webnovel

chapter 10

wote wanageuka na kumwona lindiwe manumbu anamwachia tulya mkono 'hili Balaa tena' anawaza tulya anamwangalia lindiwe aliyekuwa anamwangalia kama anataka kummeza kwa macho.Tulya anaamua kumpuuzia na kuondoka pasipo kutia neno,kabla hajafika mbali anakutana na sinde "nilikuwa nakuja kukutafuta,unaendeleaje" anauliza sinde baada tu ya kumuona " Niko sawa,tunaweza kwenda nyumbani" anajibu tulya akiweka mikono yake kiunoni " bado kifua kinauma?" anauliza sinde kwa wasiwasi " hapana sijisikii tu kukaa hapa tena" " utakuwa unaumwa kweli wewe unakimbia hadi ngoma" sinde anamshika paji la uso kumpima " nimekwambia Niko sawa" sinde anamwangalia kwa mashaka " najisikia vizuri Sasa hivi sema tu nimechoka tunaweza kuondoka kama umenielewa" tulya anamwakikishia.

kabla sinde hajafanya maamuzi wanasikia watu wakigombana kule alikotoka tulya "makelele hayo kina nani wanagombana" sinde anataka aende kuangalia tulya anamzuia "acha twende huko mtakuja mpigwe ngeu ugomvi usio wahusu" tulya anajua fika ni manumbu na lindiwe watakuwa wanagombana na yeye ndio atakuwa sababu anamvuta sinde waondoke kabisa kabla vumbi halijamfikia.usiku huo tulya hakupata usingizi mawazo yake yote yakitawaliwa na nzangamba asijue ni kwa nini.

Ni wiki Sasa imepita tangu siku ya sherehe, nzagamba anatoka akiwa na ulimbo kwenye kijiti na mwingine akiuweka mdomoni nakuanza kuutafuna na kutema mate akiulainisha " mama Mimi naondoka" anamuaga mama yake aliyekuwa ndani sauti yake ikiwa nzito kutokana na ulimbo uliojaa mdomoni,bibi sumbo anachungulia na kumuona kijana wake na kijiti Cha ulimbo mkononi huku akiichomeka kalimba yake kiunoni "wenzako wanaweka sime kiunoni wewe unachomeka kalimba, kwa nini usibebe hata upinde tu" nzagamba anamaliza kuweka kalimba yake kiunoni "utakuwa mama kumbukumbu zako sio nzuri siku hizi,umesahau kuwa mwanao hata nitembee usiku wa manane hakuna kitakachonidhuru"

bibi sumbo anatoka nje akiwa na kipeo chenye viazi "sijapika Leo beba Viazi hivi utakula mtoni" anampatia lakini nzagamba anachukua kiazi kimoja tu "rudisha hivyo hiki kinanitosha,tangu Jana tunakula viazi tu" "wewe ulitaka tule nini,kama unataka kula vizuri si uoe mkeo akupikie humuonei hata huruma mama yako nimezeeka sina hata mtu wa kunichotea maji,hembu niambie ukweli ulipoenda siku ya tambiko hukupata hata Binti au tukatafute Kijiji Cha jirani" nzagamba anamwangalia mama yake rohoni akiwaza 'akipata nafasi tu hashwindi kuitumia ipasavyo' anaamua kuondoka akijua maada ya kuoa haitaisha karibuni "unanipuuzia au Mimi naongea wewe unaondoka we nzagamba wewe,hivi usiponisikiliza Mimi utamsikiliza nani baba yako angekuwepi ungemfanyia hivi" anamsikia mama yake akilalamika anaendelea kutembea tu," nawaambieni mizimu mwanangu asipooa na mwakani hakuna mbuzi" bibi sumbo anaendelea kutangaza vita na mizimu akirudi ndani.

Anafika mtoni na kuweka mitego yake sehemu nzuri akiwa amezungushia ulimbo kwenye vijiti sehemu ndege wanapokuja kunywa maji Ili wakitua wanase kwenye ulimbo. anasimama pembeni na kuangalia kama imekaa vizuri baada ya kujihakikishia anatoka kwenye maji na kwenda kusimama chini ya mti mkubwa anaangalia jua Kali la mchana lililokuwa limewaka "kiangazi kinakaribia kuisha miti itaanza kuchipua na mwaka utakaribia kwisha" anasikia sauti nyuma yake anageuka na kuona nzagamba mdogo akiwa na baba yake Mzee kizinga wakiwa wamekaa chini ya mti huo juu ya jiwe kubwa lililopo chini ya mti .

Miaka kadhaa iliyopita nzagamba akiwa bado mdogo akijiandaa kwenda jando walipenda Kuja kukaa hapa na baba yake mara nyingi Mzee huyo akiwa na wosia wa kumwachia kijana wake "jua limekuwa Kali sana siku hizi" nzagamba anamwangalia nzagamba mdogo aliyekuwa amelalia mgongo wake na mikono yake akiiweka chini ya kichwa chake akiwa amefumba macho na Mzee kizinga akiwa amekaa.zilikuwa ni kumbukumbu zake za miaka ya nyuma pindi baba yake bado Yuko hai. Yalikuwa ni majira kama haya " Kila majira yanawakati wake na lazima yaje, Sasa tunaukaribia msimu wa miti kuchipua kuwa na maua mazuri na matunda yasionyeshewa mvua" anaeleza Mzee kizinga.

Nzagamba anafungua macho na kukaa taratibu kama usawa aliokaa baba yake "napenda matunda ya michipuo sana hasa sanse msimu ukifika tutaenda wote nyuma ya mlima kutafuta baba" anaongea nzagamba kwa shauku akimfanya baba yake acheke " ndio mwanangu tutaenda endapo mizimu ikitujalia uzima" anaongea Mzee kizinga tabasamu lake usoni likififia na macho yake yakijawa na huzuni nzagamba analiona hilo lakini kabla hajafuatilia macho ya baba yake yanarudi kawaida tena "Nina uhakika tutakuwa wazima baba na tutaenda wote" anamtia moyo baba yake na Mzee kizinga anatabasamu.

Anatoa kidani kilichotengenezwa kwa ngozi ya chui chenye kichuma chini kinachoning'inia kama kengele na kuanza kumfunga kwenye msuli wake wa mkono "kwa kuwa msuli wako bado mdogo nimekuwekea mkanda wa kuvuta Nina uhakika ukiwa mkubwa mkandaa huu utakutosha" anaongea Mzee kizinga akikagua kidani kama kimekaa vizuri "lakini hii si ulitakiwa kunipa nikitoka jando?" anauliza nzagamba akiwa na wasiwasi kwamba hamuelewi baba yake " ndio naelewa lakini ni Bora kuwahi kuliko uchelewe ukose kabisa" anageuka na kutoa mkuki usiokuwa na fimbo yake na kumpa" huu ni mkuki wa ukoo wetu kawaida hupewa mtoto wa kwanza lakini Mimi nakuamini sana wewe kuliko kaka zako Nina uhakika utautunza vizuri na kulinda heshima ya ukoo wetu kwa sababu wewe ni jasiri sana niahidi utafanya hivyo" anasisitiza Mzee kizinga nzagamba anaupokea "kwa nini usingempa kaka mkubwa"

Mzee kizinga aliyekuwa na wake wawili bibi sumbo akiwa mke mkubwa sababu uzao wake ulikuwa wa shida Mzee kizinga alioa mke wa pili na kuzaa nae watoto watatu wakiume ambao wote ni wakubwa kwa nzagamba ndipo bibi sumbo alipopata ujauzito na kumzaa nzagamba na baadae mke mdogo bibi leangi alizaa mtoto wa kike mmoja na kumfanya Mzee kizinga kuwa na watoto watano.mzee kizinga alimwamini sana nzangamba kwani licha ya umri wake mdogo alikuwa na akili,nguvu na maarifa akijua akimwachia majukumu ya familia ataitunza vizuri.

"hapana hata wewe unastaili mwanangu na siku zote ukumbuke majukumu ya ukoo wetu yapo mikononi mwako na hautaniangusha na ujue popote nitakapokuwa nitajivunia wewe" nzagamba aliyekuwa anaelewa kwa nini baba yake anafanya hivyo anaangalia pembeni kuzuia machozi yake.

Siku mbili zilizopita usiku akiwa amerudi nyumbani akitokea ngomani aliwasikia wazazi wake wakiongea kwani walijua bado hajarudi muda wa ngoma kuisha ulikuwa bado lakini yeye aliwahi kurudi " sitaki,mtoto bado mdogo kizinga usimfanyie hivyo majukumu ya ukoo ni makubwa mno" aliongea bibi sumbo akilia, nzagamba anataka kuingilia aulize nini kinaendelea anamsikia baba yake akisema "sina Cha kufanya mke wangu mizimu inaniita nisipofanya Mambo mapema nitachelewa na nikiondoka utawala ukaenda kwa mtu mwingine ukoo wetu utaharibikiwa" nzagamba alihisi mwili wake ukifa ganzi hakuamini alichokuwa anakisikia kwani Kila mtu anajua kutembelewa na mizimu mana yake nini,bibi sumbo aliendelea kulia "nyamaza mke wangu unatakiwa kuwa imara kwa ajili ya mtoto wetu inanivunja moyo kuwaacha namna hii lakini sina usemi juu ya hili na wewe unalijua hili vizuri, nisikilize kwa makini" nzagamba aliyekuwa anataka kuondoka anasimama tena nakutaka kusikia baba yake anasemaje " Mimi nitamkabidhi mkuki nzagamba lakini Mimi nikiondoka uuchukue na kuutunza sehemu salama mpaka pale mda utakapofika nzangamba akaweza kuutunza ndo ummpe na umueleze kila kitu"

bibi sumbo aliyekuwa analia kwa Sasa alikuwa ametulia na Mzee kizinga anaendelea "unajua huo mkuki unamaanisha nini na ni watu wangapi wanautafuta hatima ya maisha ya mbeleni ya himaya nzima ya mpuli ipo kwenye mkuki huo,Hakikisha upo salama kabisa na ukumbuke maneno ya mtabiri vizuri usije ukapuuzia hata kidogo" anasisitiza Mzee kizinga " utabiri umekuwa wa Karne nyingi hujawahi kutimia una uhakika gani kuwa utakuwa juu yetu sisi" anauliza bibi sumbo na kumfanya nzagamba kule njee kupoteza wazo la baba yake kutembelewa na mizimu na akili yake kuhamia kwenye utabiri ambao hajawahi kuuisikia "sisi hatuwezi jua hilo lakini mtabiri aliyekuja siku nzagamba amezaliwa alisema mda ukifika atakuja tena mpaka wakati huo tunatakiwa kuwa makini" nzagamba aliamua kuondoka hakutaka kusikia zaidi kwani moyo wake tayari ulikuwa unamuuma kumpoteza baba yake.

urudi wakati Mzee kizinga akimkabidhi mkuki nzagamba anakubali majukumu yote aliyokuwa anamwachia baba yake " sawa baba nitalinda ukoo wetu kwa nguvu zangu zote nakuahidi" anasimama na kupiga goti Moja chini lingine juu na kukutanisha mikono yake juu akikunja ngumi kwa mikono yake yote miwili kuonyesha kukubali majukumu mazito ya kulinda ukoo katika umri mdogo.

Nzagamba mdogo na baba yake wanapotea pale kwenye jiwe na nzagamba mkubwa aliyesimama akipaangalia pale akirudi katika Hali yake anavuta pumzi ndefu na kujisemea " ni afadhali tu baba ulitangulia mapema ungekuwa mzima ungeweka wapi sura yako kwa aibu hii" anapanda juu ya mti na kutoa kalimba yake akiwaza ni utabiri gani ambao baba na mama yake walikuwa wanauzungumzia na familia yake au ukoo wake unaficha Siri gani,anaamua kupuuzia mawazo yake na kuanza kupiga kalimba yake.

Tulya na sinde wakiwa wametoka mtoni wanaisikia sauti ya kalimba "nzagamba ndo anafika saa hizi" anaongea sinde nakuanza kufuatiza mziki wa kalimba na mluzi wake.

Tulya aliyekuwa kimya nyuma akisikiliza mapigo ya moyo wake yaliyokuwa yakipanda Kila baada ya sekunde anapunguza mwendo.sinde anageuka na kuona kamwacha nyuma anasimama na kumsubiri " uko sawa" anauliza baada ya kumuona tulya akipumua kwa shida " kifua kinabana" " tena?" anauliza sinde " haya jikaze tufike nyumbani ukanywe dawa" wanatembea polepole mpaka wanafika nyumbani sinde anaweka kibuyu chake haraka na kumsaidia tulya kutua Cha kwake " nenda kapumzike ndani nakuletea dawa" anaagiza sinde akiingia nyumba kubwa.

Tulya anaingia ndani nyumba ndogo na kujilaza kitandani baada ya muda anafika sinde akiwa na mzizi mkononi "tafuna hii umeze maji yake, mbona ulikuwa sawa tu kimetokea nini" anauliza akikaa kitandani alipo tulya.Tulya anaupokea na kuanza kutafuna akifikiria mapigo yake ya moyo yanatokana na nini 'muziki' anawaza 'ndio muziki Kila akisikia mziki wa nzagamba mapigo ya moyo yanaenda mbio moyo unaanza kumsukuma kama akimbie aende amkumbatie amwambie usijali hauko peke yako nipo hapa kwa ajili yako hata Dunia nzima ikimtenga Ili apate faraja aache kupiga mziki huo wa huzuni Kila siku.

Tulya anaona akiacha kusikia mziki wa nzagamba atakuwa sawa " sinde ninaweza nikaacha kwenda mtoni kwa muda mpaka kifua changu kitakapopona" anakuja na sababu ya muhimu ya kukwepa kwenda mtoni " ndio Haina haja ya kuuliza na nitamwambia baba akutafutie mizizi mizuri utapona tu" sinde anamfariji.Wakiwa ndani wanasikia makele nje " mbona kama ni sauti ya kaka kilinge hii wanagombana na nani" anauliza tulya wote wakinyanyuka na kutoka njee.

Kutoka nje wanamuona kilinge na zinge wakipandishiana sauti " nimekwambia sijui chochote niseme mara ngapi" anajitetea zinge "kwa nini usijue wakati mda wote mpo wote" tulya na sinde wanafika na kuingilia kati " Kuna nini kaka kilinge" tulya anauliza,kilinge hajibu chochote anaondoka akiwa na hasira na kuwafanya sinde na tulya wamwangalie zinge " sijafanya kitu Mimi mbona mnaniangalia hivyo" anajitetea zinge baada ya kuona wadogo zake wakimwangalia kama mkosaji " Sasa kwa nini kaka kilinge akukasirikie" anauliza sinde na wote wanamwangalia kwa jicho la kutokumwamini na kumfanya zinge acheke kidogo " sijagombana nae,na wewe tulya jiandae nasikia umepata mchumba na wanakuja kukuona kabla jua halijazama" anaongea zinge akikimbia kuelekea anakoenda kilinge akimwita amsubiri.

Huku nyuma tulya anabaki kama amemwagiwa maji ya baridi " amesemaje yule?"