1 SURA YA 1

MWAKA 2070

 

  Ilikuwa asubuhi yenye baridi kali anga lilitandwa na ukungu. Madereva wa vyombo vya moto waliwasha taa zao ambazo ziliwasaidia kuona mbele Ili kuepuka kusababisha ajari. 

Ndani ya gari moja aina ya MERCEDES BENZ G CLASS, kulikuwa Na watu wanne walikuwa wamevaa miwani myeusi iliyowasaidia kuona magari yaliyo mbele Yao bila hata kuwasha taa za gari Hilo. Maana ilikuwa miwani ya kieletroniki inayotumia mionzi.

  Dereva wa Gari hilo alionekana ni mwanamke mmoja mwenye midomo laini na sura nzuri ya kuvutia. Miwani myeusi aliyoivaa Ndiyo ilificha uzuri ulio katika macho yake na ilimfanya aonekane mwanamke ambaye ni UNAPPROACHABLE yaani ni ngumu kuwa karibu naye.

  "NANA G Naomba ongeza kasi tuweze mfikisha kwa wakuu Huyu mtu inaonekana ni mtu wa muhimu sana. Tuiwahi ndege ya saa mbili katika uwanja wa SONGWE INTERNATIONAL AIRPORT. 

"This is our last chance tumepoteza muda mwingi kumtafuta Huyu mtu ambaye ilikuwa sio rahisi kuamini kwamba anaishi maisha ya ukulima wa mazao huku uyole". Alisema mmoja wa wale watu wanne walikuwa ndani ya gari aliyekuwa ameketi karibu Nana G.

  "Sawa MICHAEL ondoa Shaka kuhusu hilo but before I woke my monster please tighten your seat belts sihitaji lawama juu ya kitakachofata." Nana G alisema huku akiikaza mikono yake juu ya usukani na kukanyaga mafuta nyuso yake ikionesha kuwa yupo kazini.

Gari lilipita kwa kasi majira ya saa kumi na mbili na kukunja kulia na kuicha njia inayoelekea Ziwa ngozi njia ya kwenda nchi jirani MALAWI . Na kufata njia inayoelekea UYOLE sehemu iliyochangamka kwa kiasi chake katika jiji la mbeya.

  Ndani ya nusu saa gari aina ya Mercedes Benz g class ilikunja kushoto kufata Barabara inayoelekea NANENANE , hali ya hewa ilikuwa bado si shwari manyunyu yalikuwa yakishuka taratibu kutokana na hali ya ukungu mzito.

"I think I have to take the top lane tutachelewa sio kwa msongamano wa magari haya ya mizigo. Nana g alisema huku akiangalia nyuma kwa kutumia kioo kidogo kilicho mbele ya gari hilo.

  "Yanaelekea zambia hayo jaribu kufanya unavotaka tuwahi flight kabla hatujaikosa na muda wa kazi yetu ukawa umepitiliza." Sauti nyororo ya kike ilisikika ambaye aliyekuwa kimya toka safari imeanza.

Pembeni yake kulikuwa na kijana mwanaume aliyeonekana amepitiwa na usingizi. Lakini kitambaa cheusi kilifunika uso wake.

  "Bado hajaamka tu? Aliuliza Michael baada ya kuona mtu waliyetumwa kumfata bado hajaamka mpaka sasa. 

"Hii dawa ya usingizi Ni toleo jipya kutoka Kwa jopo la wataalamu wa madawa kwenye kikosi, it will take almost three hours till it wears out" Alijibu Alicia aliyekuwa karibu na kijana huyo aliyepitiwa na usingizi.

  "That means bado kama saa moja aamke? Aliuliza nana huku akiongeza mwendo wa Gari hilo.

"That's right nana kabla hatujafika airport atakuwa tayari yupo macho." Michael Ndiye aliyejibu wakati huu huku akiangalia saa iliyokuwa mkononi mwake.

 

  ****

 

 

 

 

 

 

IGOMA UYOLE

"Habari za sahizi kijana? Sauti nzito ilisikika na kumfanya kijana aliyekuwa yupo busy na shughuli za kilimo kugeuka na kuona mtu asiyeweza kumtambua.

Salama habari za sahizi? Aliuliza kijana huyo ambaye alionesha wasi wasi juu ya ujio wa mtu huyo.

  "Salama tu, samahani nimeelekezwa nije huku shambani kwamba nitamkuta mtu ninaye mtafuta maana Nina shida naye." Aliongea yule mtu mwenye sauti nzito huku akijaribu kusogea karibu ya kijana yule.

Unamtafuta nani kwani? Kijana yule aliuliza

"Namtafuta kijana mwenye miaka ishirini na Saba hajaoa na amemaliza elimu ya juu katika chuo kikuu cha dar es salaam naweza fahamu yupo wapi? Sauti nzito ilisikika tena.

Wh...Who are you? Kijana aliuliza huku nyuso yake ikionesha kutofurahishwa na taarifa alizotoa yule jamaa. Maana katika kijiji hicho ni yeye pekee aliyefanikiwa kufika elimu ya chuo kikuu. 

"Mimi ni moja wa rafiki wa rafiki yake nimeagizwa kumfata huku" ilisema sauti ile

"Huenda Huyu mtu hajui sura ya mtu aliyetumwa amtafute but Kama ni wale watu ninaowajua Mimi Basi huenda wana picha zangu za zamani Na hawajui nikoje kwa sasa.

Ngoja nijiweke Sawa huenda wamekuja tena kunifata wale watu niliokutana nao mwaka 2067. Yule kijana alifikili na aliinama chini bila kuonesha kwamba anajiandaa kwa mbio katika milima ya upoloto ambayo inasifika kwa kuwa na miti ya aina nyingi ikiwemo mipine, miti ya biashara katika milima hii.

"Nitawapoteza kwenye pori lile la babu, hawawezi nishika na muda umeenda Giza linaingia sio muda. Yule kijana alitafakali huku akifunga vizuri Kamba za viatu alivyovaa siku hiyo.

Kijana unamfahamu huyo mtu nayemuulizia maan nimeelekezwa nije kwako nitapata majibu sahihi.

"Kaka simfahamu mtu huyo unaye muulizia labda uende mbele kidogo utakuta kuna vijana wengine waulize huenda wanamjua." Alisema huku akiinuka baada ya kukaza kamba.

  "Sawa hakuna shida ngoja niende mbele unakosema, asnte kwa taarifa." Ilisikika ile sauti nzito.

Mara baada ya kusogea hatua ishirini kutoka alipokuwa kijana yule simu ya yule jamaa ili ita na bila kusita akaipokea.

  "Nimefanikiwa kupata picha yake ya sasa katika chumba chake nakutumia whatsapp fungua uangalie tusipoteze muda kumtafuta, kumbuka we have a deadline of this mission." Sauti ya mwanadada ilisikika na bila shaka ilikuwa ni sauti ya mwanadada mrembo asiyetaka utani katika kazi ambaye jina lake aliitwa Nana Adam mwanguku.

  Yule jamaa bila kupoteza muda alifungua picha katika programu Husika na kuona sura ya mtu anayemtafuta. 

Na kwakuwa alikuwa na kumbukumbu kali Alijua tu Huyu ndye aliyezungumza naye muda mfupi uliopita.

"Kijana subiri kwanza" yule jamaa aligeuka nyuma na kukuta mtu aliyezungumza naye dakika chache zilizopita akitimua mbio kuelekea upande wa pili wa barabara, ambako kuna msitu mkubwa wa miti ya asili na ile ya kupandwa.

  Yule kijana alitimua mbio kuliko kawaida Na milima ilionekana tambarare Kwa wakati huo maan Aliweza kukwea mlima Kama nyani hii Ni kutokana na uzoefu wake wa muda mrefu wa kuishi katika maeneo hayo.

Yule jamaa alipoona mtu aliyemuita hataki kugeuka nyuma alifanya maamuzi ya haraka ya kupiga simu kwa wenzake watatu waliokua katika Gari aina ya MERCEDES BENZ G CLASS na kuwataarifu kuwa yawezekana mtu wanayemtafuta ndyo huyo anapanda kilima kwa kasi.

"You can see him he has just passed by you and he is heading to the other side of the road. Kuna msitu mkubwa tuangalie tusije mpoteza.

"All of you take your tools and run toward him. We need to catch him before the sun sets this is our chance." Alitoa maelekezo haraka katika moja ya kifaa kilichofungwa pembeni ya shati lake lenye rangi ya kijani.

"Got you captain our eyes are on him we're ready for pursuit." Mabinti wawili na mwanaume mmja walishika njia kutoka walikokuwa na kufata uelekeo wa mtu aliyekuwa akikimbia kwa kasi ya ajabu, bila kuangalia nyuma.

"He is so fast" nana alisema kumjulisha captain wake aliyekuwa akielekea uelekeo waliokuwa wao.

"Use you tools take him down" ilisikika sauti ya mamlaka na ndipo nana aliposimama na kuchukua sindano iliyokuwa na rangi ya blue na kuiweka katika SNIPER RIFLE na kwa kutumia kiona mbali kilicho juu ya bunduki hiyo , aliweza kuona namna kijana yule akikwea upande wa pili wa msitu wa kupandwa.

"Eagles eyes on him he is in my target now he can't escape" nana alisema huku kijasho chembamba kikishuka toka kwenye paji la uso wake laini. Na dakika chache baadae akabonyesha kiachia risasi na kumlenga kijana yule aliyekuwa akikimbia.

Sindano ilipita kwa kasi ya ajabu na kuwaacha nyuma vijana wawili waliokuwa wakimfukuzia kijana aliyekuwa mbele yao na kumpata kijana huyo kwenye sehemu ya juu ya uti wa mgongo.

Dawa iliyokuwa katika sindani ilisambaa kwa haraka baada ya kuingia katika mfumo mkuu wa neva ambao ni uti wa mgongo na kusambaa kwa haraka sana na kumfanya kijana yule aanguke baada ya kukimbia kwa hatua ishirini mbele.

"That's nana g" sauti ya kike ilisikika na kugeuka nyuma kuona ni kweli nagrina ameshika bunduki mkononi mwake.

"Got him" alisema nana katika kifaa cha kuwasiliana na dakika chache alitokea captain wa kikundi hicho na kumpongeza kwa kazi nzuri.

  "Go and confirm if it's him" alisema na kisha nana alisogea walipo wenzake waliokuwa wakisubiri wenzao wafike ndio wamtoe sindano iliyokuwa karibu na shingo.

Ichomoe hiyo sindano tayr dawa ishaingia na hawezi kuamka kwa masaa kumi na nne kutoka sasa. Alisema nagrina na kumuamuru mmja wa vijana wale.

  Alicia chomoa taratibu na mgeuze tuhakiki kama ni yeye tunayemtafuta. 

Sawa nana aliitikia Alice na kisha kufanya kama alivyoagizwa.

"It's him" alisema nana baada ya kufananisha na picha aliyokuwa nayo kwenye kifaa chake cha kielekroniki.

"Take him in the car" aliamuru Michael captain wa hicho kikundi na George alimtupia begani mwake kama furushi la viazi na kuanza kushuka naye kuelekea uelekeo walikoliacha gari lao.

  "Inatupasa tuondoke haraka iwezekanavyo na kuiwahi ndege inayoelekea dar es salaam itatoondoka kesho saa moja, kutokana na maelekezo tuliyopewa kazi inabidi iishe kesho saa sita mchana. Tutaiwahi ndege katika uwanja wa ndege wa SONGWE AIRPORT na kumfikisha makao makuu." alisema Michael na kisha kupiga simu ambayo haikupokelewa kwa wakati huo.

"He must be a very important man, mpaka mkuu katutuma huku tumfuate Huyu kijana" alisema Alice ambaye alikuwa kimya toka walipokuwa wakirejea taratibu kuelekea kwenye usafiri waliokuwa nao.

avataravatar
Next chapter