webnovel

chapter 16

Tulya anaangalia mikono yake inayouma kwa kutengeneza vyungu machozi yanazidi kumdondoka asijue afanye nini?anafanya Kila kitu kwa ajili ya ndoa yake na kuridhika kukaa na nzagamba licha ya udhaifu wake ambao hakutaka kuuzungumzia kwani tayari watu wameongea mengi juu ya hilo.Yeye alichokuwa anakitaka ni kukaa pembeni yake kumtia nguvu,kuwa kama kivuli chake popote anapoenda ajue Kuna mtu ambaye hajali matatizo yake na hajaliona tatizo lake kabisa lakini nzagamba anamchukia na hataki hata kumtia machoni.Hawezi kuvunja uchumba safari hii kwani mambo yamefika mbali,wazazi wake wamepelekewa taarifa tayari na wanajiandaa Kuja kwa maandalizi ya harusi hataki kuwatia aibu nyingine tena kwani sio wao tu watakao aibika mjomba ake pia Mzee Shana atakuwa matatizoni ndugu yake sinde bado hajaolewa je hiii ikileta picha mbaya na uchumba wa sinde kuvunjika pia yeye atakuwa mgeni wa nani?

Macho yamevimba kwa kulia anawaza mengi kichwa kikimpasuka kwa msongo wa mawazo na kulia kwa mda mrefu wimbi zito la usingizi linampitia pale kitandani,sinde anakuja kumchungulia na kumuona amelala akaona ni afadhali kwani muda ule tulya alimtoa aende nyumba kubwa na amwambie runde kuwa amechoka amelala kidogo kujipumzisha na kumfanya sinde aahidi kutokusema kitu chochote kwa wazazi wake mpaka pale atakapojua Cha kufanya na sinde amefanya hivyo.

Mida ya jioni kabla jua halijazama tulya anashtuliwa na sinde aliyekuja kumwamsha

" amka Vaa vizuri njoo huku nje mama mkwe wako amekuja" sinde anaongea kwa sauti ya chini.

" eeh!" wenge la usingizi linamtoka tulya anaamka haraka na kujitengeneza vizuri anavaa viatu vyake na kusimama.

" Yuko wapi" anauliza

" nyumba kubwa anaongea na mama,nadhani alijua umeshakaa ndani tayari kaja na vitu vyako vya kukutunza"

wanatoka haraka na kuelekea nyumba kubwa, wanafika na kumkuta bibi sumbo na runde wakiwa wamesimama uani bibi sumbo akiangalia baadhi ya vyungu alivyofinyanga tulya havikuwa vibaya sana kwa umbo ukizingatia aliyefinyanga ndio mara yake ya kwanza kushika hata udongo, ni mwanzo mzuri anafurahishwa zaidi na tabia ya tulya ya kuanza kuwajibika kabla hata ya kuolewa, na kuona mwanae anabahati sana kupata mwanamke kama tulya na kuona mizimu haikumnyima vyote.

"shikamoo" bibi sumbo anakeuka na kumuona tulya aliyesimama nyuma yake akiwa ameinamisha kichwa

" nimekwambia usifanye hivyo Mimi ni mama yako Sasa" bibi sumbo anakumbusha tena tabia ya tulya kuangalia chini akiwa anaongea nae.tulya ananyanyua uso wake kumwangalia bibi sumbo lakini sio kwa mda mrefu na hakuweza kumwangalia machoni zaidi macho yake yamepita juu juu tu na kuishia kwenye nywele zake kichwani zilizokatwa na kuelekea upande mwingine.

Licha ya tulya kuwa waruwaru hajasahau mafunzo aliyoyapokea akiwa mwali.namna ya kuishi na mumewe pamoja na wakwe zake na ni jinsi gani anatakiwa kuwa akiwa Mbele Yao licha ya bibi sumbo kumpa uhuru hakutaka kuutumia vibaya usije ukamgharimu.licha ya hivyo roho yake ilimtuma kumpa heshima anayostaili bibi huyu.

" samahani umenikuta nimepumzika kidogo" tulya anatoa tabasamu zuri kumzuga bibi huyu asijue kilichopo moyoni mwake.

" Haina shida mwanangu,najua utakuwa umechoka" bibi sumbo anarudisha tabasamu na macho yake kuelekeza kwenye vyungu vilivyowekwa kwenye kichanja

" mama yako kaniambia Kila kitu,na nimependa kazi yako ni nzuri sana"

" hapana mama bado najifunza" tulya anaongea akisogea karibu na kichanja akiangalia vyungu vilivyofunikwa.

Bibi sumbo anachukua kimoja na kukirusha kidogo juu kama anapima uzito.

" hapana, umefanya vizuri kwa mtu uliyejifunza kwa siku tatu tu hii ni hatua kubwa sana, ona.." anakirudha tena chungu juu na kukiweka juu ya kichanja " .. sio vizito, na hii inamaanisha hujaweka udongo mwingi umevikadiria sawa kabisa hata ukivichoma havitakuwa vyepesi sana na ukifinyanga mitungi watu wengi wataitumia kuchotea maji kwani haitakuwa mizito,najivunia sana wewe.

Tulya anatoa tabasamu akifurahi kujua Kuna mtu anathamini anachokifanya.

" kwani unajua kufinyanga?" anauliza wakianza kutembea kutoka uani kuelekea upande wa pili wa nyumba waliko sinde na mama yake.

" kwa nini,naongea sana au" anauliza bibi sumbo akisimama na kumwangalia usoni na tulya anainamisha uso haraka.

" hapana,nilikuwa simaanishi hivyo nimeshangaa tu kuona unajua Mambo mengi kuhusu vyungu"

bibi sumbo Anacheka kidogo

" bibi yangu alikuwa mfinyanzi mzuri,na hamna mtu aliyerithi,Mimi nilijaribu kujifunza nikashindwa kwani wakati mwingine udongo huchagua mtu wa kuuongoza"

"kivipi,nilijua ukiupenda kutoka moyoni tu unaweza kufinyanga" tulya anaongea na kumwangalia bibi huyo usoni akitaka kujua zaidi ni kama amepata mwalimu mpya.

" kuupenda tu haitoshi" bibi sumbo anaenda kukaa kwenye gogo tulya nae anamfuata na kukaa pembeni yake hawakuwa na haja ya kutafuta kivuli jua la jioni hakikuwa Kali hivyo wanalipatia migogo Yao kukwepa kukunja nyuso zao wakiliangalia.

" wewe mtu akija kukuvua nguo na kuchezea utajisikiaje?"

"vibaya"

" ndivyo ulivyo udongo,Kuna mizimu inayolinda udongo nayo huchagua mtu wa kuutunza udongo kwani watu wengine hujawa na roho za husda pale wanapogundua talanta walizonazo na kupoteza thamani ya udongo na wao,kwa hiyo udongo ukiupenda, ukauthamini na kuupatia kipa umbele nao utakutunza na endapo mizimu ikikuchagua kumiliki udongo ujue unamiliki ardhi yote na hiyo inahitaji busara kubwa kwani ukikiuka miiko unalaaniwa kipaji kinapotea pia"

" kinapoteaje?"

" wengi mikono Yao huanza kukataa kushika udongo namaanisha akishika udongo mikono inatetemeka,au akitengeneza vyungu vinavunjika,vyungu ni vya thamani sana kwani ndimo vinavyotoka vyakula vyotevyote baada ya ardhi"

" je, ni nani mmiliki wa udongo na ardhi?" tulya anazidi kuuliza kwani hakujua kama ufinyazi una maana kubwa ndani yake na hii imekuwa ni hadithi nyingine kwake na amejawa na shauku ya kutaka kujua zaidi.

" bibi yangu aliniambia hajawahi kutokea kwa miaka mingi sana,kwani mmliki wa ardhi siku zote hutembea na mtemi,na watemi wote waliopita hata wa Sasa Hana mfinyanzi hivyo ni lazima tujue mizimu haijachagua mmiliki bado"

Tulya anazidi kutokuelewa mfinyanzi na mtemi Kuna husiana nini,anaona kumbe ufinyanzi unazaidi ya kufinyanga vyungu.Bibi sumbo anamwangalia tulya akipambana na ubongo wake kuchanganua Mambo. tabasamu linamtoka mdomoni na kuona mkwewe ni mdadisi sana na Yuko kama mbwa kichaa aking'ata haachii utamuulia hapohapo,kuna upande wa moyo wake unafurahia hilo na upande mwingine ukihofia kwa yatakayomkabili mbeleni kwa tabia hiyo itakuwa ni vigumu zaidi kwake.Anatikisa kichwa chake kutupilia mawazo hayo pembeni akijua mizimu itashughulikia mengine.

" usijali,ukijua kujifunza mwalimu wako atakuelekeza zaidi kwani Kila mfinyanzi lazima ajue hayo"

Tulya anawaza kama mama yake runde anayajua hayo na hata kama anajua itakuwa sio kama bibi sumbo.

" ulikuwa unalia?"

anashtuliwa na swali la bibi sumbo anageuka na kumwangalia usoni lakini alikuwa hamwangalii macho yake yalikuwa Mbele kama Kuna mtu mwingine anaongea nae huko lakini walikuwa wawili tu na Moja kwa Moja akajua swali lilikuwa lake anapeleka mikono yake machoni kuyafikicha macho yake akijiuliza amejuaje na imekuwa mda mrefu tangu amalize kulia na wakati anatoka alimuuliza sinde kama macho yake yamevimba sinde akasema yako vizuri sema wekundu wa usingizi tu huyu kajuaje.

Anamwangalia nakuona anajiuliza tena kajuaje bibi sumbo ananyoosha mkono wake wa kushoto uliokuwa na bangili mbili kutokana na yeye kuwa mjane haruhusiwi kuvaa urembo mwingi na kama amevaa zile mbili zitakuwa na maana yake na tulya kujiuliza maana yake nini lakini hakuwa tayari kumuuliza.vidole vyake vinagusa chini ya macho yake na kusema

" macho yako yamekakachaa kama umeoga maji ya chumvi ndio maana nikajua ulikuwa unalia kwani haiwezekani ukaoga maji ya chumvi kwa sababu hapa Kijijini hatuna"

Bibi sumbo anamshangaza tena tulya,kwani tayari alishajua kilichotokea tulya hakutaka kumwongopea kama alivyopanga kwani inavyoonekana bibi huyu anaona mpaka ini la ng'ombe anaetembea na hakutaka kujikamatisha uongo na kumfanya amchukie pia, kuchukiwa na nzagamba kunatosha kwa Sasa na bibi huyu akimchukia hiyo ni dalili ya punda kuota pembe na yeye anajua atasimama upande gani endapo hilo litatokea hivyo anaamua kukaa kimya macho yake yakiangalia vidole vyake anavyovichezea kama anaona baridi na akitafuta joto kupitia mikono.

" umeonana nae?" anauliza tena na tulya kugeuza macho kumwangalia macho yao yanakutana na tulya kugeuza haraka.

" lazima amekuja na atakuwa ameongea mengi" bibi sumbo anavuta pumzi ndefu.

" unajua nzagamba amepitia mengi sana, nadhani umeshasikia mengi tangu uje hapa Kijijini"

"ndio "

"alishakata tamaa kabisa ya kuoa Mimi tu ndio niliyekuwa nampigia makelele lakini hakutaka hata kusikia,hivyo taarifa za kuoa zilipomfikia alishtuka sana,lakini hakuwa na kipingamizi kikubwa kiasi hicho kwani alijua utakaa baada ya mda utakimbia tu na kumuacha ukijua ukweli,nilivyomwambia unajua Kila kitu inaonekana kama aliridhia lakini sio kutoka moyoni alikuwa na mashaka,naona baada ya kusikia kilichotokea kati yako na manumbu kimembadili zaidi"

"nisamehe kwa hilo" tulya anaangalia chini kwa aibu

" usiseme hivyo,Mimi sikulaumu ninachoshukuru ni wewe kumchagua yeye kati ya wanaume wengine wote tofauti na manumbu" anatulia kidogo kama akimpima tulya kama kamuelewa na kuendelea

" hata Mimi mwanaume anayepiga namkumbia" anatania bibi sumbo na wote Wanacheka

" ninachoomba ni uvumilivu tu,namjua mwangu anaroho nzuri mkioana atawajibika na kadri muda unavyokwenda atajifunza kufungua moyo wake tena na atakupenda, mwanaume gani anayeweza kupuuzia mrembo kama wewe" tulya anaona aibu kidogo mama mkwe wake kumsifia

"naomba uwe upande wake utaniahidi hilo tulya" anamshika mikono,tulya anaangalia mikono yake na kuona imepauka pia kucha zake fupi sana Moja kwa Moja anajua kuwa hazikuwi kutokana na kufanya kazi mda wote,bila kutarajia na yeye anaweka mikono juu ya mikono ya bibi sumbo akimwangalia kwa tabasamu la ujasiri

" usijali,nakuahidi nitakuwa pembeni yake" anaahidi na bibi sumbo kutoa tabasamu pia.

Bibi sumbo anasimama tulya anasimama pia,wakati huu jua limeshazama kukibakiwa na mawingu ya dhahabu tu upande wa mgharibi Giza likiiandama mashariki mpaka utosi wa mbingu bibi sumbo anaanza kutembea kuelekea uliko mlango wa nyumba kubwa tulya nae akimfuata nyuma.

" Mimi naondoka,nitakuja kukuona siku nyingine,ukichoma vyungu unibakizie kimoja nitakuja kuchukua"

"sawa"

" na uwe makini usije ukaungua,bibi harusi hatakiwi kuwa na makovu"

"sawa"

bibi sumbo anaaga na kuondoka,tulya anaenda kusaidiana na sinde kupika baada ya kula wanaenda kulala.ilimchukua mda mrefu kupitiwa usingizi akiwaza Mambo mbalimbali waliongea na bibi sumbo akinzia la mfinyanzi kuwa mmliki wa ardhi akitaka kujua zaidi kuhusu hilo na mwisho akamalizia na nzagamba roho yake ikilipuka kwa kitendo Cha kumuwaza tu macho yake makali yakimfanya mwili kusisimuka kwa woga.Anayatupia mbali yote hayo na kuamua kutafuta usingizi kwani kesho ni siku nyingine tena kwake,anajifunika kaniki mpaka kichwani na haikuchukua mda kwa usingizi mzito kumjia.

Ilikuwa ni mchana nzagamba akipiga kalimba kama ilivyo kawaida yake akiwa juu ya mtu huku amefumba macho yake kuufurahia mziki na kusahau yote.

" nzagamba"

anashtuliwa na sauti iliyomuita na kuangalia chini,anashangaa kumuona aliyekuja anashuku kwa kujirusha na kutua chini

"umefuata nini hapa"