webnovel

NAFSI ILIYOUTEKA MOYO

Kelvin_Wambea · Urban
Not enough ratings
2 Chs

SUBILA SANIFUU...

Nafsi iliyobeba Subila Kwa kipindi Cha muda pasipo kutambua kama fikra zipo sahihi Kwa kiumbe ninachokipenda kuliko kiwango Cha hisia za kibinadamu, kuna wakati nahisi Wenda nikimtizama tu basi moyo wangu utakuwa na furaha sanaa na ndivyo inavyokuwa pindi tu nikiona sura yenye tabasamu lake zuri na mashavu yenye dimpoz... Ucheshi wake, mienendo yake, tabia yake nzuri na staili yake ya maisha vinanivutia sana kitu kinachofanya nizidi kumpenda Kila baada ya sekunde moja hakika nimezama katika hali isiyokuwa ya kawaidaa

Lakini ilikuwa ngumu kukutana nae na kuzungumza kumjuza ni jinsi Gani maisha yangu yaliyo jaws upendo juu yake ndani ya moyo wangu yanavyoendeshwa na hisia za mwili kiasi kwamba siwezi vumilia kukaa na hata kusinzia pasipo kumuwaza yeye... Alionrkana mtu ambae hapendi kampani ya wavulana pia yupo bize sana muda wote, ni mtu anaependa kujishughurisha na elimu pamoja na dini tu na si mambo mengine hata nilipomuita hakutaka kuja pia hakupenda kusikiliza...

Nilifikiria ni mtu asiependa maswala ya mapenzi na anaechukia wanaume wenye mtizamo huo juu yake hivyo sikutaka niwe chukizo na kikwazo Mbele yake Imani yangu ni kuwa siku moja nitamjuza dhamira yangu nae atanipatia jibu sahihi ili nifanye hitimisho la fikiria zangu kuwa hapendi wanaume... Kwa kuwa Mimi pia ni mtu wa dini na ninasoma Kwa juhudi pia hivyo nikaamini kwamba popote pale nafsi hii itakapokuwepo basi nitajitahidi isiwe mbali NAMI..

Kanisani tulikutana tulitizamana pasipo kuongeleshana na wakati mwingine tulisalimiana tu,Kila mmoja alifanya mambo yake ilikuwa ni jambo linaloniumiza lakini sikuwa na budi kutulia na kuvumilia nikiamini upendo wangu utasafiri kumuelekea nae ipo siku atanipenda tu... Niliamini hivyooo siku zote na miaka ikapita...

Wakati mwingine nikafikiria Wenda ni kweli Sina sababu ya yeye kunipenda na Sina sifa za kuwa nae kwenye mahusiano pengine hanipendi kweli.. nikahisi kukataa tamaa na kusubilia uhalisia wa mitazamo yangu pengine Wenda itokee miujiza kwake ili siku moja katika mawazo yake basi ipite taswila yangu na mitizamo yake iwe juu yangu nae achambue uwepo wangu katika mboni za macho yake... Na ikiwa akiri yake ikakubali kutengeneza sehemu ya kumbukumbu yangu ili atunze matukio yangu na kuifanya sehemu ya muendelezo wa maisha yake basi afikirie kuishi NAMI.....