha uso wake na kuung'ta mkono wake lakini bado hakumwachia,tulya anaona huu ndio mwisho wake akiharibiwa Amna mtu atakayetaka kumuoa zaidi ya kulazimishwa aolewe na manumbu na watu kumuita Binti asiyejiheshimu.

mawazo mengi yanampita kichwani akiomba msaada kwa mizimu kwani hakuwa radhi kukumbana na jamii ambayo ingemuhukumu maisha yake yote pamoja na kizazi chake.

Wakati akiendelea kupambana na mwazo anashangaa manumbu akianguka chini kama kapigwa na kitu kizito.anageuka na kumuona nzagamba anapata nafasi anakimbia na kujificha mgongoni kwake.

" unadhani unafanya nini" nzagamba anamuuliza na kuinama chini kumpiga ngumi nyingine ya taya manumbu anajizoazoa chini na kutema vitu vyekundu.

" naona unakipaji kuzuri sana Cha kuchukua wachumba zangu" anamuuliza uso ukionyesha hasira isiyokifani

" haubadiliki wewe" manumbu anajizoa pale chini na kusimama.

" nani mchumbaako" anaongea huku akiendelea kutema mate.

" huyo hata hakupendi,anafanya hivyo kwa sababu ana hasira na Mimi kwa kilichotokea siku ile usiku unaweza kwenda tuache sisi tuongee tuyamalize"

nzagamba anageuka na kumwangalia tulya aliyekuwa akitikisa kichwa kuashiria kukataa ' anatafuta kuniharibia kabisa huyu' anawaza.

" kwa nilichokiona Mimi wewe ndio uliokuwa unamlazimisha kuongea yeye hataki au Mimi naingilia kitu hapa" anaongea nzangamba kwa sauti yake ileile ya taratibu kana kwamba hajakasirika akimwangalia tulya.

" hapana Mimi sikutaka kuongea nae" anajitetea na nzagamba kumgeukia manumbu.

" kiongozi gani wewe usiyekuwa na mfano watu wakijua ulichokifanya hapa watakuchukuliaje,lindiwe atajisikiaje akisikia kilichotokea Nina uhakika ataumia sana kwa nini usijiheshimu"

mfupa wa hasira unamkaba tulya kooni akiwaza kuwa nzagamba anamhofia lindiwe tu wakati yeye ndie aliyekuwa kwenye matatizo hapa anajipatia uhakika kuwa bado anampenda lindiwe licha ya kuolewa na manumbu anafuta machozi yake yaliyokuwa yamefika kidevuni pasipo yeye kujua.

" toka hapa nisikuone tena la sivyo nitakuharibia Kila kitu na usirudie tena" anamwamru na manumbu anaamka na kuanza kujikongoja akiondoka.

"na wewe" anamgeukia tulya aliyekuwa kwenye mawazo " kwani si unatakiwa kuwa ndani unafanya nini hapa, tena ukiwa peke yako"

" bado,naanza kukaa ndani kesho" anajibu kwa kigugumuzi akijizuia kulia macho yake yakiwa kwenye mkono wake alioushika manumbu na Sasa ukiacha alama za vidole vyake.

nzagamba anamwangalia kwa muda.

" nenda nyumbani" anaongea na kabla tulya hajajibu anaanza kuondoka.

" nilitaka kuongea na wewe"

nzagamba anasimama na baada ya muda anageuka na kumwangalia,tulya anapiga hatua za taratibu mpaka pale alipo macho yake yakiwa chini pumzi zikimkata.

" nilitaka nikwambie kuwa sitaweza kuvunja uchumba kama ulivyosema sababu Mambo yamefika mbali, nakuomba samahani"

nzagamba anamwangalia pasipo kusema kitu na tulya ananyanyua uso wake na kumwangalia na macho yao yanapokutana anarudisha tena chini baada ya kuona nzagamba hasemi kitu anaendelea " samahani kwa kukutumia wewe kumkataa manumbu, nakuapia halikuwa lengo langu,tangu nifike hapa Kijijini vijana niliokuwa nawasikia ilikuwa ni manumbu,Tinde na wewe. siku hiyo nilipoambiwa naolewa na manumbu sikuwa na namna kwani manumbu simpendi na Tinde ni mchumba wa sinde nikasema Kuna mtu nampenda nilipoambiwa nimtaje sikuwa na namna kwani mtu aliyebakia alikuwa wewe tu ninaekujua kwa hiyo nikakutaja kwani sikutarajia kama mjomba angeleta posa kweli,samahani sana lakini Sasa nitafanya Kila liwezekanalo kwa ajili ya uhusiano wetu Ili nisikuaibishe zaidi nitawajibika kwa makosa yangu"

" kwani Mimi unanipenda"

"eeh!"

anagutuliwa na swali lake na kunyanyua kichwa kumwangalia usoni macho yao yanakutana wanaangaliana kwa mda tulya anashusha uso wake asijue Cha kujibu moyo wake ukienda mbio.' kwani nampenda' anajiuliza.

" nenda nyumbani"

nzagamba anageuka na kutaka kuondoka

" unanichukia " tulya anauliza

" nikikwambia nakuchukia utavunja uchumba"

" kwa sababu bado unampenda lindiwe" swali linamshtua kidogo nzagamba anapiga hatua na kumsogelea karibu

" nikikwambia nampenda na nitaendekea kumpenda utavunja uchumba"

tulya ananyamaza na kuendelea kuchezea vidole vyake Koo likimkaba kwikwi ya machozi ikimponyoka mdomoni kwake kuona nzagamba hakatai upendo wake kwa lindiwe.

" nenda nyumbani" na kwa neno hilo anaondoka akimwacha tulya kasimama pale machozi aliyokuwa akiyazuia yakimdondoka,anajitwisha kibuyu nakuondoka. unalia nini wakati wewe mwenyewe humpendi shida Iko wapi anajisemea akielekea nyumbani.

Kama ilivyo mila kesho yake tulya hakuruhusiwa kutoka nje tena wala kushika chochote shamra shamra za kumtunza zikianza,wamama na mabinti waliolewa na wasioolewa wakija pale kumsalimia na kutwanga mahindi na mtama wakitengeneza chakula kitakachopikwa siku ya harusi na pumba kutumika kumpaka mwali kwa ajili ya kulainisha ngozi na wengine kuleta mafuta mbalimbali ya wanyama na mimea kwa ajili ya kumpaka.tulya hakuwa na marafiki kwa sababu alikuwa ni mgeni Mahali hapa ila marafiki zake sinde na mama yake runde ndio waliokuja na alishukuru sana kwa hilo.

ingawa wengi walikuja kwa tumbo la umbea lilikuwa limewabana la kutaka kumuona mwanamke anayeolewa na nzagamba Kuna wengine waliodiriki kumuuliza amempendea nini na wengine kumuonya kuwa atajuta afikirie uamuzi wake na wengine kumpa ushari mzuri wakisema ndoa ni ndoa tu muhimu ni upendo na heshima yote hayo yalimpa faraja kwani yalimsogezea siku na kumpunguzia upweke wa kukaa peke yake ndani.

" mda wa kuoga maji tayari" sauti ya sinde inamshtua kwenye mawazo pale kitandani.

" kwa nini nisiioge tu usiku wakati wa kulala" anajitetea akikaa vizuri.

" hapana ni lazima ukaoge Sasa hivi"

" joto sana sinde,kamwambie mama nimeshaoga"

" amka,Mimi mwenyewe nataka siku ya harusi uwe nyororo kama nyoka, nzagamba akikushika unateleza" sinde anatania na kucheka kwa nguvu huku akimvuta anyanyuke kitandani.hali ilikuwa ni ngumu kwa tulya kuoga maji ya moto Kila siku asubuhi,mchana na jioni kwa msimu huu wa joto,lakini inamlazimu kwani hiyo ilikuwa ni Sheria.

"shangazi anakuja kesho eeh"

" mmh"

" nitafurahi kumuona na kukaa nae kwa mda mrefu kipindi amekuleta hata hakukaa" sinde anaongea lakini tulya anatulia tu akiingia kwenye dimbwi la mawazo.

" unawaza nini"

" vipi Kama mama na baba wasipompenda nzagamba " tulya anaongea wasiwasi wake.

" usiwe na tatizo,licha ya matatizo yake, nzagamba bado ni kijana mzuri sana na haimchukui mtu mda mrefu kuanguka katika dimbwi la mapenzi nae Nina uhakika shangazi akimuona lazima atazimia moyo wewe utaona" tulya anatoa tabasamu.

"na ni afadhali ya nzagamba kuliko hao wazee aliposema wakuoe" sinde anaongezea huku tulya akiitikia kwa kichwa kukubaliana nae akianza kuelekea nje.

"nzagamba amekuja kukuona" swali la sinde linamzima miguu tulya na kusimama.

" ndio"

" kweli ee! lini? akasemaje?"

" Sasa hivi hapa si unamuona"

furaha ya sinde inamtoka usoni baada ya kuelewa maana ya alichokisema tulya.tulya anatoka na kuelekea nje kuoga akijifunika gubigubi mpaka kichwani kwani kimila na desturi watu wengi hawaruhusiwi kumuona sura mpaka siku ya harusi.

" itabidi nifanye kitu" anajisemea sinde anayemwonea huruma tulya kwani tangu aanze kukaa ndani hii ni wiki ya pili Sasa nzagamba hajaja kumuona,Sheria huwa haziruhusu lakini vijana wengi hutoroka nyakati za usiku kwenda kuwaona wachumba zao wakiwa wali wakiwapelekea zawadi mbalimbali na hii inaitwa kujiiba lakini nzagamba hajaja hata mara Moja.aje kwani ananipenda si kaanguka kwenye mtego tu asiweze kutoka,anajiwazia tulya akiingia bafuni.