webnovel

MSUMALI

Mapenzi ni kama msumali, msumali ukiwa mpya unyooka, lakini, tatizo huanza msumali huo ukishaanza kugongwa na nyundo, hapa huitaji umakini ili msumali huo usipinde, hata hivyo, kupinda sio tatizo, tatizo ni namna ya kuunyoosha na usivunjike, huu ndio wakati ambao umakini mkubwa zaidi huitajika vinginevyo msumali huo utavunjika.

John_Raphael_8794 · Realistic
Not enough ratings
1 Chs

BAADA YA SIKU 365, MWAKA ULIPINDUKA NA KUINGIA MWAKA MPYA AMBAO ULIKUWA NI KWAKA 2020.

Kuna watu wawili wanapendana, namna wanavyoishi inavutia kuwashuhudia.

Kama ukipata bahati ya kuwaona hawa watu wawili, mvulana na msichana, mme na mke, utasema mh!, kwenye hii dunia ya duara dufu kuna watu wanapendana jamani!!!.

Lakini cha kushangaza!, watu hawa hawana mtoto hadi leo 2020 ambao ni mwaka wa pili tangu wameingia kwenye ndoa.

Kuna sababu juu ya upendo wao wa dhati na kuna sababu juu ya kwanini hawana mtoto ikiwa daktari Antony Mbona aliwathibitishia kuwa hawana matatizo yoyote ya uzazi, na hata uchumi wao ukiutazama, unaruhusu kuwa hata na watoto zaidi ya watano kwani, Jerry ni mnajimu wa serikali, alikuwa mtu wa kucheza na habari za nyota na anga, habari za kubashiri kama mvua itanyesha kesho au hainyeshi. Alikuwa mtaalamu wa anga, alijua majina yote ya nyota:- nyota ya jaa na nyota ya mshale, akrabu, na akraksi, alijua habari zote za mwezi:- mwezi mchanga na mpevu, kalisto, titania, miranda na yuropa.

MIAKA MIWILI NYUMA, ILIKUA MWAKA 2018, ILIKUA HIVI:-

Merry na Jerry wakiwa kwenye uchumba.

Merry: Bebi, ivi kwanini mahusiano uvunjika!.

Jerry: Kwa sababu uvunjikaa..., kwanini umeniuliza hivo wangu!.

Merry: Kwasababu mi' staki kuona mapenzi yetu yanavunjikaa....

Jerry: Oke, Mapenzi yanavunjika kwa sababu nyingi, lakini, hata kama nitakutajia sababu, sitoweza kuzitaja zote maana zipo nyingi mno, ngoja nikutajie ninazoziona mimi:- kwanza, kuzoweana kupita kiasi hadi unakuta wapenzi wanaanza kuvunjiana heshima.

Merry: Unamaanisha makuzi au!

Jerry: Eeeh.., yaani sio kama yasiwepo, hapanaa...ila isiwe kupitiliza.

Merry: Sawa wangu, endeleaa...

Jerry: Pili, Tamaa, yaani unakuta mtu ana mtu wake lakini bado anahtaji kuwa na danga, pia wanawake wanakuwa sana na tamaa ya pesa.

Merry: Mh mbona hapo umesema kwa wanawake tu, kwani mwanaume hawawezi kuwa na tamaa ya pesa akarubuniwa na li- shuga mami!, Sema kwa otee...

Jerry: Haya sawa, kwa ote.

Merry: Enhe nyingine, endelea nakuskilizaa...

Jerry: Sababu nyingine ni ujio wa mgeni kwenye familia, hapa namzungumzia mtoto, yaani, wakati wapenzi wanaishi wawili tu upendana sana, lakini, pindi tu mtoto anapozaliwa upendo upungua kwasababu upendo ule uanza kugawanyika, ila usiseme kwamba naongelea upande wenu wanawake tu hapanaa..

Merry: Enhe, endeleaa tu usijali mme wangu.

Jerry: Sawa mke wangu, basi kinachotokea ni kwamba, mama huamisha nusu ya upendo kutoka kwa mumeo na kwenda kwa mwanae ambaye huwa mgeni mpya kwenye familia.

Merry alihema kidogo, alishusha pumzi kama mtu aliyetoka kupandisha mlima.

Merry: OKE J, mi nitajitaidi kuyazuwia hayo yote, mmh..

Aliehema tena

Na kuhusu mtoto, ha..ha.. hatutokuwa na mtoto maisha yetu yote, tusizae, bora tuishi tu hivihivi wasela.

TUNARUDI MWAKA 2020.

Kwenye maisha kila kitu utokea kwa sababu, na dunia inaweza kubadili matakwa yako.

Ilikua jioni, Merry na Jerry walikuwa mtaani wakipiga misele ya huku na huku kusheherekea mapenzi yao, baada ya kukata kona mbili tatu walikutana na familia yenye baba, mama na mtoto, ni kama falme iliyokamilika yaani ina mfalme, malkia na mwanamfalme.

Ile familia iliwavutia, wakajikuta kama wanadeni, wakajiona kama watu wasiojali agizo la mungu kwa bin adam juu ya kuzaana na kuijaza dunia, waligeuka na kuwatazama tena, mfalme alikuwa amevaa Tisheti yenye rangi sawa na malkia na mwanawake pia, tisheti nyekundu zenye maandishi mgongoni, maandishi yaliyosomeka "KING", "QUEEN", na "PRINCE". Kitu kile kiliwafanya watamani kuwa na mtoto.

Jerry alijihisi kama mtawala asiye na alama wala damu ya kurithi kiti chake cha ufalme pindi mda wake utakapotimia.

walipatwa na wivu uliokumbatiana na tamaa.

Upweke unaweza kuwa sababu nyingine kwa Merry kutamani kuwa na mtoto.

Wakati Jerry yupo kazini, merry alibaki nyumbani peke yake katika lile jumba kubwa akiwa ancheza na midori.

Mpangilio wa majumba katika eneo lile ni wa mbalimbali, Merry inamchukua hata mwezi mmoja angalau hadi kuja kuonana na jirani.

Siku moja Jerry aliporudi nyumbani alimkuta mke wake akicheza na matoi, taratibu J alimkumbatia mke wake, kuanzia pale Jerry akatambua kuwa mkewe ni mgonjwa, anaumwa homa ya upweke, ni ukweli ulio uchi kwamba, upweke ulimzidi merry nguvu, hivyo akatambua kuwa mkewake anahitaji swahiba, anahitaji mtu wa kucheza nae, anahtaji mtu wa kucheka na kuongea nae, anahitaji mtoto.

Lakini, Jerry alihofia mapenzi yao kuporomoka.

BAADA YA MWEZI MMOJA

Merry na jerry wakiwa kitandani wamelala lakini hawajasinzia, huku merry akiugusagusa uchebe wa mumewe.

Merry: Bebi, kuna kitu naomba nikuambiee..

Jerry: Mh, sa wewe ukitaka kuniambia kitu ndo hadi uniombe!, niambie tuu usijali.

Merry, mmh, haya, bebii, mi nina mimbaa...

Jerry alitabasamu na kuzichumu lipsi za merry.

Jerry: Ngoja nifanye masahihisho mke wangu, TUNA MIMBA, sema tuna mimba yaani ote, mimi na wewe, huyo mtoto kwenye tumbo lako ni nusu yako na nusu yangu, sitokuacha uteseke peke yako, najua siwezi kuibeba tumboni lakini nitaibeba kwenye moyo wangu. Nimefrahi, nitabaki na wewe na nitakuwa baba wa chochote kitakachozaliwa.

MAISHA NDANI YA UJAUZITO

Bado wanafraha hata kama mke ni mjamzito, bado wanapendana, labda wataacha kupendana baada ya wawili hawa kujifungua.

Mwezi mmoja, miezi miwili, hadi miezi tisa ilipotimia na mtoto akazaliwa.

BAADA YA MIAKA KUMI.

Hadi mtoto alipotimiza miaka kumi, alikuwa shuhuda wa upendo, alishuhudia jinsi wazazi wake wanavyopendana.

SIKU MOJA USIKU.

Ulikuwa usiku, Jerry na Merry wakiwa kitandani. Jerry alianza kumpapasa mkewe,

Merry: niache bwana, mkewe alifoka, Merry alikataa kushikwa, Jerry alijaribu tena jaribio lile lakini mama watoto wake alikataa katukatu na kuutoa ule mkono wa mumewe kwenye kiuno chake.

Siku ya kwanza, siku ya pili, siku ya tatu Merry aliamua kuama upande wa kitanda ili kuepuka usumbufu wa kushikwashikwa na ba watoto wake. Zamani walilala wakiwa wamekumbatiana mithiri ya ile sanamu ya wapendanao, baadae walilala wakiwa wametazamana sura kwa sura lakini bila kukumbatiana, kisha wakaanza kulala wakiwa wamegeuziana migongo na sasa kila mtu analala upande wake, wanalala ule mtindo maarufu kwa jina la mzunguwanne. Jerry akuwa na budi kuizowea ile hali, ikabidi alale tu kimyaaa...!!!, bila kumbugudhi mwenzie.

SIKU CHACHE BAADAE

Jerry yupo chooni, yupo chooni anapiga puchu, alifanya hivo kila siku, alisubiri tu mke wake apitiwe na usingizi ili aende chooni kujichua. Jerry aliamua kumwambia rafiki yake baada ya kukutana naye huko kwenye dangulo moja lililopo katikati ya mji, alifunguka juu ya changamoto anazokutananazo nyumbani kwake kwa mke wake,

Jerry: Mike, mi nina tatizo

Mike: Sema

Jerry: Ni tatizo tu na mke wangu

Mike: Tatizo gani sasa! mke wako ni mchawi au!

Jerry: Hapana, hataki kushiriki na mimi

Mike: Ahahahah!!!, kwahiyo hamli chakula kwenye meza moja siku hizi?

Jerry: Mike, hamna haja ya kuongea kama watoto, mke wangu hataki kunipa mzigo siku hizi, miezi inakatika sasa, sijaambulia kitu, naishia kukitazama tu kama cha mtoto mchangaa...

Mike: duh!!!, kwahyo unafanyaje siku hizi, unapiga nyeto, au!!

Jerry: ...mh mh...

Mike: Njoo huku, njoo nikuoneshe kitu,

Jerry anaongozana na rafiki yake hadi mbele ya mlango mmoja, wanaingia kwenye chumba kimoja chenye taa zenye mwanga hafifu za rangi rangi ziwakazo kwa kumetameta, zinawaka kwa mtindo wa kuwaka na kuzima. Ndani ya kile chumba kulikuwa na wanawake makahaba, wanaogeuza miili yao kuwa bidhaa. Mike alianza kuwashikashika na kuwatomasatomasa wale machangudoa kama nyanya gengeni, anavua shati yake, nao wale makahaba wanaanza kumpapasapapasa Mike kifuani na wengine wakiingiza ulimi kwenye maskio yake.

Mike alimuomba kigori mmoja amhudumie Jerry ili ayasahau matatizo ya nyumbani kwake.

Mike: We!, mpe raha huyo, mpe vityuu...

Mwanadada mmoja alielekea kwa Jerry, alimvua shati na kuamza kumpapasa kama mtu anayetafuta shilingi kwenye mchanga.

Jerry alionekana kuto kuwa mzoefu na vitu vile, aliisogeza shati yake kwa mabega na kufunga shikizo, alianza kutafuta namna ya kutoroka. Baada ya mda Jerry alitoroka baada ya kudanganya kuwa anaenda mariwato. Alitoka mikononi mwa wale watu na kurudi nyumbani kwa mkewe. Alipofika nyumbani alikuta chakula kipo juu ya meza, kimeshaandaliwa vizuri tayari kwa kuliwa. Alitulia kidogo kabla ya kuanza kufunua na kuanza kula taratibu huku akionekana kuwa kwenye kisima kirefu cha mawazo. Alimega tonge mbili tatu na kunawa, aliingia chumbani kwake na kumkuta mkewe akiwa amelala fofofo. Alichukua shuka na kumfunika vizuri sehemu yake ya miguu aliyoiacha wazi kisha na yeye kulala upande wa miguuni mwa mkewe.